Akatuambia; atatoa posa nikiwa kwake, siwezi msubiri hapa nyumbani

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,330
51,836
Anaandika, Robert Heriel

"Kwa nini umejipeleka mwenyewe?"
"Umeamua kujirahisisha kwa huyo mwanaume"
"Unaitia aibu familia"
Yalikuwa maneno ya mama na watu wazima wengine waliokuwa wakimwambia Dada yangu. Dada alikuwa kanuna hasa, sikuwahi kumuona katika namna Ile. Alikuwa kanuna kikweli kweli.

Leo Taikon sitaki kusimulia sana, najua wengi humu siwalipi kusoma maandiko yangu 😊 lakini nanyi si hamnilipi. Basi sawa.

Moja ya changamoto wanayopitia dada zetu siku hizi ni suala la kuchumbiwa. Kimsingi hili limekuwa tatizo katika jamii yetu. Nadhani kwa sasa kila familia yenye mtoto wa kike inawezakuwa inakabiliwa na tatizo hili.

Dada zetu wanapata shida, hata kama watajikaza au kuzuga kuwa haiwatese lakini kimsingi inawatesa. Sio wao tuu hata wazazi pamoja na vijana wa kiume.

Hakuna mwanamke yeyote duniani asiyependa kuolewa kwa heshima/kufuata taratibu za kimila na kisheria. Hakuna! Lakini mazingira ya dunia ya sasa hayawapi sapoti. Na hapo ndipo wahenga wa zamani wanapoonekana kutuzidi akili kizazi cha sasa katika upande wa ndoa na mahusiano.

Ukabila usingeruhusu jambo hili kutokea. Kuua ukabila kuna faida nyingi lakini moja ya hasara zake ni pamoja na janga la katika ndoa.

Turudi kwenye stori yetu;
Wazazi na ndugu wakazidi kumsakama dada yetu ambaye alikuwa anaishi na mwanaume kinyumba pasi na ndoa kwa zaidi ya mwaka sasa tangu amalize chuo miaka mitano iliyopita. Hii ni kusema dada yangu anamiaka 28 hivi.

Dada akafungua kinywa chake akasema huku akiwa analia;
"Mimi ningefanyaje mama? Ningefanyaje! Ninyi mnataka heshima hilo hata mimi nataka mpate lakini vipi kwa upande wangu?

Wote ninyi ni mashahidi jinsi nilivyohangika kutafuta mchumba, nilifunga na kuomba, nilijiunga mpaka na vikundi vya kanisani kwa ajili ya kupata mchumba lakini wapi. Imenichukua miaka sita kumpata mwanaume huyu ambaye angalau yeye ameonyesha dalili njema ya kuwa mume wangu.

Siwezi msubiri, siwezi fuata sheria katika dunia hii isiyofuata sheria kwa sasa. Yaani nikae nyumbani hapa kusubiri posa wakati najua maelfu kwa maelfu ya wanawake wanaowinda wanaume wa kuwaoa. Kwa kweli siwezi subiri posa nikiwa hapa nyumbani.

Nitasubiri posa nikiwa naishi naye, send-off nikiwa naye,
Kitchenpart nikiwa naye,
Mpaka ndoa itafungwa nikiwa kwake.

Siwezi kusubiri, kwa kweli. Acha mnione hivyo lakini hii ni kwaajili ya maisha yangu. Mimi ndio nimechagua njia hiyo"

Akameza mate yake huku akilia, alafu akaendelea huku akimtazama Mama;
"Nisamehe mama, hujui tuu changamoto ilivyo kwa kipindi hiki. Tena akheri mimi ninahuyo aliyeniweka ndani hata kama siyo kwa ndoa, kuna wanawake maelfu wanatamani hata huyo wa "SOGEA TUISHI" lakini hawana na hawapati".

"Mungu ndiye anajua, hatuwezi kupita njia moja watu wote, huenda sikuandikiwa kuolewa ndipo niishi na mwanaume. Nani ajuaye niliandikiwa niishi na mwanaume ndipo anioe!"

Dada akamaliza, Taikon kama mnavyonijua nikasema lazima niwafikishie wadau wangu humu ili tupate habari na wachambuzi wachambue, wakosoaji wakosoe, watukanaji watukane, wajuaji walete ujuaji wao, mafarisayo wamuone dada yangu mdhambi, basi kila mtu na mawazo yake. Wala sio kosa.

Kimsingi, siku hizi wanawake uvumilivu wao umekuwa mdogo. Hawaamini tena kwenye kusubiri wakiwa nyumbani, wanaona wanachelewa sana au pengine wanahofu ya kukosa kabisa. Kuliko wasubirie wameona wakaidakie ndoa juu kwa juu kama sandakalawe! Doooh! Ndoa imekuwa sandakalawe mwenye kupata apate mwenye kukosa akose.

