Akaunti ya tweeter ya Mhe. Rais na Mhe. Makamu wa Rais kila wakitweet hakuna viongozi wa CCM wanaungana naye; tujisahihishe

Huo mi naona ni kuwa mtumwa kwa kiongozi. Asee kati ya vitu vinanipa hard time ni kuwa "chawa" wa kiongozi. Mi siwezi na siwezagi. Kama mama amejenga mazingira ya kutotengeneza machawa hilo ni jambo la kupongeza kwake.
 
Mhe. Rais anapotweet inatia hamasa kuona aliowateua wakijumhuka naye, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu the same. Huyu ni Mkuu wa nchi na anapotumia mitandao anataka kuzungumza na Dunia. Anapomaliza kuzungumza au kutuma ujumbe Duniani then waliopochini yake wasilike,retweet wala reply inavunja moyo.

Hili lina impact kubwa Sana, ukitaka kuangalia tizama idadi ya comments na retweets zinavyopungua kwenye akaunti hizi. Ni kwa sababu kipindi wamepata madaraka na tulipotaka watuteue tulikuwa tunafuatilia kila anachotweet nakukisupport ila alipotuteu basi hadi account zake hatuzifungui.

Leo ni Christmas na Mhe. Rais amewatakia Watanzania heri ya sikukuu hii ya Noel, lakini hakuna Mbunge, Mkuu wa wilaya,mkoa, Waziri Wala mteule yoyote aliyecomment.

Viongozi kumuunga na kumsaidia Kiongozi nipamoja na kufuatilia anayofanya na kumtia moyo. Mhe. Rais akisoma comments hasa kipindi hiki cha mapumziko akakuta kwenye tweet zake pamejaaa KERO za wananchi anafika mahali anawaza je Nina safu sahihi? Sometimes tengeni muda wenu kutolea ufafanuzi au majibu ya tweets za Viongozi wa Kitaifa. Hawa viongozi wanahitaji kulindwa Kwa njia mbalimbali na ulinzi mmoja wapo mkubwa nikuona wale aliowateua wanasimama naye kwenye Nuru na giza. Akipost shambulieni jukwaa Kwa staha na msikereke na majibu au hoja za wapinzani wake, siasa nikujibizana siyo kukaa kimya ukisubiri upewe microphone ndo useme.

Mwisho nimpongeze Mhe. Rais kwa kazi nzuri anayofanya nikitambua wazi yeye kama Mama anahitajika na familia binafsi lakini anahitajika nasisi wanafamilia waliotawanyika. Asichoke kutuhudumia Kwa haki, asikasirishwe na mmoja wetu akahukumu Kwa hasira, asizingwe na hoja zinazowasilishwa kwake isivyo faa akaelekeza mateso kwetu. Atambue sisi ndio tunaweza kumtia majaribuni au kumwokoa na movu shetani. Atuvumilie na atafakari upya Kuhusu hatma ya wananchi waliowekwa ndani pasipo na dhamana huku Tanzania bara wakati wakati watuhumiwa wa makosa hayohayo huko Zanzibar wanapewa dhamana. Yeye ni Rais wa Jamhuri wa Muungano, arejeshe usawa wa haki ya kusikilizwa na kuachiwa Huru Hadi pale watakapopatikana na hatia.

Kila la kheri 2022 my President
Kila mtu yupo kimaslahi hakuna anaye mpenda mwenzake ni unafiki na kuviziana kichobaki ndani ya ccm
 
Back
Top Bottom