Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu Dar es salaam linamshikilia Seif Abdallah Mohamed, mkazi wa Tuangoma Kigamboni jijini Dar es salaam, kwa tuhuma za kujifanya Katibu Mkuu Kiongozi wa Ikulu na kuendesha vitendo vya utapeli katika ofisi mbalimbali za Serikali ikiwemo Wizara ya Mambo ya Ndani.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Operesheni ya Jeshi la Polisi Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas, amesema Seif mwenye umri wa miaka 35 alitiwa mbaroni baada ya kumpigia simu kiongozi wa ngazi za juu kwa nia ya kutekeleza vitendo hivyo vya utapeli.
Kamanda Sabas anasema Seif anatuhumiwa kuwa alikuwa akitumia majina zaidi ya manne katika vitendo hivyo vya utapeli ikiwemo kujitambulisha kama mkuu wa nidhamu na maadili wa chama cha mapinduzi (CCM).
Chanzo: Channel Ten