Akamatwa kwa kuvaa fulana yenye picha ya Besigye

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
160530124854_bbc-uganda_640x360_bbc_nocredit.jpg


Baadhi ya raia nchini nchini Uganda wamelaumu hatua ya kukamatwa kwa mwanamme moja ambaye anadaiwa kuvaa fulana yenye picha na kiongozi wa upinzani Kizza Besigye.

Samson Tumusiime alikamatwa mwishoni mwa wiki.

Hivi majuzi aliweka picha kwenye mtandao wa Facebook akiwa amevaa fulana hiyo.

Watu wengine wawili ambao wanadaiwa kuchapisha fulana hiyo nao wamekamatwa

Kulingana na msemaji polisi Fred Enanga, ni kuwa washukiwa hao watatu walikamatwa kwa sababu walikuwa wamepanga kufanya maandamano yaliyo kinyume na sheria.
 
Ya ngoswe tumwachie ngoswe, tuangalie ya hapa kwetu Tanzania yanayotukabili na kutuumiza vichwa
 
....safi sana M7. Kamata wote hao na tia ndani. Maana bila wewe M7 Uganda haiwezi kutawalika. Mpaka kizazi kitakapojielewa ndiyo wape demokrasia, ila kwa sasa kandamiza mwanawane wasipumue kabisa, kwani amani ya Uganda tunaihitaji mno africa mashariki.
 
Back
Top Bottom