Akidi inakuwaje wakati wa kupitisha miswada tukikumbuka mwongozo CYBERCRIME ACT

kuku dume

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
414
62
Sikuwahi kufuatilia upitishwaji wa sheria lakini ile ya juzi nilifuatilia sababu hasa ikiwa ni kwamba mifumo ya kompyuta na data za kidigitali zinayahusu sana maisha yangu. Niliifuatilia na niliona sheria ngumu sana ikitungu. Nilichonifanya nifuatilie pia ni vile nilipata mswada, nikausoma na kwa bahati mbaya nikabakiwa na mkanganyiko.
Pamoja na marejebisho lakini Mimi ninatamani kujua jambo.
Msinicheke wala kunishangaa maana nimekwisha kuwaambia kwamba Mimi ni mgeni sana kwa sheria ingawaje naipenda sana sheria takatifu ya Mungu isiyo na mawaa(Kutoka 20:1-17, Kumbukumbu la Torati 5, 1Yohana 2:3-4).
Juzi wabunge waliniacha na utata.
Nimekuwa kiongozi kanisani kwetu na kikao hakianzi bila akidi kutimia.

Juzi kuna mbunge aliomba muongozo wa akidi tena akasema jambo lililokuwa likifanyika linayagusa maisha ya watu.
Nina wasiwasi kama nilisinzia lakini mpaka Waziri Mkuu anasimama sikusikia majibu.

Jambo hili likoje kwa anayejua?
 
Back
Top Bottom