Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Mwaka 1975 Mzee Mwinyi alijiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani, baada ya kutokea kashfa kule Shinyanga. Lakini miaka 10 baadae akawa rais wa pili wa Tanzania. Edward Lowassa alijiuzulu uwaziri mkuu mwaka 2008 baada ya kashfa ya richmond kuhusishwa na utendaji wa ofisi ya waziri mkuu. Lakini ni Lowassa huyo huyo aliyepata kura milioni 6 kwenye uchaguzi wa mwaka jana.
Waziri wa nishati Profesa SospeterMuhongo alijiuzulu baada ya kashfa ya escrow kuhusishwa na ofisi iliyokuwa chini yake. Leo waziri Muhongo kapewa tena ofisi ile ile na ninaamini rais aliyempa wadhifa huo ameamini katika utendaji wake. Lakini naona kuna nguvu kubwa inayotaka rais amwajibishe waziri Muhongo kwa sababu ya sms aliyoituma kwa yule Mama aliyekuwa na dhamana ya kusimamia mabomba ya mafuta kule bandarini. Waziri hafukuzwi kazi kwa ushahidi wa sms.
Kama Mzee Mwinyi alisamehewa na akaja kuwa rais kwa miaka kumi, kama Mzee Lowassa alisamehewa na akaja kupigiwa kura na watanzania milioni 6, Muhongo ni nani mpaka aonekane ni kiumbe kutoka sayari nyingine?. Hizi nongwa, zinatupeleka wapi watanzania?.