Jembajemba
JF-Expert Member
- Feb 3, 2007
- 260
- 32
WAKATI moto wa sakata la utata wa kampuni ya kitapeli ya Richmond ukiendelea kuwaka, huku Bunge likisubiri kwa hamu hatua zitakazochukuliwa dhidi ya watuhumiwa, bomu jingine la ufisadi mkubwa uliofanyika kwenye akaunti ya Madeni ya Nje ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) limelipuka kufuatia vigogo kadhaa Serikalini wakiwemo wastaafu kubainika walinufaika kwenye ufisadi huo.
Habari za uhakika kutoka vyanzo vyetu ndani ya Serikali viliambia Majira Jumapili kwamba tayari Serikali kupitia vyombo vyake vya uchunguzi kwa kushirikiana na mataifa mbalimbali imegundua nyumba na hoteli za kifahari zinazomilikiwa na viongozi wa Serikalini, wafanyabiashara maarufu na viongozi mashahuri wastaafu walionufaika kwa namna moja au nyingine na ubadhirifu wa sh, bilioni 133 za akaunti ya EPA.
Miongoni mwa mambo yaliyosaidia kubainika kwa mali hizo ni baada ya baadhi ya mataifa ya nje kuihoji Serikali ya Tanzania juu ya uwezo wa viongozi hao kuzimiliki.
Uchunguzi wa kina na uliopata uthibitisho kutoka kwa maofisa wa ngazi muhimu wanaojua mchakato wa chini kwa chini unaofanywa kufuatilia zilikopelekwa fedha hizo, pia umeeleza kuwa kuna mabilioni ya fedha za mafisadi hao zimenaswa kwenye akaunti mbalimbali za nje.
Katika Uchunguzi huo nchi zilizogundulika kuwa watuhmiwa wamewekeza miradi mbali na fedha ni pamoja na Uswidi, Marekani, Ubeligiji, Dubai, Afrika Kusini na nchi kadhaa zenye ushirikiano wa kibiashara na Tanzania.
Mimi nawashangaa watu wanaohofia taarifa ya uchunguzi wa Richmond, wangejua kilichomo ndani ya taarifa ya EPA wasingezungumza, ninaamini wananchi wakijua majina yaliyomo kwenye taarifa ya EPA wangetaka wawekwe kizuizini moja kwa moja wakati uchunguzi ukiendelea.
Unajua wakati Rais alipozungumza kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi hakutaja majina ya vigogo waliohusishwa, ni majina yanayotisha, wamo viongozi waandamizi wakiwemo Makatibu Wakuu wa Wizara kadhaa walioko Serikalini na waliostaafu," kilisema chanzo chetu.
Habari hizo zilieleza kwamba licha ya vigogo wa Serikali pia wapo wafanyabiashara maarufu nchini huku baadhi yao wakiwa tayari wametajwa kwenye ripoti ya Richmond.
Uchunguzi wa Serikali umefanyika kwa siri kubwa, ndio maana hata Bunge ilipoomba ripoti hiyo Serikali haikutaka kutoa maelezo zaidi kwani kufanya hivyo kwa sasa kungevuruga uchunguzi unaoendelea, Serikali imeomba nchi kadhaa kutoa ushirikiano na tayari nchi husika zimeitikia kwa sharti kwamba iwe siri kubwa, kiliongeza chanzo chetu na kuthibitisha kuwa tayari baadhi ya akaunti hizo zimefungwa.
Pamoja na taratibu zingine Serikali inafanya uchunguzi kujua namna watuhumiwa hao walivyopata fedha zilizoko kwenye akaunti zao za nje pamoja na uwezo wa kujenga nyumba na hoteli za kifahari ambazo hata nchi husika zinashangaa uwezo wa Watanzania hao.
source:
http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=5704