Ajiua kwa kukumbwa na ukimwi

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
266
DOTTO Manyinyi (40), mkazi wa Kijiji cha Kitalamanka, Kata ya Sazira wilayani hapa amekufa kwa kujinyonga baada ya kugundua kuwa ana ukimwi.

Habari zilizopatikana kutoka ndani ya Jeshi la Polisi wilayani hapa zinasema tukio hilo lilitokea Desemba 12 mwaka huu majira ya usiku ambapo ndugu zake waliokuwa wakiishi naye kukuta amekufa kwa kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani.

Imeelezwa chanzo cha kifo ni kutokana na mwanamke huyo kupimwa na kugundulika kuwa na ugonjwa wa ukimwi na kwamba huenda ndiyo ikawa sababu ya yeye kuchukua uamuzi huo.

Habari zaidi zinaeleza kuwa mwanamke huyo aliugua kwa muda mrefu na kwamba alipoenda kupimwa alikutwa na maambukizi ya ugonjwa huo na tangu wakati huo alikuwa akiishi kwa kuhangaika.

Katika tukio jingine, Daniel Bhoke Mwitiro (4), mkazi wa mtaa wa Bunda Stoo, amekufa maji baada ya kutumbukia katika shimo la choo.

Akielezea mkasa huo baba wa marehemu, Bhoke Mwitiro, alisema tukio hilo lilitokea Desema 12, mwaka huu, majira ya saa 10 jioni wakati mtoto huyo alipokuwa akicheza na wenzake.

“Wakati anacheza na wenzake ndipo alipotumbukia katika shimo hilo na wenzake walipoona hivyo walikimbia kwenda kumtaarifu mama yake na mpaka anatolewa alikuwa ameshafariki,” alisema.

Kutokana na tukio hilo, Jeshi la Polisi wilayani hapa limewataka wananchi waliochimba mashimo ya aina yoyote na kuyaacha wazi kuhakikisha wanayafunika hasa katika nyakati hizi ambazo mvua zinanyesha kwani ni hatari hasa kwa watoto.
 
Poor Dotto, hakupata huduma na ushuari nasaha kiasi cha kuelewa kwamba ukimwi kwa sasa sio mzigo kama ilivyokua miaka ya nyuma... Hii ni ishara tosha kwamba more need to be done

RIP
 
Poor Dotto, hakupata huduma na ushuari nasaha kiasi cha kuelewa kwamba ukimwi kwa sasa sio mzigo kama ilivyokua miaka ya nyuma... Hii ni ishara tosha kwamba more need to be done

RIP
Labda huko hakuna wataalamu wa ushauri nasaha.
 
Bado unyanyapaa ndio chanzo kikubwa cha watu kujitoa uhai. Bado ktk society zetu UKIMWI ni kama curse hivi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom