Akaunti ya TFF Yafilisiwa na TRA

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,739
4,732
Ndugu wana JF nimesikia kupitia Channel 10 kuwa TRA wameamua kuifilisi akaunti ya TFF na sababu za msingi za wao kufanya hivyo ni TFF kushindwa kulipia gharama za makocha wa timu ya Taifa Kuanzia MAXIMO NA POUSELN, Nimepata shaka sana kwani katika kumbukumbu zangu hii ilikuwa ni ahadi za Rais Kikwete kuwa serikali italeta Makocha wa kigeni ili kuinua kiwango cha Soka hapa Bongo na italipia gharama zote za makocha hao.

My Take.
1. Kama ilikuwa ni ahadi ya Serikali na ikatekeleza ahadi ya kuleta makocha hao hivi nani alikuwa anawalipa na walikuwa wanalipwa Tsh. ngapi na je fedha walizokuwa wakilipwa zilitoka wapi?

2. Wakati wa ujio wa makocha hao TFF walipewa taarifa kuwa wanatakiwa kuwalipia gharama hao makocha, maana tukiangalia kwa Maximo kwa sasa hayupo na hakuna anacholidai taifa hili.

3. Hii pia inanipa wasiwasi na Ahadi za Rais inawezekana haweki kumbukumbu zake wakati anapoongea na inawezekana leo hii akiulizwa juu ya ahadi hii anaweza kukana kuwa hakuitoa.

** Kutokana ka kufilisiwa huko inasemekana inawezekana Round ya pili ya ligi kuu ikachelewa kuanza kwani fedha walizochukua ni zile Nauli za Timu zilizotolewa na wadhamini wa Ligi KUU.
 
Wakati wenzetu wakifanya kila kitu kwa utaratibu wake sisi kila kitu ni siasa na siasa ni kila kitu. Tusipojenga mfumo wa kuwajibishana, ole wetu. Mtu anaahidi kujenga daraja hata pasipokuwa na mto, halafu watu wanashangilia na kugawa kura!
 
hongera saana TRA, mmefanya kazi nzuri saana , mpira wa miguu ni mchezo unaotakiwa uwe wa mfano kwa matendo mazuri, kwani watoto wote wa kike na kiume wakiwa wadogo wote hupenda kucheza mchezo huo , sasa hapa kwetu mchezo huu bado unachezwa na watoto, maana hao walioshika uongozi wa mpira baado wana mawazo ya kitoto, TRA wabaneni mpaka walipe hizo fedha na fuatilieni mpaka faini wanazozipiga klabu hakikisheni mnakata kodi yenu. na zile fedha wanazopokea toka fifa kateni kodi mpaka watie akili na wawe mfano bora.maana hawa watu ni wavivu saana hata wa kusimamia mapato sahihi ya viingilio vya milangoni .siku moja simamieni nyinyi wenyewe ukataji tiketi na uingiaji uwanjani muone fedha kibao mtakusanya nasisitiza TFF ni wazembe,wazembe ile mbaya hivi inakuingia akilini kudaiwa hiyo fedha na hawana mikakati yoyote ya kulipa zaidi ya kufikiria kulipiwa au kusamehewa jamani hata kualika timu toka nje na kuandaa mashindano fulani mnashindwa?
 
Yote unayoongea juu ya udhaifu wa TFF nayakubali, lakini suala langu ni Hao makocha waliokuja kwa ahadi ya JK je TFF walitaarifwa kuwa wanatakiwa kuwalipia gharama na kama ndiyo je ahadi ya JK alikuwa anatuhadaa watanzania?
 
Hahahaaa TFF baba, wamelewa kabisa, sasa wametonesha kidonda cha serikali, wao walivyowatosa madogo kwenye mshiko wao walidhani ni zile tim za vilabu vidogo wanazowababaisha? Maana vilabu vikubwa vina watu wao ndani ya TFF. Wakawaulize wanasiasa waliokuwa wakiichefua serikali hizo bili za TRA zilivyowashukia, chezea serikali weye...

TFF ni kituko, story hii kama itathibitisha nadhani hii adhabu haiwatoshi wana a ot of sub-standards na vikanuni vyao vinavyoundwa kila ligi inapokweisha ilimradi tu kulindana ndani kwa ndani
 
