Akaunti ya pamoja ya muungano kusubiri majadiliano ya pande zote mbili

Mathayo Fungo

JF-Expert Member
Nov 13, 2018
319
510
Bunge limeelezwa kuwa, akaunti ya pamoja ya fedha haijafunguliwa na kuanza kufanya kazi kwa kuwa majadiliano kati ya serikali ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayajakamilika.

Kauli hiyo ilitolea bungeni jana na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk Ashatu Kijaji alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (chadema), Zainab Mussa Bakar.

Katika swali lake, mbunge huyo alisema kwa muujibu wa Katiba kuna asilimia ya mapato inatakiwa iende serikali ya Mapinduzi Zanzibar. "Je, utekelezaji wa suala hili umefikia wapi", alihoji.

Dk Kijaji alijibu kwa kusema kuwa utaratibu wa uendeshaji wa akaunti ya pamoja ya fedha umependekezwa kwenye ripoti ya mapendekezo ya vigezo vya kugawana mapato na kuchangia gharama za muungano iliyoandaliwa na Tume ya Pamoja ya Fedha ya mwaka 2006.

Hata hivyo, akunti ya pamoja ya fedha haijafunguliwa na kuanza kufanya kazi kwa kuwa majadiliano kati ya serikali zote mbili kuhusu mapendekezo ya Tume hayajakamilika.
Naibu waziri.jpg
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom