EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,477
- 15,320
Raia wa Kinigeria Ogujiuba Zaccheus (mwenye kiatu) baada ya kukamatwa na kilo 26.2 za ephedrine alizokuwa anajaribu kuzileta Tanzania.
Raia wa Nigeria amekamatwa akijaribu kuingiza Tanzania kilo 26.2 za ephedrine. Mnigeria huyo, Ogujiuba Zaccheus, mwenye umri wa miaka 48, alikamatwa juzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Lagos. Dawa hizo zilikuwa zimefichwa kwa ustadi mkubwa ndani ya soli za viatu vya kike.
Minigeria huyo ameiambia mamlaka huzika kuwa alipewa mzigo huo wa viatu vya kike na rafiki yake ili kuuleta Tanzania. Amesema hata hivyo alikamatwa wakati mzigo huo ulipokaguliwa na kugundulika kuwa ulikuwa na ephedrine ndani yake. Aidha amesema anajuta kwa kujihusisha na usafirishaji haramu wa dawa za kulevya. Mnigeria anafanya kazi kama electrician na ana mke na watoto sita.
Ephedrine inatimika kutibu magonjwa ya aina mbalimbali. Hata hivyo, mgonjwa anaruhusiwa kutumia ephedrine baada ya kuandikiwa na daktari. Pia katika nchi nyingi ephedrine inauzwa tuu na mfamasia ndani phamarcy zinazotambuliwa kisheria.
Ephedrine inatumika pia kupunguza unene kwa muda mfupi. Inatumika kusaidia kutokuwa na appetite (hamu) ya kula ili kupunguza unene. Kwa mfano, inatumika sana na bodybuilders na wanariadha kupunguza unene kabla ya mashindano. Hata hivyo, madhara yake ya muda mrefu hayajulikani.
Tafiti zinadai kuwa ephedrine inasaidia katika kusoma, kufikiri na ku-concentrate kwa muda mrefu kuliko caffeine. Baadhi ya wanafunzi na watu wanaofanya kazi kwenye makampuni makubwa (white-collar workers) wanatumia ephedrine yenye herbal supplements kwa sababu hizi.
Ephedrine inatumika pia kwa ajili ya starehe (recreational use) na haina tofauti sana na amphetamine. Ephedrine inaweza kutumika kutengeneza methamphetamine haramu. Hii imefanya ephedrine kutafutwa sana kwa ajili ya kuzalisha methamphetamine haramu kinyume na sheria za nchi nyingi.
Kwa maelezo zaidi juu ya biashara ya ephedrine Afrika Mashariki na matumizi yake katika kutengeza methamphetamine pitia: Dawa za Kulevya: Dkt. Abdullah na Saboori Pharma