Yote unayoongea juu ya udhaifu wa TFF nayakubali, lakini suala langu ni Hao makocha waliokuja kwa ahadi ya JK je TFF walitaarifwa kuwa wanatakiwa kuwalipia gharama na kama ndiyo je ahadi ya JK alikuwa anatuhadaa watanzania?
nchi yetu ina udhaifu mwingi saana, ktk hili kwanza nashutumu saana kada ya uandishi wa habari , wanapaswa wachunguze na watupe taarifa njia ya malipo ya mishahara ya hawa watu ilikuaje? mf; walikuwa wanapokelea mshahara pale tff kwa maana ya wizara inaingiza kwenye akaunt za tff au walikuwa wanapokelea moja kwa moja wizarani? au walikuwa wanamlipa kienyeji mtaaani? kumbuka mh SUGU amekuwa anapiga kelele saaana juu ya hawa wasanii kutoka nje wanalipa kodi? na njia ya malipo yao inafanyikaje? binafsi napenda saana hawa TFF wabanwe mbavu haswa hebu ona mwenyewe mikakati yao, imekaa kikuhurumiwa badala ya kufuatilia na kubuni jinsi gani? ya kulipa hizo kodi, ahadi ya rais aliitekeleza kocha alikuja na hakuwahi kulalamika juu ya mshahara na hata akawaita na makocha wengine toka kwao kwa ajiri ya timu za vijana nao vp au tff ilipandia hapo na kukwepa kodi.
 
Safi sana TRA TFF walikuwa wanajikagua wenyewe ni aibu tff kuwa omba omba inabidi iajiri wataalamu haswa sio kuokota vilaza naomba Tra wasiishie TFF waingie Simba Na Yanga kuna ufisadi na ukwepaji mkubwa wa kodi haiwezekani vilabu vinunue wachezaji kwa mamilioni au wauze kwa mamilioni bila kulipa kodi serikalini hii itasaidia kuwabana viongozi wezi
 
Hongera sana sana TRA, hawa jamaa walijiona wao ni juu ya Tanzania sasa hivi wanapiga DANADANA uchaguzi mkuu wakilenga kombe la mataifa la Afrika wapate mpango hapo.
 
TRA imekomba ile account nono ya TFFv/s VODACOM kwa ajili ya kuendeshea ligi... yaani washapata sababu ya kusimamisha mzunguko wa pili sasa..
 
Ndugu wana JF nimesikia kupitia Channel 10 kuwa TRA wameamua kuifilisi akaunti ya TFF na sababu za msingi za wao kufanya hivyo ni TFF kushindwa kulipia gharama za makocha wa timu ya Taifa Kuanzia MAXIMO NA POUSELN, Nimepata shaka sana kwani katika kumbukumbu zangu hii ilikuwa ni ahadi za Rais Kikwete kuwa serikali italeta Makocha wa kigeni ili kuinua kiwango cha Soka hapa Bongo na italipia gharama zote za makocha hao.

My Take.
1. Kama ilikuwa ni ahadi ya Serikali na ikatekeleza ahadi ya kuleta makocha hao hivi nani alikuwa anawalipa na walikuwa wanalipwa Tsh. ngapi na je fedha walizokuwa wakilipwa zilitoka wapi?

2. Wakati wa ujio wa makocha hao TFF walipewa taarifa kuwa wanatakiwa kuwalipia gharama hao makocha, maana tukiangalia kwa Maximo kwa sasa hayupo na hakuna anacholidai taifa hili.

3. Hii pia inanipa wasiwasi na Ahadi za Rais inawezekana haweki kumbukumbu zake wakati anapoongea na inawezekana leo hii akiulizwa juu ya ahadi hii anaweza kukana kuwa hakuitoa.

** Kutokana ka kufilisiwa huko inasemekana inawezekana Round ya pili ya ligi kuu ikachelewa kuanza kwani fedha walizochukua ni zile Nauli za Timu zilizotolewa na wadhamini wa Ligi KUU.
kibogo elewa kitu kimoja mwajiri wako akikulipe TShs. 1,000,000 ni wajibu wake kukukata wewe kibogo kodi ya mapato ya TShs. 1,000,000 na kuiwakilisha TRA. Haijalishi hiyo TShs. 1,000,000 ilitoka kwa nani kinachoangaliwa hapa ni kwamba wewe kibogo umepokea pato la TShs. 1,000,000 yule anayekupa hizo pesa anawajibika kukusanya kodi ya serikali na kuiwakilisha kunakohusika
 
Last edited by a moderator:
Yote unayoongea juu ya udhaifu wa TFF nayakubali, lakini suala langu ni Hao makocha waliokuja kwa ahadi ya JK je TFF walitaarifwa kuwa wanatakiwa kuwalipia gharama na kama ndiyo je ahadi ya JK alikuwa anatuhadaa watanzania?
na hata kama serikali ndio inapaswa kulipa ni kwa kuisaidia TFF, hivyo TFF nendeni serikalini muwaeleze wawape hiyo pesa mwalipe TRA.
Uswahili umezidi sana hapa na hii hatua ya TRA inaweza angalau ikasaidia kuwaamsha wadau wa mpira. Kila siku utasikia makato ya mechi ambayo chanzo chake kikuu ni viingilio vya watazamaji lakini huwezi kusikia fungu la kulipa kodi!
Na pale unaposikia timu zinagombania mchezaji kwa kuwalipa mpaka US $100,000 lakini kwenye vitabu vyao wanaonyesha sifuri kwenye ushuru.
TRA kazeni kamba na muende zaidi ya hapo kwa kuziingilia hata hizi klabu

Back
Top Bottom