Wanawake wanarukia wanaume juu kwa juu kwa kuogopa wakitua chini kutakuwa na jam ya mapambano. No rule in hell, kumaanisha hakuna sheria kuzimu/jehanamu. Yaani kwa wahuni au dunia ya wahuni hakuna sheria 😂😂,
Mnapasuana tuu.

Sio ajabu wanawake siku hizi wanaonekana maharage ya Mbeya maji mara moja. Kwani mmoja anaogopa akijifanya mfuata sheria na maadili wanatokea wahuni kusikojulikana wanapita na mwanaume anayempenda. Kwa kuhofia hill basi naye anajikuta kwenye msafara wa mazombi😀😀 ili kuendana na sheria za kuzimu.

Dada yangu anasema alisubiri amechoka, ameona kila anaowasubiri hawaji na wanaoa kwengine tena wanaoolewa ni wale aliowazidi credit za kimaadili na kiuzuri.

Taikon anatabiri kuwa miaka ijayo ule mfumo wa kuchaguliwa wachumba utarudi miaka mingi ijayo ingawaje itakuwa ngumu ku-function kwa sababu ukabila kwa kiasi kikubwa utakuwa umedondoka, dini zitakuwa zimedondoka.

Hivyo wasichana na vijana watatamani kuchaguliwa wenza wao lakini hilo halitawezekana.

Hapo ndipo tofauti ya binadamu na mnyama itazidi kuwa ndogo.
Mwanamke atakuwa anazaa Kama mbuzi au ng'ombe tuu kila mtoto na baba yake na hilo lisiwe shida.

Nini Maoni yako?

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Dar es Salaam.
 
Waache wazae kwa upumbavu wao, wakiwa kwenye peak wanachagua wanaume, wanaleta ujuaji kwenye mahusiano hawajui kama wana expire date

Wanawake wanapaswa kujua bila wanaume maisha yao ni kama kuzimu, furaha na amani ya maisha yao inakuwepo wakiwa chini ya mwanaume kwa njia ya ndoa.
 
waache wazae kwa upumbavu wao, wakiwa kwenye peak wanachagua wanaume, wanaleta ujuaji kwenye mahusiano hawajui kama wana expire date

Wanawake wanapaswa kujua bila wanaume maisha yao ni kama kuzimu, furaha na amani ya maisha yao inakuwepo wakiwa chini ya mwanaume kwa njia ya ndoa.

Hatari Sana.
 
Anaandika, Robert Heriel

"Kwa nini umejipeleka mwenyewe?"
"Umeamua kujirahisisha kwa huyo mwanaume"
"Unaitia aibu familia"
Yalikuwa maneno ya mama na watu wazima wengine waliokuwa wakimwambia Dada yangu. Dada alikuwa kanuna hasa, sikuwahi kumuona katika namna Ile. Alikuwa kanuna kikweli kweli.

Leo Taikon sitaki kusimulia sana, najua wengi humu siwalipi kusoma maandiko yangu lakini nanyi si hamnilipi. Basi sawa.

Moja ya changamoto wanayopitia dada zetu siku hizi ni suala la kuchumbiwa. Kimsingi hili limekuwa tatizo katika jamii yetu. Nadhani kwa sasa kila familia yenye mtoto wa kike inawezakuwa inakabiliwa na tatizo hili.

Dada zetu wanapata shida, hata kama watajikaza au kuzuga kuwa haiwatese lakini kimsingi inawatesa. Sio wao tuu hata wazazi pamoja na vijana wa kiume.

Hakuna mwanamke yeyote duniani asiyependa kuolewa kwa heshima/kufuata taratibu za kimila na kisheria. Hakuna! Lakini mazingira ya dunia ya sasa hayawapi sapoti. Na hapo ndipo wahenga wa zamani wanapoonekana kutuzidi akili kizazi cha sasa katika upande wa ndoa na mahusiano.

Ukabila usingeruhusu jambo hili kutokea. Kuua ukabila kuna faida nyingi lakini moja ya hasara zake ni pamoja na janga la katika ndoa.

Turudi kwenye stori yetu;
Wazazi na ndugu wakazidi kumsakama dada yetu ambaye alikuwa anaishi na mwanaume kinyumba pasi na ndoa kwa zaidi ya mwaka sasa tangu amalize chuo miaka mitano iliyopita. Hii ni kusema dada yangu anamiaka 28 hivi.

