AKIKI au AQEEQ: Jiwe/kito chenye nguvu ambacho utatamani kuwa nacho Baada ya kusoma hapa!

Rakims

JF-Expert Member
Jun 4, 2014
4,982
4,481
JIWE LA AKIKI



banded-agate_1331x.jpg




Katika makala hii nitakuelezea kuhusu kito chenye nguvu za miujiza zilizojificha ndani yake na baraka Kito cha Aqeeq faida zake ni nyingi na kipo katika historia mbalimbali na maarufu kama pete iliyowahi kuvaliwa na Mtume Muhammad Swala Allahu 3aleyhi wasalam.

Nitakuelezea nini Aqeeq na historia yake ni ipi na inafaida zipi ambazo huenda na wewe ukazipata vilevile baada ya kuvaa;
Kwa haya na mengineyo unaweza kuendelea kuperuzi kupitia blog yangu bonyeza hapa chini:

Rakims Spiritual

Kito cha Aqeeq ni moja kati ya vito bora zaidi vinavyouzwa ulimwenguni kote,
kito hiki maalum pia hufahamika kama Agate Kingereza na عقيق نبات Kiarabu kiswahili nadhani wanaita AKIKI pia,
Pia kama utahitaji naweza kukuagizia kutoka Turkey au Yemen na vile vile unaweza kuagiza mwenyewe mtandaoni ikiwa unajua utaratibu na usifanye pupa katika kuchagua maana wengi huuza AKIKI ambazo ni FEKI. Pia unaweza kuagiza mwenyewe katika website inayoaminika ya OTTOMAN

Vyovyote iwezekanavyo unaweza kupata kilicho asili lakini kwa hali ilivyo sasa hivi duniani na katika ulimwengu wa masoko ni rahisi sana kupata vya bei rahisi na vinapatikana katika maduka ya mitandaoni maarufu kama Ebay na Aliexpress.

Baada kupata maombi mengi ya kuelezea kuhusu vito vya pete za nyota kutoka kwenu nimeona pia nianze kwa kuelezea vile ambavyo ni vikubwa katika historia na vinavyoweza kumfaa kila mtu.

Pia katika maelekezo haya nitakueleza ni jinsi gani unaweza kupata hiki kito kikiwa cha uhakika na sio vyupa au zircon zinazosambazwa mitandaoni na kutapeli watu. Pia nitakuelekeza rangi sahihi ya kito hiki na faida zake kwa ujumla.


KITO CHA AKIKI NI NINI

Kwanza kabisa nitakueleza kabisa jiwe hili ni nini?

Jiwe la AKIKI ni kito ambacho kipo aina nyingi tofauti.
Ni madini yanayotokana na Familia ya Quartz; ambayo pia nimeeleza inajulikana kama AGATE Kingereza na pia kama Achates, Aqiq, Akik, Aqiq au عقيق نبات katika lugha tofauti.

Inawezekana pia ukakuta kito hiki kikiwa na rangi tofauti,
Vyovyote vile lakini maarufu zaidi huwa ni Rangi nyekundu,Kijani na Damu ya mzee.
Zile nyekundu ni Maarufu zinaitwa AKIKI za YEMEN lakini hii si sawa ni vile tu mtu akitaka kusifu kitu chake kuwa cha asili ndio anasema hivyo
yani:
"hii yenyewe kutoka sehemu fulani"
kwa sababu hiyo ndio inaitwa AKIKI asili ya Yemen.

Kama nilivyoelezea juu, ni jiwe ambalo ni maarafu na unaweza kupata sehemu yoyote duniani lakini ukihitaji AKIKI za asili ni bora zaidi ukapata kutoka Yemen kwa sababu zenyewe huwa na Quality kubwa.

HISTORIA YA JIWE LA AKIKI:

Jina lake linatoka katika kisiwa kikubwa zaidi katika Bahari ya Mediterania na moja ya mikoa 20 ya Italia.

Kinachoitwa Sicily na katika mto wake wa Achetes River. ambapo jiwe la kwanza la AKIKI lilipatikana huko.

Siku hizi mto huo unajulikana kama Dirillo au Acate. Pia katika kiarabu mtu huo unaitwa kama Wadi‑Ikrilu ambayo maana yake ni mto wa Acrille ambapo ilikuwa koloni la Ugiriki la zamani lililoko katika mkoa wa kisasa wa Ragusa,
Pale watu walipojua na kuelewa kito hiki cha thamani wakaanza kukitumia kama mapambo na kubeba na kuanza kuchunguza kutafuta zipi ambazo ni nzuri zaidi Duniani katika maeneo tofauti tofauti.

