Ajizi ya Kitochi cha Mkwere, Mchagga aingizwa mjini kichwakichwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajizi ya Kitochi cha Mkwere, Mchagga aingizwa mjini kichwakichwa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, May 16, 2010.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  May 16, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mkwere anaendelea kuwafunga Watanzania magoli ya kisigino, nao kwa ukarimu wa Kitochi wanamshangilia!

  KWa utamaduni wa Wachagga na hata makabila mengine, unapoita wazee kwa mashauri, unapaswa kuitisha Kitochi kama heshima kwa maana haiwezekani kwa aliye mdogo akawaita wakubwa waje kumsikiliza kwenye shauri. Hata Mangi anapotaka ushauri kwa wazee na yeye ni mtawala, bado ataitisha mkutano na Kitochi kitakuwepo. Ama Kitochi ni sawa na chakula, asusa hata soda, maji kahawa, chai, togwa au aina yeyote ile ya ukarimu inayotolewa na mtu anapofikiwa na ugeni au anapoitisha shauri.

  Kijana wa Kichagga anapotaka kuoa, kujenga nyumba hata kununua kiamba, lazima aitishe shauri kwa wazee na kwa utamaduni wa Kichagga, basi kitochi hutumika kama ukarimu wa kuitisha mkutano na wala si hongo ili Wazee au walioitwa kwenye mkutano waafiki kile mtoa Kitochi anachotaka.

  Sasa huyu askofu wa Kichagga ama naye ni mfupi wa kuufahamu utamaduni wa Kichagga au naye aliingia mkenge kama ule wa Wazeewa Dar na kuafiki anachosema Mkwere bila kufafanua.

  Ukweli ni kuwa hata kama ukitoa Kitochi Uchaggani, hakina maana kuwa basi unachotaka kitafanikiwa au ni lazima kitokee. Kitochi kitanyweka na utasikilizwa na uamuzi wa Wazee hautegemei eti kisa umewapa Kitochi au hukuwapa! Kupewa Kitochi haina maana ukubali kile ulichoitiwa na kwamba kwa kuwa ulikarimiwa na Kitochi, basi lazima uwajibike na kulipa fadhina na kukubaliana na anayetoa kitochi.

  Je amesahau kuwa Kitochi ni sawa na Tambiko? hata Biblia (na labda Kurani) ziliongelea wale wahenga wetu waliotoa Zaka ili wapate wakati wa kuwa na ana kwa ana na Muumba? Je kasahau Kitochi cha Kaini kilichokataliwa? au Kitochi cha Ibrahimu ambacho kilimpa wadhifa wa kuwa Baba wa Mataifa? Je kasahau kuwa hata Ukwereni tambiko linaweza lisilete mvua na ukame ukaendelea?

  Sasa Mkwere anapolaghai umma kudai hata CUF na CHADEMA waligawa Vitochi kabla yake, anasahau kuuambia umma kuwa uamozi wa mwisho ulikuwa ni wa Wazee wenyewe kuamua nani wanayemtaka na si kutokana na kupewa Kitochi!

  Sasa kwa kuwa CCM na Serikali yake wameamua kurubuni Watanzania na kuwahonga na hata kuhalalisha Rushwa na kuiita Kitochi au Takrima, basi ni wazi kuwa kamwe vita vya Ufisadi na kuondoa Rushwa havitaisha Tanzania!

  Alichokiacha kwa makusudi kabisa Kikwete kukitaja ni ile nguvu ya Takrima na Rushwa inayofanywa na Chama Chake na Serikali yake ya CCM ya kulegeza magoti na hapo hapo kutoa vitisho vya kulazimisha walioria Kitochi waafiki kile mtoa Kitochi anachotaka.

  Asifikiri tumekisahau Kitochi alichotoa Mkapa na Sumaye ambao baada ya kuwalisha mbege Wazee wa Kichagga, waliwachimbia mkwala ambao walifanya kweli kwa kuzuia fedha za Maendeleo kisa Wachagga waliamua kuchagua Upinzani.

  Kama jinsi Kitochi kwa Wazee wa Dar kilivyofanya kazi wii mbili zilizopita na mkwala wa kuwa na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama, basi ni wazi Watawala wa Tanzania hufanya ukarimu ili kupanda mbegu za woga kwa Wananchi kwa kutumia vitisho, ulaghai na kila aina ya udanganyifu.

  Angalia jinsi gani Wakuu wa Mikoa yenye madini ya Dhahabu, Uranium na madini mengine wanavyoitisha mikutano na kugawa vyakula, pombe na hata nguo halafu kutumia vitisho kwa Wananchi wa maeneo kuwa wasikpokubaliana na Serikali, basi Serikali itatumia nguzu zake Kikatiba kuhkikisha inalolitaka linatokea na hivyo kuwapuuzia Wananchi na Sauti na hata Haki zao.

  Kikwete ni muongo, kama juzi kadai hahitaji kura za Wafanyakazi, iweje leo awaambie Viongozi wa Dini kwa kutumia KItochi alichokifanya cha kuitisha Semina na kuwakarimu kisha kuwafanya majuha na mapunguani kwa mfano wa Kitochi na kuonyesha kwa ulimwengu kuwa ilikuwa na ulazima kwake kuwapa Wazee wa Kichagga Kitochi ili apewe kura?

  Kikwete anapaswa auambie umma rasmi na Wazi kuwa yeye, CCM na Serikali yao Rushwa, Takrima na Ufisadi ni mwendo mdundo, wataendendelea kutoa Vitochi kila kona, mara leo watu wanapewa magari ya wagonjwa, pikipiki, vocha za pembejeo, barabara zinachongwa, maji yanatiririka bombani na mikutano na halaiki nyingi inafanywa huku Watanzania wanalishwa, nyweshwa na kuvishwa Vitochi na kupewa mikwala "Wapinzani wataleta umasikini, Wapinzani wataleta umwagaji damu na kuchinjana na kuhatarisha amani, utulivu na mshikamano, Wapinzani ni maadui wa muungano. Sisi CCM tuna marafiki Wafadhili Mabwana Wakubwa Wazungu waliowapeni kisima na madawati, tuchagueni sisi CCM la sivyo mtasahauliwa kimaendeleo!"

  Sawasawa na Vitochi wanavyopewa na Wawekezaji ambao huja kuvunja bikira za Rasilimali zetu na kutubaka. Wao huwapa Watawala wetu Ki-Jitochi na kwa zulia jekundu tunawapa si Sadolini bali Pipa zima la hazina!

  Kikwete anauwezo mkubwa sana nao ni kuvunja utamaduni wa Vitochi, kwa kutoa kauli moja ya kukomesha tabia hizi za Vitochi. Kama kadiriki kudai haongezi mishahara na haogopi kunyimwa kura za Wafanyakazi, basi awaambie wenzake wasihangaike kugawa Vitochi na iwe ni marufuku kugawa vitochi na kama Watanzania watakasirika kwa kukosa Vitochi, basi CCM na Kikwete viwe tayari kuishi na matokeo ya uamuzi huo.

  Leo hii kasi ya rushwa inazidi kipimo kiasi fungu kubwa la bajeti yetu tegemezi kutoka kwa Wakubwa wa Ulaya imepunguzwa na watu wanaanza kutafutana na kuangalia nani mchawi huku wanasahau mkorogaji mkuu majivu na maganda ya mayai kwaambia Viongozi wa Tanzania wazi kuwa "Bila Rushwa na Takrima, Tanzania haina Maendeleo!"
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  May 16, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Rev. Kishoka,
  Mkuu binafsi sikubaliani na hoja nzima kwani kuna tofauti kubwa sana kati ya KUHONGA na KUKARIMU..Ikiwa tunashindwa kutofautisha vitu hivi basi kweli hakuna haja wala sababu ya kupiga vita rushwa kwani hatuelewi wala hatuna maana.
  Hivi kweli ukikamatwa na Askari ukampa kitu kidogo akale ni ukarimu au hongo!. Na ukimpa rafiki au mgeni wako kidogo hicho hicho akale ni Ukarimu au hongo..hili neno in good faith linasimama wapi jamani?
  Kama hatuna majibu ya mifano midogo kama hii sioni sababu kabisa ya kujadili tena Takrima kwa malengo ya kuondoa/kuboresha tamaduni za makabila..
   