Dada akafungua kinywa chake akasema huku akiwa analia;
"Mimi ningefanyaje mama? Ningefanyaje! Ninyi mnataka heshima hilo hata mimi nataka mpate lakini vipi kwa upande wangu?

Wote ninyi ni mashahidi jinsi nilivyohangika kutafuta mchumba, nilifunga na kuomba, nilijiunga mpaka na vikundi vya kanisani kwa ajili ya kupata mchumba lakini wapi. Imenichukua miaka sita kumpata mwanaume huyu ambaye angalau yeye ameonyesha dalili njema ya kuwa mume wangu.

Siwezi msubiri, siwezi fuata sheria katika dunia hii isiyofuata sheria kwa sasa. Yaani nikae nyumbani hapa kusubiri posa wakati najua maelfu kwa maelfu ya wanawake wanaowinda wanaume wa kuwaoa. Kwa kweli siwezi subiri posa nikiwa hapa nyumbani.

Nitasubiri posa nikiwa naishi naye, send-off nikiwa naye,
Kitchenpart nikiwa naye,
Mpaka ndoa itafungwa nikiwa kwake.

Siwezi kusubiri, kwa kweli. Acha mnione hivyo lakini hii ni kwaajili ya maisha yangu. Mimi ndio nimechagua njia hiyo"

Akameza mate yake huku akilia, alafu akaendelea huku akimtazama Mama;
"Nisamehe mama, hujui tuu changamoto ilivyo kwa kipindi hiki. Tena akheri mimi ninahuyo aliyeniweka ndani hata kama siyo kwa ndoa, kuna wanawake maelfu wanatamani hata huyo wa "SOGEA TUISHI" lakini hawana na hawapati".

"Mungu ndiye anajua, hatuwezi kupita njia moja watu wote, huenda sikuandikiwa kuolewa ndipo niishi na mwanaume. Nani ajuaye niliandikiwa niishi na mwanaume ndipo anioe!"

Dada akamaliza, Taikon kama mnavyonijua nikasema lazima niwafikishie wadau wangu humu ili tupate habari na wachambuzi wachambue, wakosoaji wakosoe, watukanaji watukane, wajuaji walete ujuaji wao, mafarisayo wamuone dada yangu mdhambi, basi kila mtu na mawazo yake. Wala sio kosa.

Kimsingi, siku hizi wanawake uvumilivu wao umekuwa mdogo. Hawaamini tena kwenye kusubiri wakiwa nyumbani, wanaona wanachelewa sana au pengine wanahofu ya kukosa kabisa. Kuliko wasubirie wameona wakaidakie ndoa juu kwa juu kama sandakalawe! Doooh! Ndoa imekuwa sandakalawe mwenye kupata apate mwenye kukosa akose.

Wanawake wanarukia wanaume juu kwa juu kwa kuogopa wakitua chini kutakuwa na jam ya mapambano. No rule in hell, kumaanisha hakuna sheria kuzimu/jehanamu. Yaani kwa wahuni au dunia ya wahuni hakuna sheria ,
Mnapasuana tuu.

Sio ajabu wanawake siku hizi wanaonekana maharage ya Mbeya maji mara moja. Kwani mmoja anaogopa akijifanya mfuata sheria na maadili wanatokea wahuni kusikojulikana wanapita na mwanaume anayempenda. Kwa kuhofia hill basi naye anajikuta kwenye msafara wa mazombi ili kuendana na sheria za kuzimu.

Dada yangu anasema alisubiri amechoka, ameona kila anaowasubiri hawaji na wanaoa kwengine tena wanaoolewa ni wale aliowazidi credit za kimaadili na kiuzuri.

Taikon anatabiri kuwa miaka ijayo ule mfumo wa kuchaguliwa wachumba utarudi miaka mingi ijayo ingawaje itakuwa ngumu ku-function kwa sababu ukabila kwa kiasi kikubwa utakuwa umedondoka, dini zitakuwa zimedondoka.

Hivyo wasichana na vijana watatamani kuchaguliwa wenza wao lakini hilo halitawezekana.

Hapo ndipo tofauti ya binadamu na mnyama itazidi kuwa ndogo.
Mwanamke atakuwa anazaa Kama mbuzi au ng'ombe tuu kila mtoto na baba yake na hilo lisiwe shida.

Nini Maoni yako?

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Dar es Salaam.
Uko vizuri kaka
 
Kadri siku zinavyoenda wanawake wanashuka thamani, mim naona dada ako ametumia akili kubwa kuliona hilo ,kwa miaka aliyo nayo ilikuwa ni lazima afanye hivyo ili alete heshima kwake hata kwa familia yenu pia.
 
Back
Top Bottom