Hivi leo AKIKI nzuri unaweza kuzipata Yemen na ambazo zinaitwa Yemen Aqeeq. Kutokana na faida ya jiwe hili na usambazaji wake kuwa hautoshelezi baadhi ya Makampuni yakaanza kuhamia China kwa ajili ya kutafuta uzalishaji wa Jiwe hili na ambapo utakuta jiwe hilo linafanana sana na AKIKI lakini halina thamani ya uhakika.

Hadi leo kwa maelfu ya miaka AKIKI imekuwa ikitumika kama kito katika Mapambo na zilikuwa ni fashion za zamani kwa watu.
Leo hii watu wengi hutumia zaidi katika pete,kidani,tasbihi na mapambo mengine.

Faida za jiwe la AKIKI.

Jiwe hili lina nafasi muhimu katika dini ya Kiislamu. Ni jiwe maalum kwa Waislamu.

Pia kama ilivyokuwa maarufu mtume Mohammad Rasool Allah (S.A.W.) alikuwa na pete iliyokuwa na kito cha AKIKI. Mfano wake ni pichani:


Maelezo haya yametoka katika Hadithi.

Kwanini uvae jiwe la Akiki?

Aqeeq ni jiwe maalum sana kwa dini ya kiislamu na kwa waislamu.

Lakini pia ni muhimu kwa dini zingine kwa kuwa ni kito cha zamani sana katika miaka iliyopita, na kilichokuwa kikitambulika tangu enzi za Hz. Adam.
Inawezekana vile vile ukapata akiki katika rangi tofauti Nyekundu,Kijani,nyeupe,maziwa,njano,Kijivu na nyeusi.

Pia ina zaidi ya aina mia moja lakini yenye nguvu zaidi ni Akiki za Yemen na ambazo ni adimu.

Yemeni Aqeeq zina rangi damu ya mzee lakini iliyokoza zaidi kwa wekundu, na ambazo ni ghali zaidi na ngumu kupatikana.

Siku hizi watu wanauza pete yenye vito vya Aqeeq kama Yemen katika tovuti za Ebay, etsy n.k

kwanza kabisa kama unavaa pete yenye vito vya aqeeq kwa sababu ya kupata faida, unapaswa kuwa na jiwe halisi, ambalo sio rahisi
kupata kwa bei hio kwenye maduka ya mtandaoni.

Hapa nitaelewaelezea faida kumi 10 za kuvaa kito cha Aqeeq:

FAIDA 10 ZA KUVAA AKIKI: Kutoka dhehebu la mashia

1: kuvaa kito cha Aqeeq inakuletea faraja katika moyo na ni nzuri kwa nuru ya macho na inasaidia kuondoa unyogovu,huzuni na msongo wa hasira. Jiwe hili linachukua miale ya Jua na kupitisha nuru yake na kufyonzwa na kuingizwa katika mwili wako.
Pia ni nzuri kwa afya yako hofu yako na upweke ulionao na inakuongezea nguvu na ujasiri.

2: Kama vile inavyoaminika kiislamu kuna milima ya Akiki mbinguni. Milima hii inaaminika kukinga Hekalu la Bibi Fatima na Imam Ali (katika imani za mashia) ambayo milele inamtukuza na kumsifu Allah (SWT).

3: Kama ukivaa jiwe la Akiki kwenye pete au mapambo mengineyo (kubeba kirahisi pia unaweza kubeba jiwe peke yake) basi rizqi(kipato chako) kitaongezeka. Na utakuwa umejikinga na uchawi,hatari na Ajali na pia itakukinga na maadui zako.

4:Mtume wetu mtukufu alisema pia "yoyote mwenye kuvaa Akiki basi matumaini yake yatafanikiwa" Hadithi kutoka kwa Salman Farsi ilisema kwamba mtume wa mwisho alimwambia Imam Ali avae pete katika mkono wake wa kulia nae atawekwa kwenye orodha ya Muqarrabeen (yani waliokaribu na Allah).
Imam akamuuliza mtume hao Muqarrabeen walikuwa ni kina nani?ambapo mtume akamjibu walikuwa ni Jibriil(Gabriel) na Mikaiil(Michael).
Nae Imam akauliza ni jiwe gani natakiwa kuvaa?
Mtume akamjibu Jiwe la Akiki, kwani jiwe hili jekundu laini lilikuwa limekubali Upweke wa Mwenyezi Mungu, Mitume wake na Utume wa mtume wake wa mwisho na Kiongozi Imam Ali ibn Abi Taleb.

5: Kwa kito cha Akiki: Imam Ali ibn Abi Taleb alisema ukivaa kito hiki katika pete, basi utakuwa umebarikiwa na utakuwa umeokolewa kutokana na mateso.

6: Faida nyingine kuhusu Akiki Imam Jaffar e Sadiq anasema ukisali ukiwa na jiwe la Akiki ni mara 40 ya bila kusali nalo.

7: faida nyingine ya Akiki; Imam Musa e Kazim anasema ni sawabu(malipo) makubwa kutumia tasbihi ya Akiki.

8: faida nyingine Imam Muhammad Taqi alisema ukivaa jiwe hili basi litakuondolea umasikini na kufuta tofauti katika moyo.

9: Kwa Yemeni Aqiq; Imam Muhammad Baqar alisema kama mtu atavaa pete yenye kito hiki na akageuza mkono wake mbele na kukitizama na kusoma Surah Qadr (sura ya 97), Allah atamlinda siku nzima kutokana na majanga ikiwa yatatoka mbinguni au Ardhini basi atalindwa hadi jioni na marafiki wa Mwenyezi Mungu watamuongoza.

10: Imam Reza pia alisema “Yoyote atakae vaa pete yenye kito cha Akiki. kwanza kabisa hata kuwa mwenye kuhitajia na pili majaliwa yake kwa Mwenyezi Mungu yatakuwa mazuri".

Kwa faida za kawaida tofauti na ushia bonyeza link hii chini:

Rakims Spiritual

Wapi unaweza kupata Akiki ya kweli?

Jiwe hili kulitambua original na feki sio rahisi ni ngumu kidogo na hususani kama hujui kutofautisha vito zaidi ya rangi tu, kwako itakuwa ngumu kupata akiki ambayo ni sahihi na unaweza kuangukia kupata feki unless utafika kwa mtu ambaye ana uzoefu na mawe na pia kama ni Sonara basi awe ni mwenye ujuzi na mawe haya wengine nao ni wezi tu kama waliopo mitandaoni.
Na vile imekuwa ni maarufu kila mtu anataka kuvaa kama sunna basi wengi wao unakuta wanavaa ushanga na machupa kwenye pete zao bila kujua na kuaminishwa ni Akiki nao wakakubali kisa tu anaeuza ni Muhindi au Mwarabu.

Kama utahitaji kuijua Akiki sahihi basi naweza kukushauri jambo.
Unaweza kuwasiliana nami kupitia WhatsApp ili kuweza kuagiza kutoka kwangu lakini pia kama una jamaa ambao wapo Yemen unaweza kuwaagizia au Abu Dhabi na Turkey lakini China haijarishi utauziwa bei gani ni Feki tu na ukikuta ina uhalisia basi jua ni ya maabala.
Na vile vile unaweza kuagiza kutoka Ottoman website niliyoweka hapo juu wewe mwenyewe au unaweza kujaribu huko huko mitandaoni bahati yako.

Akiki zinazotoka Yemen bei zake ni ghali kidogo tofauti na vito vingine.
Na kwa sasa soko lake lilivyokuwa adimu basi Akiki nyingi za kuokota okota ukivaa utakuwa huna tofauti na mtu aliyevaa pambo tu na haitakunufaisha chochote.
Unaweza kuwasiliana nami nikakuagizia nilio waagizia wana fahamu kama itakuwa ni sahihi kwao wakisema hapa basi naweza kuonyesha Screenshot zao ieleweke nikikuagizia sifanyi kazi ya kanisa utatakiwa kunilipa pia kwa maana likitokea tatizo hasara ni yangu.

Vile vile si rahisi kujua ni ipi Akiki ya kweli ikiwa teyari ipo kwenye pete nashauri kama unaagiza basi agiza kito peke yake bila pete ili ikifika unaweza kuipima na kujua vema.

Na vile vile ni bora zaidi kuagiza sehemu ambapo wanatoa certificate za ununuzi kama vile Aqeeq Stone Jewellery.

Aina za Mawe ya Akiki.

Mawe haya huwa katika ukubwa tofauti na rangi tofauti inategemea na uhalisi wake.

Maarufu sana kama niivyosema ni hiyo damu ya mzee nyekundu inayotoka Yemen ambayo vilevile hutambulika kama Yemen Aqeeq.


Pia kuna Akiki ya kijani na ambayo ni maarufu vile vile kutokana na faida zake. Ina faida nyingi na inasaidia vile vile kuweka usawa katika akili yako ni kuondosha msongo wa mawazo.
Pia ni nzuri kwako kama unahitaji kwa ajili ya utulivu na Furaha.


Pia kuna Sulemani Aqeeq ni tofauti kabisa na Akiki hii nazo zipo na rangi zake na baadhi ni maziwa,brown,kijivu na nyeupe.
Nyeupe zake zinaitwa Akiki nyeupe lakini si kweli hizi ni madini mengine na tofauti na Akiki na kwa jina lake huwa ni Onyx Maarufu sana huwa na rangi nyeusi.