 3. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #3
  May 16, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  mie naona hapo ni lugha tu wakuu
  kwa nini umkarim mtu wakati wa kuhitaji jambo furani kwake?
  hiyo haina ubishi ni rushwa kamili, na kukarimu kunamhusu mwenyeji kwa mgeni wake,
  lakini cha kushangaza ni kwamba mgeni ndiyo hukarimu mwenyeji, hii vipi? ni karimu ya namna gani.
  mi naona sote tumelala,
  unapoenda ugenini na kuwakarimu wenyeji wako wewe una lako jambo tu na si vinginevyo
  nikiwa na njaa hunikaribishi kula,,, nkishiba unajifanya kunikaribisha kula hapo siwezi kukuelewa kamweutakuwa una agenda za siri na mie
   
 4. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #4
  May 16, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Sikuwahi kufikiri kama unaweza kuwa of this type.....goodfaith wakati unatoa pesa with motive? Ukarimu is not a motive in this case......kama ni kipindi cha uchaguzi....motive ni kupata kura. Kea nnn uwaite kipindi hiki na uwape kitochi? Time, time, time!!
   
 5. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #5
  May 16, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mkandara,

  Waafrika wana utamaduni mzuri sana wa Ukarimu, umeanza miaka mingi sana hata kabla ya Mkoloni kuja. Huo ni ukarimu na kama ukitaka kuuita ndiyo Takrima ni hiyari yako.

  Lakini Tanzania ya sasa, kuna tofauti kubwa sana kati ya Utamaduni wa jadi wa Kiafrika na Watanzania wa Ukarimu na Utamaduni ulioletwa kwa nguvu za kisiasa ambazo huishia kuwa ni ukarimu wa kurubuni haki za Wananchi ili mtu fulani, kikundi fulani au chama fulani kipate dhamana ya kuwa kiongozi na kutawala.

  Badala ya wanasiasa na vyama kutumia hoja na utendaji kazi kama uhalalisho wa uwezo wao kuongeza na kustahili dhamana na imani ya kuongoza, wao wamegeuka na kuanza kutumia rushwa kwa kuivisha kilemba cha ukoka na kuita Takrima na kufananisha na Utamaduni wa asili wa Mwafrika na Mtanzania.

  Spika Sitta alipotoa kauli rasmi na kusema kwa Mbunge kutoa pikipiki au kujenga kisima ni ukarimu, huku inajulikana wazi ni ukarimu kukidhi mahitaji ya lazima na matokeo yake ni Wananchi kumpa kura huyu anayewafadhili kwa kutumia mali na si kutumia rasilimali na mapato ya Taifa kuleta maendeleo, hiyo ni rushwa na si ukarimu.

  Mbunge angeeleweka kama angefanya ukarimu wa kulisha, kunywesha na kuvisha watu baada ya kuchaguliwa kama ahsante (hata hii nayo ina madoamadoa ya rushwa) lakini si kabla ya kuchaguliwa!
   
 6. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #6
  May 16, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  In short hatuna rais Tanzania, haiwezekani sheria ya gharama ya uchaguzi aisign yeye kabla ya hata ya uchaguzi avunje yeye, Aibu kbwa hii Tz
   
 7. M

  Mkandara Verified User

  #7
  May 16, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu hukunielewa soma vizuri utakuta unachozungumza ndicho nilichoandika.. Nilichosema ni uwezo wa kutofautisha maana ya Hongo na Ukarimu. Ukisha jua tofauti hakuna haja ya kufananisha takrima chafu (hongo) na Takrimu safi ya ukarimu.
   
