Sam GM
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 535
- 30
Kuna huyu jamaa rafiki yangu mara kwa mara amekuwa akija kutafuta ushauri kwangu, mara ya mwisho kaniambia kuwa kila akilala na mkewe anawaota ma-ex wake nikashindwa kumsaidia, juzi kaja kuniambia kuwa kwa wiki mbili mfululizo amekuwa akiwaota ma-ex wake one after another mpaka akamwambia my wife wake basi hawezi endelea na ndoa. kisha kaja kwangu kuniuliza kama kafanya jambo la busara kumuacha mama au kakosea, nimsaidie vipi?