Nyeupe yake haina faida sawa na Akiki.

kwa hivyo kuwa makini kama unahitaji kununua kama utahitaji nyeupe yake vile vile unaweza kuwasiliana nami unaweza pia kuwasiliana nami kupitia simu namba +255 783 930 601 e-mail yangu

rakimsspiritual@gmail.com


Sheria za kuvaa kito hiki?

Sheria za kuvaa kito hiki vile vile ni muhimu na watu wengi hupenda kuuliza sheria na masharti ya kuvaa pete.

Kiukweli katika kuvaa jiwe hili hakuna masharti yoyote ikiwa limetengenezwa kwa nia ya kawaida lakini kama umelitengeneza kwa nia tofauti basi ujue sheria zipo za kufuata ili kuweza kufukia unayotaka kwa sababu ya kuvaa pete hiyo.

Ni nzuri zaidi ukivaa muda wote ili kupata faida zake haraka na kwa urahisi zaidi na yeyote anaweza kuvaa sio kwa ajili ya watu fulani fulani au kwa imani fulani.

Jambo muhimu ni unapokuwa umevaa basi jiwe hili liweze kugusa vema ngozi yako ili kuweza kupata faida zake.

Hivyo hakikisha kama ni katika pete au kidani basi nyuma kiwe wazi ili kuweza kugusa ngozi yako na kuweza kupata faida zake.

Akiki ni muhimu kwa waislamu na vile vile unaweza kusoma soma google utakutana na Akiki za Shia au Akiki za Sunni kuna makala nyingi na faida nyingi zimeelezewa huko katika baadhi ya websites.

Ni muhimu kuvaa pete hii kwa mashia na Wasunni vile vile kutokana na hadithi za mtume Mohammad Rasool Allah (S.A.W.) zilizotaja kuhusu mawe haya.

Siku hizi zipo nyingi hizi bracelets na pete zenye mawe haya na zinaweza kukugusa ngozi vyovyote utakavyo.


Katika kidole gani uvae?

Kama nilivyosema hakuna sheria ya kuvaa hii pete lakini ni sunna kuvaa mkono wa kulia katika kidole cha pete lakini unaweza kuvaa kidole chochote unless unataka ziada basi unaweza kuwasiliana nami.

Mambo mawili tu muhimu ya kuzingatia;

1- Liwe ni jiwe Asilia

2- Liguse ngozi yako

Kwa jibu rahisi vaa utakavyo unless unahitaji zida unaweza kuwasiliana nami.

Bei za Mawe ya Akiki

Bei zake hubadirika kulingana na rangi na uhalisia wake na mng'ao ikiwa pamoja na usawa wake na ukubwa bila kusahau umbo lake.

Unaweza kukuta nyingi Ebay au Etsy zenye gharama nafuu ya $40-$60 pamoja na usafirishaji wa bure ambayo ni sawa na TSH 94,000/= - 141,000/= hizi bei sio za kweli na mara nyingi ni feki.

Hata kama ipo kwenye pete ya fedha.

Nyingi za kichina ni feki na zina rangi nyekundu na vingine unakuta ni kati ya $1-$2 kwa jiwe hizi ni plastick au vigae vya kuokota.

Kwa upande mwingine kuna baadhi ya kampuni zinauza Pete hizi katika Fedha katika muundo mzuri kwa $70-90.

Hizi pia ni feki lakini wanajaribu kuvutia wateja kwa design na ukubwa wa bei.
Akiki Original bei yake unaweza kukuta inaanza $80-120 na hii ni kwa grade AAA ya mawe.

Na ukikuta imetengenezwa kwa mkono kwenye silver na Imetoka Yemen basi bei yake ni kati ya $120 – $200 na inategemea rangi na ukubwa na ubunifu wake.

Kama unahitaji unaweza ukawasiliana nasi kwa simu namba +255 783 930 601 kwa kupata Original kutoka kwangu.

Pichani ni mbili nilizo nazo kwa sasa:



Moja ya Oman na nyingine ni Yemen yenye picha ya ndege.

Kwa haya na mengineyo:
Tembelea:

Rakims
 
Brother nakutafut sana ig i texted you Facebook too even in dm en kwny youtb chanel yak plz reply my dm or important thing your no
 
Brother nakutafut sana ig i texted you Facebook too even in dm en kwny youtb chanel yak plz reply my dm or important thing your no
Unaweza kuwasiliana nami kupitia WhatsApp number 0783930601.

Sijaweza kupokea ujumbe wako
 
Back
Top Bottom