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  May 16, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Rev, Kishoka,
  Haya ni makosa ya makusudi na wazi kabisa..Hongo linabakia hongo na haramu hata kama litabebeshwa kofia ya King. Sisi wote tunajua tofauti baina ya Ukarimu wa mtu na kuhongwa..Ipo siku ukarimu kama huu wa peremende utawafikia watoto wao wenyewe wabakwe ndipo wataijuia sheria.
   
 9. IronBroom

  IronBroom JF-Expert Member

  #9
  May 16, 2010
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 524
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwamba kuna tofauti kubwa si suala tena.I think kinachogomba ni malengo ya mtoaji.Hongo na Ukarimu vyote ni vitendo vya kutoa differing only in their motives.Tutajuaje hii ni hongo na sio ukarimu or otherwise?Kwa kuwa watoaji hawasemi wazi malengo(na/au husema ni ukarimu wakati ni hongo) kwa kuzingatia timing na mazingira ya utoaji tunaweza sema pasi na shaka ni kipi hasa kinatokea kati ya mawili hayo......hiyo ya Mkwere ni hongo period!
   
 10. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #10
  May 16, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,010
  Trophy Points: 280
  Katika hii biashara ya kuuza na kununua uongozi ni nani hapa mnunuzi? Na pia muuzaji ni nani ambaye ametajwa kama mwenyeji? Na vipi kuhusu huyu mnunuzi anaetajwa kama mgeni, ni mgeni kutoka wapi, ughaibuni au?. Hivi tuna rais wa aina gani ambae uchaguzi unaweza kumuehusha hata kiasi cha kuuzarau utawala wa sheria na kuidharau hukumu ya kisheria inayotolewa na majaji? Hivi ni kwa nini wahalifu kama kina babu Seya na wengineo wanaendelea kusota magerezani wakati waliowahukumu kufungwa hawana mamlaka hayo kisheria. Hata ikulu yetu haiwathamini na sisi hatuoni sababu za kuendelea kuzitambua hukumu zao. Tutaendea kula rushwa kama kazi na takukuru mlie tu kwani rais ameihalalisha, na ninyi ni kataasisi kalikowekwa kwapani na ikulu. Viongozi wetu wa kidini nao vipi dhamira zao? Wanamuunga mkono rais kuwanunua watoto zake kwa lita ya pombe ya kienyeji? Huyo shayo anamaanisha nini kumjibu rais kwamba haiwezekani kuwakusanya ila kwa kitochi? Nanyi mmenunuliwa kwa ujira wa balaki kwa balaamu?. Jumla ya kauli ya JK ni matokeo ya serikali ambayo imeshindwa kuwaletea maendeleo wananchi wake sasa inatafuta kuwahonga kwa kuwanunua wale walio mabaradhuli(watu wasiofaa) miongoni mwa jamii. Mda sii mrefu utawaona hawa mabarathuli wakija na sifa za kumpamba mkulu kem kemu na hata wengine kujifanya wao kuwa kinywa cha Mungu na kumwita mkwere chaguo la Mungu.
   
 11. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #11
  May 17, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Naona Mzee Mwinyi naye kahoji huu mkao wa Kitochi!
   
 12. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #12
  May 17, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 156
  Trophy Points: 160
  Reverend Kishoka, asante kwa mada yako nzuri iliyotulia. Kitochi Uchagani ni desturi ya zamani, uswahilini wanaita jamvi. Mathalani unataka kikao na wazee kama kutatua mgogoro au ugomvi baina yako na mke au mume, basi sharti uweke jamvi. Ni desturi ya kijamii na haina utata kabisa. Ila Mheshimiwa anaichafua kwa kuiingiza katika Siasa. Nakumbuka enzi zile za kina Bibi Lucy Lameck akigombea ubunge kule Moshi, hapakuwa na namna yeyote alitoa kitochi ili watu waje wamsikilize. Na wala katika shughuli za kitaifa sijawahi kusikia wale wazee wa kichaga wakidai anayekuja kuzungumza nao atoe kitochi, nimesikia kwa Mh Kikwete. Enzi zile Mangi akitaka kuzungumza na watu wake walipita wachili wakiwa wanapuliza ngurumo(pembe za ngombe) na ilitosha. Lakini Mangi angeweza kulisha watu wake na sio kwa kuwa anadaiwa.

