Akabidhiwa Sh 8m, aingiwa na tamaa, atapeliwa, adanganya kavamiwa, Polisi wamdaka

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
421
1,048
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linamshikilia Ally Mussa (36) mfanyabiashara kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo kwamba alinyang’anywa pesa Kiasi cha Tsh 8,000,000 maeneo ya Temeke Mwembe Yanga wakati akizipeleka Bank ya CRDB Temeke Sterio.

Alidai kuwa ghafla alivamiwa na watu sita wakiwa kwenye pikipiki tatu na mmoja akiwa na silaha ndogo walimshambulia na kumpora pesa hizo zilizokuwa ndani ya begi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro J. Muliro amesema Jeshi la Polisi lilifanya uchunguzi wa kina wa tukio hilo na ilibainika kuwa hakukuwa na unyang’anyi wa kutumia silaha bali ilikuwa ni tukio la kutengenezwa na mtoa taarifa.

Ilibainika fedha hizo alipewa na tajiri wake kuzipeleka benki na njiani aliingiwa na tamaa akatapeliwa baada ya kutaka kupata pesa US Dollar kwa kubadilishana na pesa alizokuwa nazo.

Mtuhumiwa huyo atafikishwa Mahakamani kwa kutoa taarifa za uongo kwa afisa wa Serikali.
 
Hiyo tamaa mdio sheitwan kwa maneno memgine. Kwahiyo sheitwan alimpitia😁😂🤣
 
double impacts kwa boss msala na kuidanganya jamhuri ,uwanja wao ,wakili wao na refa wao akitoka amrudie MUNGU
 
Back
Top Bottom