Akataa maiti ya mwanawe, atozwa faini ya laki 2

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MKAZI wa Kijiji cha Idiga katika Kata ya Utengule Usongwe wilayani Mbeya, ametozwa faini ya Sh 200,000 zikiwa ni malipo ya fedhea kwa kijiji baada ya kukataa maiti ya mtoto wake aliyejinyonga.

Kijana huyo, Anyimike Kapoya (27) maarufu kama Alfonce (27) alijinyonga kwa kwa kamba nje kidogo ya kijiji hicho.

Mkazi huyo, Alison Kapoya anayeishi katika kitongoji cha Kasale, alikutwa na adhabu hiyo jana baada ya wakazi wenzake kukasirishwa na kitendo alichokifanya cha kukataa maiti ya mwanawe.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, awali Mzee Kapoya alipelekewa taarifa za kujinyonga kwa mwanawe lakini kwa sababu ambazo hazikufahamika hakuungana na ndugu, jamaa na wakazi wenzake waliokwenda eneo la tukio kushuhudia.

Hata hivyo, kutofika kwa baba wa marehemu eneo la tukio hakukuwashangaza wakazi hao.

Jeshi la Polisi liliika na kuuchukua mwili wa kijana huyo ambaye sababu za kujinyonga hazijajulikana na kuupeleka nyumbani kwa baba yake.

Polisi walipofika nyumbani kwa Kapoya, aliukataa mwili huo bila kutoa sababu yoyote hali iliyozua tafrani nyumbani hapo hadi wazee wa kijiji walipoingilia kati na kumshauri kwa kina na hatimaye akakubali.

Kutokana na fedhea hiyo iliyowakasirisha wananchi waliokusanyika nyumbani hapo, Kapoya alitozwa kiasi hicho cha fedha na kulazimika kuzilipa papo hapo kisha vijana kuruhusiwa kwenda kuchimba kaburi na baadaye kufanya maziko.

Taarifa kutoka kwa ndugu wa marehemu zinaeleza kuwa ni siku chache tu zimepita tangu Anyimike aoe, hali inayozusha maswali mengi kuhusu sababu ya kujinyonga.
 
Back
Top Bottom