Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 54,363
- 58,385
..leo imebidi nikucheki kwa njia ya Zee manake nimekuwa nikitafuta kweli njia ya kugumiana na wewe lakini watu wananibania, nikaona sio mbaya katika miaka hii Fifte ya Independensi, nikuandikie leta. Japo ni sistim ya kilongtaimu sana,
Aka fifte za Uhuru, jana tulikuwa tunacheki runinga na wanangu, tumekuskia tumekuona na tumekubali spichi yako, ilikuwa poa sana, tulismaili kama wewe unavyosmaili kila mara lakini sasa mtu mzima, huwa unachukua muda wako kufikiria kuhusu hii laifu yetu ya kitaa ama watu wako wa karibu wanakudanganya kwamba ishu freshi tu?
Huku kwetu kimenuka ndugu yangu, watu wanapiga buku na mkwanja wa kukopa wakifikiria labda wakirudi kutoka maskonga kitaeleweka, wakirudi huku ajira zenyewe zinakuwa za kushtukiana, kama mtu hakushtukii anakupotezea, unakaa na mikaratasi yako ambayo umeisotea miaka kadhaa, wenzako wanaendelea kupeta.
Hapo ndipo mayanki wanapoanza kutafuta njia nyingine mbadala ya kuendesha laifu yao, sasa kuna taipu mbili hapa mshua, kuna wale wa kitaa ambao walikosa hata mkwanja wa kukopa, hawa ndio wanakuwa wakabaji, ile amani tunayojivunia inakuwa huko kwenu tu huku kwetu gozigozi mtindo mmoja.
Hatuna raha mshua, tukitoka kutafuta tunakabwa, tunanyang'anywa hata kile kidogo tulichonacho mwanangu, sasa hapa sisi tutakuwa tunajivunia amani gani, ndo' maana watu wanadata mpaka wanafikia kipindi wanasema bora wangezaliwa madogi mbele kuliko wanadamu bongo.
Wanashindwa hata kushtukia kwamba dogi ni dogi tu na ubinadamu una raha yake!
Misosi sasa, kila siku bei juu mwanangu, sasa hivi mpaka shuga kuweka kwente matii, imekuwa anasa, watu wanapiga chai bila mashuga wala nini, ishu za uji wa chumvi ndio zimetawala kitaani, na laifu inaendelea.
Manake imejini yuaself Mista prezident, kipato cha mtanzania ni chini ya dola moja, halafu shuga yenyewe kwa Mangi ni buku mbili, ...sema mwenyewe, unashika nini unaacha nini hapo?
Sema mwenyewe kama sio gozi gizo?
Haya, ukiachana na kesi hiyo, hivi hawa mandata a.k.a mapolisi wanafundishwa nini kule depo?
Mbona wamekuwa watu wa kutunyanyasa sana badala ya kuwa washkaji zao? Mbona wanakuwa wakitukamata wanapenda sana tuwakatie kitu kidogo kuliko kusimamia sheria kitaa kikanyooka?
Si mmewaongezea mikwanja juzi juzi tu hawa jamaa?
Sio siri nina mengi sana ya kukwambia mshua ila siimbi sasa, kama Izzo angalau umepata picha angalau kwa uchache,nila kuna ishu za maticha, manesi, na wamachinga, ishu ziko kibao mshua .
Wasaalam