Akigundua mwafrika ni uchamwi akigundua mzungu ni Sayansi!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Akigundua mwafrika ni uchamwi akigundua mzungu ni Sayansi!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Anold, Mar 11, 2011.

 1. A

  Anold JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 297
  Trophy Points: 180
  Toka mzee anayesadikiwa kuwa anatoa dawa yenye uwezo wa kutibu magonjwa yaliyoshindikana mengi yamekuwa yakisemwa. Pamoja na mzee huyo kujaribu kueleza chanzo cha upatikanaji wa dawa hiyo bado wasiwasi na mashaka yanaendelea na kila mtu anataka kujua kuwa ni kweli dawa hiyo inaponywa au vipi. hii ndiyo tabia ya kiafrika ya kutoamini mambo yanayomhusisha Mungu, wengi wanamtafuta sana Mungu ila ndani ya nafsi zao kuna kutokuamini na mashaka juu ya uwezo wa Mungu na hili linakuja kupata nguvu hasa ikitokea anayesimama na kukiri kuwa anaugunduzi fulani ni mtu wa kawaida. Kama tukio la Loliondo lingekuwa limetokea katika nchi za ulaya watu wengi wangeamini na kumshukuru Mungu kwa dawa hiyo, wengi wamekuwa wakiamini kuwa mwafrika hawezi kugundua chochote na kamwe ugunduzi wake daima utawekewa walakini, waafrika wengi wamekuwa akutukuza wazungu na kuamini kila kitu wanachokifanya. Si katika mambo ya Loliondo tu ila waafrika wengi hawaamini watu wao kuwa wanaweza kufanya chochote, ndio maana hata katika nyanja ningine kama michezo n.k wengi hawaamini kuwa watu wetu wanaweza, daima wazungu ndiyo wanaonekana kuwa wanauwezo wakufanya kitu chochote na kufanikiwa, huo ni umaskini wa fikra. Huu ni ukoloni wa fikra na ni mbaya zaidi hata ule wa kuchapwa viboko ili kuvuna mkonge.
  Mchungaji huyu kama ingekuwa yupo katika nchi za wenzetu kwao ingekuwa faida kubwa kwa jamii yote maana wangefanya mazingira ya kumtia moyo na kufanya jambo hilo liwe na faida pamoja na heshima kwa taifa. Kwetu si hivyo kwani pamoja na watu wengi kukiri kuwa wamepata nafuu baada ya kutumia dawa hiyo watu wengi wamekuwa wakitoa maneno na kejeli bila hata kufanya utafiti japo kwa hao wagonjwa waliotumia hiyo dawa. Baadhi ya Viongozi wa dini hasa wale wanaojiona ni wa kiroho kupita wengine wamekuwa wakisaidia kumponda mzee huyo kwa kusema mungu hawezi kusaidiwa na dawa maana imani walionayo ni kuwa kila kitu cha mungu lazima kifanyike katika njia ya muujiza, wachungaji wa namna hiyo ni wale ambao wanajua kuhubiri tu ila hawajalisoma neno la Mungu kwa kina maana katika biblia kuna maeneo mengi ambayo watumishi wa mungu wa zamani walifanya huku wakitumia vitu ambavyo katika jamii ya sasa inayojiona ni bora ingetafsiri kuwa ni ushirikina, hebu fikiria suala la neemani kuoga mara saba mtoni, Yesu kumpaka mate kipofu na kuona, n.k mambo kama hayo yangefanywa na mtumishi wa leo hasa wa kanisa lisilo na sifa ya kuitwa la kiroho mtu huyo angeitwa mchawi. Tatizo kubwa ni kuwa wanadamu wengi hudhani kuwa utendaji wa Mungu ni sawa na mwanadamu wakawaida hivyo kila kitu kinachotokea lazima kiwe kinaendana na mtazamo wa akili zao huu ni upotevu usioelezeka. Kama ugunduzi huu ungefanywa na Mzungu kila mtu angekubali na kuita kuwa wamebobea katika sayansi lakini kwakuwa Ugunduzi huu umefaywa na mtanzania mwenzetu tena mzee aliyechoka tena sio kutoka kanisa la kiroho hawakubali wanamwita mchawi hawaamini kuwa Mungu anaweza kumtumia!!!
   
 2. A

  Anold JF-Expert Member

  #2

 3. L

  Leornado JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kunya anye Mzungu akinya mzawa kaharisha.

  Yupo wapi yule jamaa aliebuni gari Zanzibar na Karume alionyeshwa kipaji kile?

  Sana sana mafisadi wanatathmini jinsi gani wamrubuni Babu ili wajifaidishe wao kupitia Babu manake mia tano anayotoza ni kidogo sana.
  Huoni kina Kakobe wanavyomkejeli wakati wao kama wachungaji wangekuwa mstari wa mbele kufurahia muujiza huu kupitia mchungaji huyu.
   
 4. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  tushakuwa corrupted na uzungu ndo maana hatutakaa tuendelee hata siku moja
   
 5. M

  Mpasi New Member

  #5
  Mar 11, 2011
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Cha kushangaza pia ni kuwa Babu wa loliondo hakuwalazimisha watu kwenda wala hakupiga mbiu kuwaambia watu waende...waliopona ndo wametoa ushuhuda,wacha kila mtu ajaribu kwenda...HAKUNA MTU ANALAZIMISHWA JAMANI:panda:
   
 6. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  mkuu, sisi tumejaa moyo wa kujipenda kupita kiasi, ikitokea mtu anaonekana kukubalika basi tunamfunika kwa nguvu zote!
   
 7. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Babu huyu anatumia imani kutibu magonjwa sugu ya kisayansi,tiba ya magonjwa ya kisayansi ina utaratibu wake wa kuthibitishwa na utaratibu huo ni wa kisayansi na si vinginevyo.hatuwezi kuamini kuwa dawa hii inatibu magonjwa haya yaliovumbiliwa kisayansi ispokuwa pale itakapofanyiwa utafiti na kuthibitika kuwa tiba halali.sioni ni kivipi watafiti wa kiafrika wanapuuzwa,je ni kweli hakuna wanasayansi wavumbuzi ambao ni weusi?hakuna PHD holders kwenye fani ya sayansi?evidence iko wapi inayoonyesha mwanasayansi wa africa amepuuzwa?
  Kwa sasa namuona mchungaji huyu ni mbabaishaji mpaka tutakapothibitisha dawa yake inaponyesha.tusitumie bibilia kupotosha!
   
 8. Tram Almasi

  Tram Almasi JF-Expert Member

  #8
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 755
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hapooo sasa,huyu babu amekuwa na anatoa huduma bila kujitangaza au kuita watu waende kwakwe kama ilivyo kwa viongozi wengine wa kiroho ambao hutumia vyombo vya habari kujitangaza au kutangaza kile wanachodai ni mafanikio ya tiba zao kwa njia ya maombi. Nimewahi ona ktk TV kiongozi mmoja wa kiroho anatangazia umma kwamba ameweza kumtibu mgonjwa wa kansa ya damu!
  Ninachojiuliza mm,hili pia linahitaji udhibitisho wa kisayansi au ni yale ya babu tu?
   
 9. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #9
  Mar 11, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Hatupendani. Roho za kwanini zinatusumbua.
  Africa kuna wavumbuzi wengi tu ila wanapotezewa.
  Na huyo babu angekuwa anatoza hela nyingi mate yangewakauka kwa kuchonga.
   
 10. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #10
  Mar 11, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  kweli methali zinatimia ss
   
Loading...