Akifanya mazuri tupongeze sio kusema mabaya tu huu ndio uungwana

Andie

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
713
1,641
Wanajukwaa salaam,
Uungwana ni kua mkweli kama tuna msema Sizonje kwa mabaya kama kuminya demokrasia, kutapeli wakulima wa kerosho, kutoshaurika, nk naomba pia tuseme mazuri yake.

Katika kuinua uchumi kaongeza kodi mpaka wafanyabiashara wamepukutika mitaji, tumpongeze jamani.

Katika kukuza uwekezaji kawateka wazekezaji mf MO na Manji kupelekea wawekezaji kuikimbia nchi kama Manji na wengine kina Kishimba nk. Gazeti la The Economist likatubainisha kati ya nchi zisizo salama kwa uwekezaji. Jamani tupongeze.

Katika kujali raia, tumeshuhudha maiti zikiokotwa kwenye viroba bila kuwepo na tamko lolote la kulaani vitendo hivi, jamani tupongeze.

Katika kujenga umoja wa kitaifa Sizonje kateua watu wa kanda yake kwa upendeleo wa hali ya juu jamani hivi na hili hamuoni kua kachangia kujenga umoja wa kitaifa ?

Katika kuheshidu watu na utu wao, kajitahidi sana kutekeleza hili kwa kuwadhalilisha wanawake kwnf kuwauliza wamepanuliwa wapi, je wanataka wapanuliwe ? Kaulh hizi ni za kiungwana dhidi ya utu. Tupongeze.

Katika kupambana na ufisadi, jamani achana na vile vibilioni vya EPA sijui ESCROW hapa ni trillion 1.5 ziliyeyuka bila kujua zimetowekea wapi na wanaohoji wanakula risasi, jamani hivi kweli kabisa kuna asieona jitihadi hizi za kupambana na ufisadi ? Acheni unafiki bwana pongezeni.

Katika kuheshimu maamuzi ya bunge, sisi hatujali bajeti iliyopitishwa hapana tunachota mabilioni na kujijengea uwanja wa ndege wa kimataifa ambapo ni ndege yake tu ndo inatua kama alivyofanya Mobutu kijijini kwake. Jamani hata na hili hamuoni kua tunaeshimu bajeti ya bunge, pongezeni.

Katika kuheshimu mahakama kama muimili wa serikali tupo vizuri. Mahakama ikizuia bomoa bomoa sisi hatujali tunabomoa na ninaomba mpongeze acheni unafiki ebo mazuri yote haya hamuoni ?.

Katika kujali wafanyakazi tumewajali kweli kweli, miaka mitano bila kuwaongeza mishahara wala kumapandisha madaraja. Jitihada zetu kwa kweli zimetukuka naomba mpongeze.

Katika kuwa wanyenyekevu, pia tumekua wanyenyekevu sana mpaka tumetamka kua sisi ni mawe hasa hata tukifa Mungu hawezi kuwaongoza malaika vizuri sisi ndo tunafaa kuwaongoza malaika. Pongezeni mliokaa huko nyuma.

Katika kujali rasilimali zetu, jamani kaakiba ketu pale hazini tunakachota na kughalimikia misafara ya magari 75 unaona tunahitaji pongezi.

Kwahaya yote jamani mimi binafsi naweka wazi nitamchangua Sizonje, narudia kura yangu kwa Sizonje nitamchangua yeye ila iwapo tu nitaokotwa kwenye kiroba changu ufukweni ila nikiwa timamu hapana hata kama nitabaki peke angu siwezi kumchagua Sizonje.
 
Mlisha ishiwa Vyakuongea
Mata Sajiri Id kumi kumi
Lakini Wapiga Kura wapo pale pale
Kura yako ni moja tu
Mpo wachache kama Pundamilia Weupe Tanzania
Na Hamtoshi hata kuzamisha mtumbwi wa Gogo la mhama.
Fikirieni 2025 kwa mwaka huu mnalo
Mmekalia ukuti wa moto
 
Mlisha ishiwa Vyakuongea
Mata Sajiri Id kumi kumi
Lakini Wapiga Kura wapo pale pale
Kura yako ni moja tu
Mpo wachache kama Pundamilia Weupe Tanzania
Na Hamtoshi hata kuzamisha mtumbwi wa Gogo la mhama.
Fikirieni 2025 kwa mwaka huu mnalo
Mmekalia ukuti wa moto
Kwakua wapiga kura kidogo ndio mkaweka SIKU MBILI ZA UPIGAJI KURA
 
Mlisha ishiwa Vyakuongea
Mata Sajiri Id kumi kumi
Lakini Wapiga Kura wapo pale pale
Kura yako ni moja tu
Mpo wachache kama Pundamilia Weupe Tanzania
Na Hamtoshi hata kuzamisha mtumbwi wa Gogo la mhama.
Fikirieni 2025 kwa mwaka huu mnalo
Mmekalia ukuti wa moto

Kama mnauhakika na ushindi, unapotezaje muda wako kujibizana na mliowashinda?
 
Sawa kungwi wetu. Sizonje anatembea na tbc utadhani ni kopo la chooni kwake. Kila akienda kujisaidia lazime alikute. Jamani tumpongeze
 
Mama yangu amehusikaje humu nilita nikutukane ila nikagundua wewe nyumbu pita tu na unyumbu wako.
 
Back
Top Bottom