Ajiunga na Kidato cha Kwanza akiwa na kichanga

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,895
22,659
Mwanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya sekondari Chipuputa, Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara (jina limehifadhiwa), ameripoti shuleni akiwa na mtoto mchanga.

Uongozi wa shule umesema, mtoto huyo alijifungua baada ya kuhitimu darasa la saba mwezi Oktoba mwaka jana.

USSR
---

MWANAFUNZI wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Chipuputa, Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara (jina limehifadhiwa kwa kuwa ni mtoto), ameripoti shuleni akiwa na mtoto mchanga.

Uongozi wa shule umeeleza kuwa mtoto huyo alijifungua baada ya kuhitimu darasa la saba mwezi Oktoba mwaka jana.

Wilayani hapa jana, Mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Osmondi Nkanovya alibainisha kuwapo shida hiyo alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu maendeleo ya kuripoti kwa wanafunzi waliochaguliwa kuanza masomo ya kidato cha kwanza mwaka huu.

Mwalimu Nkanovya alisema shule hiyo kwa mwaka huu wa 2023 ilipangiwa kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza 194. Kati yao, wavulana ni 93 na wasichana ni 101.

Alisema Shule ya Sekondari Chipuputa imekuwa na mwenendo mzuri wa wanafunzi kuripoti shuleni kwa mwaka huu, akibainisha kuwa hadi jana, walikuwa wameripoti ni 186. Kati yao, wavulana ni 88 na wasichana 98.

Mkuu wa shule alisema kuwa kati ya wanafunzi hao, mmoja aliripoti shuleni akiwa na mtoto mchanga.
"Inaonekana wazi kwamba hata wakati anafanya mtihani wa darasa la saba, wamanafunzi huyo aliufanya akiwa na ujauzito," mwalimu huyo alisema.

Kiongozi huyo wa shule alisema mwanafunzi huyo baada ya kuripoti shuleni na mtoto mchanga, alipokewa kisha kuelezwa kuwa kwa mwaka huu hatoweza kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza, hivyo anatakiwa kwenda kumlea mtoto wake na anarejee shuleni mwakani kujiunga na kidato cha kwanza kwa ajili ya kuendelea na masomo yake.

Mwalimu huyo alisema wameshuhudia mwamko mzuri kwa wanafunzi kuripoti shuleni kwa wakati, kukiwa na wanafunzi wanane pekee (akiwamo mwenye mtoto) ambao hawajaripoti shuleni kati ya wanafunzi 194 waliopangwa kuripoti kwenye shule hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu, Mariamu Chaurembo alisema serikali wilayani humo inaendelea kuwafuatilia wazazi na walezi ambao watoto wao hawajaripoti shuleni na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Alisema wapo baadhi ya watoto ambao walipaswa kujiunga na kidato cha kwanza na tayari wamepata ujauzito, hivyo kushindwa kuripoti shuleni na serikali wilayani hapa inaendelea kufuatilia takwimu halisi za wanafunzi ambao wamepata ujauzito ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.
 
Ni uzembe mkubwa sana na kushindwa kuwajibika kwa Serikali, wazazi na jamii kwa ujumla kwa mtoto wa darasa la saba kupata mimba.
Kwahiyo unataka Nani awajibike kwa mfano, Serikali ifanye Nini, wazazi wafanye Nini? Kumshika muweka mimba ili akakae jera ili mtoto ahudumiwe na Nani?

Sheria ya miaka 30 jela Ni butu na Haina meno na hata nikiwa Mimi mzazi siwezi kumfunga muweka mimba ,, Ni kumpiga faini muwekaji then mtoto anatafutiwa shule akasome, mwenye mtoto ndio atabeba msalaba wa kumsomesha maana possibility ya kumpa mimba nyingine huko mbele Ni kubwa.

Kwisha tusisumbuane kupelekea mahakamani na kupotezeana muda.
 
Nunuu, chapatakati ni tamu sana all the way from chipuputa.

Binti alifanya mchezo mtamu wa kupuputana
 
Pongezi kwa serikali ya mama samia suruhu hasani hakika ni jambo kubwa imefanya
 
Ni uzembe mkubwa sana na kushindwa kuwajibika kwa Serikali, wazazi na jamii kwa ujumla kwa mtoto wa darasa la saba kupata mimba.
Kwani shule ni martinity home!! Duh tunaenda wapi!? Ndio huyo mzazi anaweza kuua hako kachanga
 
Anaenda kuwaharibu wenzie waone ni jambo la kawaida kujifungua wakiwa masomoni. Upuuzi mtupu
Huko kusini ni kawaida Yao, vitoto vinaanza umalaya vikiwa vidogo sana. Kuna Kijiji jimoja jina kapuni; watoto wore wa like shule ya msingi wamewekwa panga uzazi kuepuka mimba; ngoja tusubiri matokeo yake.
 
Hili ni jambo zuri.

I hope atafika mbali, yaani kosa la kufanya mapenzi tu ndo umfukuze shule mtoto!!
 
Pongezi kwa serikali ya mama samia suruhu hasani hakika ni jambo kubwa imefanya
Mambo mengine hata sio ya kuyapongeza.

Tunahamasisha mmomonyoko wa maadili kwenye jamii zetu kisa kufurahisha wafadhili.

Ngoja usikia kijana wako uliyemsomesha kwa gharama kubwa anaolewa ndio utakuja kupongeza vizuri.
 
Ni uzembe mkubwa sana na kushindwa kuwajibika kwa Serikali, wazazi na jamii kwa ujumla kwa mtoto wa darasa la saba kupata mimba.
kama unge kuwe wewe ungeweza kulinda mtoto wa kike alie vunja ungo tatizo serikali inataka kushindana na maumbile ya mungu,mtoto wa kike akisha vunja ungo anasikia nyenge kama mama mtu mzima huo ndio ukweli
 
Back
Top Bottom