  Aache kuchafulia mila za watu. Huyo Askofu ni mnafiki, hakupenda kumuudhi mheshmiwa. Ingefaa akajitokeza akatolea ufafanuzi haya.

  Kitochi si karima hata kidogo! Ni taratibu mahsusi ya kufanya vikao, ni jamvi kwa taratibu za mahali pengine. Ni kama vile kukiwa na mkutano tunawawekea watu maji Kilimanjaro mezani. Walafi wengine huwawekea wajumbe wa mkutano hata makuku.Chama cha SIASA kikitoa kitochi, bila shaka kimeshindwa kuitisha mkutano wa hadhara kwa hivyo wanahonga ili watu waje. Ni kama CCM wanavyochezesha TOT(MABINTI walio nusu uchi kwenye jukwaa na muziki wa juu sana wakichezesha viungo vyao ili kuvutia watu waje kwenye kikao).
   
 13. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #13
  May 17, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ninio tochi bana si hizi ipo taa kuba kabisa!
   
 14. W

  WildCard JF-Expert Member

  #14
  May 17, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Hili la kitochi mbona limo kwenye sheria hii! AG wetu wa zamani, Chenge, alilisimamia vizuri siku ile ya mjadala Bungeni likaingizwa. AG wa sasa, Jaji Werema, lilimkera hili akajaribu kulizima bila mafanikio baada ya Spika kumpa nafasi pana zaidi Chenge na Wabunge wengine akiwemo Dr Slaa. Takrima tunayo tu kwenye chaguzi zetu. Watu wetu ni maskini sana wa kipato na elimu.
   
 15. masharubu

  masharubu Senior Member

  #15
  May 17, 2010
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hosea upooooo ngosha? akili za kuambiwa na bosi wako changanya na zako
   
 16. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #16
  May 17, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Njile,

  Nashukuru kwa ufafanuzi wako na nyongeza kwa mada. Tena basi alichokifanya Mkwere ni kuudhihirishia umma kuwa yeye binafsi anatumia Takrima kufanya kazi yake na kupewa dhamana, bila Takrima hawezi kufanya kazi wala bila kutoa Takrima hajiamini anaweza kuwafikia Watanzania na wakamkubali.

  Hivyo swali la kuwauliza CCM ni hili, iweje wawe na mgombea ambaye hawezi kujiuza kwa hoja bali hutembeza Takrima na kisha kujinadi?
   
 17. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #17
  May 17, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,927
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Hili la mgeni kumkarimu mwenyeji bado linanipa shida sana!
   
 18. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #18
  May 17, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  angesema ukienda kilimanjaro bwana lazma ukaribishwe mbege ningeelewa but sio wewe uwape mbege wa kilimanjaro!!
   
 19. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #19
  May 17, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  na wewe nawe yaani miaka yote unakaa unajidai kuwa nchi ina raisi hii...pole mdogo wangu
   
 20. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #20
  May 17, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 156
  Trophy Points: 160
  wWote tulidanganyika tukidhani tunaye Rais Bomba tena 'chaguo la Mungu'...

  Lakini kwa kuwa tumejua, je kuna sababu gani yakubaki naye?. Tena anatuchafulia mila zetu. Mizimu ya kichaga haitakubaliana na yeyote akayegusa misingi ya tamadani zake. Tutaweka tambiko na litamrudi! Ila ni nani basi atakayesimama? Tunazidi kuyoyomea kwa uongozi, ubora unazidi kupungua kwa kila awamu (fading quality leaders)
   
Loading...