Akatwa mapanga hadi kufa akituhumiwa kwa uchawi

miss zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
2,764
2,000Kwa ufupi
  • Baadhi ya matukio ya mauaji hasa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa yamekuwa yakihusishwa imani za kishirikina.
Bukombe. Namagambo Malila (50) Mkazi wa Kijiji cha Bulumbaga, wilayani hapa amefariki dunia baada ya kukatwa mapanga na watu wasiojulikana wakimtuhumu kuwa mchawi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema mauaji hayo yalitokea Juni 4, mwaka huu saa 12.00 jioni kwenye kichaka pembeni ya barabara aliyokuwa anapita mwanamke huyo wakati akitoka kilabuni.

Mwabulambo amesema wakati wa tukio hilo marehemu alikuwa ameambata na watoto wake wawili ambao walikimbia baada ya kutishiwa na watu wasiowafahamu.

"Baada kuwatishia walimkata mwanamke huyo kwa mapanga na kumuacha kisha wakakimbia."
Mdogo wa marehemu, Ndakalya Kalunde amesema hawafahamu kilichosababisha kuuawa kwa ndugu yao kwa sababu hakuwa mchawi kama inavyodaiwa.

Mkazi wa kijiji hicho, (jina lake linahifadhiwa), amesema mama huyo alikuwa akituhumiwa kuwa mchawi na kwamba alishawahi kuitwa na uongozi wa Serikali ya kijiji kuhusu tuhuma lakini alikana.

Hata hivyo inadaiwa kuwa viongozi hao waliomwita kumhoji wamefariki dunia jambo ambalo limehusishwa na madai ya kuwa mchawi.

Diwani wa Kata ya Ruzewe Mashariki, Masanja Maduhu amewaomba wananchi kutohusisha tukio hilo na imani za kishirikina kwa sababu kifo ni mapenzi ya Mungu.

By Ernest Magashi, Mwananchi
 
scooman

JF-Expert Member
Mar 21, 2017
2,725

Haya mambo yanaiaumbua sana jamii ni vigumu sana kuthibitisha iwapo mtu ni mchawi ama la!.ila iwapo kweli alikuwa mchawi adhabu hiyo inastahili na hata kwa wengine wanajihusicha na ulozi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom