Akaunti ya Twitter ya mkurugenzi mtendaji wa Twitter yadukuliwa

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
4,446
16,301
Akaunti ya Mkurugenzi Mtendaji wa Twitter, Jack Dorsey kwenye wavuti ilivamiwa Ijumaa, na anaweza kuwa amekumbwa na hatari ambayo Twitter ilionywa hapo awali na ikakataa mara kwa mara ilikuwa shida.

Kwa kama dakika 20 Ijumaa alasiri, akaunti ya Dorsey ilituma safu ya jumbe zenye ubaguzi wa rangi na vingine. Twitter ilikubali haraka kwamba kuna mtu alikuwa ameiba akaunti, na wakasema sasa iko salama.

Tweets zilionekana kama hazijatumwa kwa kuiba akaunti halisi ya Dorsey, lakini na watekaji au matapeli wanaoshawishi mifumo ya Twitter kuwa walikuwa na simu yake na walikuwa wakituma maandishi hayo kwenye akaunti yake. Inawezekana kwamba watekaji au matapeli hawangehitaji hata nenosiri la Dorsey, au waliwahi kutolewa kwa sababu hiyo.

malisa_gj-20190831-0001.jpeg
 
Huyo mmiliki wa twiter aliyedukuliwa angekua mtanzania mijitu ingeshinda baa na kushangilia sana
 
Wadukuzi walichukua kwa muda udhibiti wa akaunti ya Twitter ya mwanzilishi na mkurugenzi wa mtandao wa kijamii wa Twitter.

Wadukuzi walianza kutumia akaunti hiyo kusambaza taarifa za chuki na kibaguzi kwa kutumia lugha chafu


Kundi la wadukuzi linalojiita Chuckling Squad limedai kuhusika na udukuzi wa akauntui ya Twitter ya Jack Dorsey.

Akaunti hiyo iliyo na mashabiki zaidi ya milioni nne ilianza kutumiwa kusambaza taarifa za chuki na kibaguzi kwa kutumia lugha chafu kwa karibu dakika kumi na tano.

Twitter inasema mitambo yake haikufikiwa na wadukuzi na badala yake kulaumu kampuni ya mawasiliano ambayo haikuitaja jina lake kwa kusababisha hitilafu hiyo.

“Nambari ya simu inayohusishwa na akaunti hiyo ilitumiwa kutokana na hitilafu ya kiufundi iliyosababishwa na kampuni hiyo ya mawasiliano ,” ilisema taarifa iliyotolewa na Twitter.

“Hali hiyo ilitoa fursa kwa watu wasio na idhini ya kutumia nambari hiyo kuanza kutuma ujumbe kwenye mtandao wa Twitter.”

Chanzo cha habari kutoka Kampuni hiyo ilithibitishia BBC kuwa wadukuzi walitumia mfumo unaojulikana kama “simswapping” kuchukua udhibiti wa akaunti ya Twitter ya Bw. Dorsey.

Huu ni mfumo ambao inatumiwa kuhamisha nambari halisi ya simu ya Dorsey katika laini nyingine- na kuanza kuitumia.

Wadukuzi mara nyingine hutoa hongo kwa wahudumu wa kampuni za mawasiliano au kuwapotosha kupata namabari halisi.

Kwa kuchukua udhibiti wa nambari hiyo wadukuzi waliweza kuandika ujumbe moja kwa moja katika akaunti ya Twitter ya Bw. Dorsey.

Japo siku hisi watumiaji wengi wa mtandao huo wanatumia programu tumishi kwenye simu zao kutuma ujumbe, awali Twitter ilibuniwa katika mfumo wa kutuma ujumbe mfupi- hali inayoisaidia kudhibiti idadi ya maneno mtumiaji anastahili kuandika.

Wadukuzi waliandika nini?

Ujumbe wa chuki na wa kibaguzi – ulitumwa moja kwa moja kwa kutumia akaunti ya Jack, na wengine waka sabaza ujumbe huokwa kutumia akaunti zingine.

Ujumbe mmoja uliashiria kuna bomu limetegwa katika makao makuu ya kampuni hiyo.

Chuckling Squad imedai kuhusika na udukuzi wa Twitter za watu mashuhuri, kama vile mwanablogu wa masela ya urembo James Charles miongoni mwa watu wengine.

Image result for CEO twitter hacked


Japo tukio hilo linaonekana kufanyika nje ya kampuni hiyo, linasalia kuwa aibu kwa mtandao wa kijamii wa Twitter, unaotoa huduma kwa viongozi wenye nguvu zaidi ulimwenguni.

The post Akaunti ya Twitter ya mwanzilishi wa Twitter yadukuliwa, kikundi hiki cha husishwa na tukio hilo appeared first on Bongo5.com.
 
Back
Top Bottom