Ajiua kwa kujilipua kwa umeme Dar es Salaam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajiua kwa kujilipua kwa umeme Dar es Salaam

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 9, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  KIJANA mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Baraka Mathias Chale (37), mkazi wa Segerea Njia Panda wilayani Ilala, amekutwa amekufa kwa kujilipua kwa umeme.

  Kwa mujibu wa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Faustine Shilogile, mwili wa marehemu umekutwa ukiwa umeharibika chumbani kwake, ukiwa umeviringishwa nyaya za umeme shingoni na katika mguu wake wa kulia.

  Kamanda Shilogile alisema nyaya hizo zilikuwa zimewekwa kwenye soketi ya umeme, huku ukiwa umewashwa, kitu kinachoashiria alijiua kwa kujilipua.

  Hata hivyo alisema inasadikiwa Chale, alifariki siku tatu kabla ya mwili wake kugunduliwa hadi majirani waliposikia harufu kali kutoka chumbani kwa marehemu ambao walitoa taarifa Polisi.

  Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), wakati uchunguzi ukiendelea.

  Katika tukio jingine, Deusdedit Kajuna (58), mfugaji na mkazi wa Tabata Bima, Ilala aligundua kuibiwa nguruwe wake 18 bandani na wezi wasiofahamika na wengine 7 wakiwa wamekufa huko Tabata Ubayaubaya.

  Kwa mujibu wa Kamanda Shilogile, pembeni mwa mabanda yalikutwa mabaki ya nyama za utumbo wa nguruwe na mabaki ya chakula.

  Aidha ilikutwa mizoga mitano ya paka, panya watatu, kuku mmoja na nguruwe mmoja ambao inasadikiwa walikula mabaki hayo ya chakula/utumbo yaliyokuwa na sumu.

  Thamani ya nguruwe wote 25 ni Sh milioni 3.75. Wataalamu wa mifugo wanaendelea na uchunguzi ili kubaini aina ya sumu iliyotumika kuwateketeza wanyama hao.
   
 2. m

  mzeelapa JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 1,034
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Nikiona post zako naziruka, huna jipya zaidi ya kunakili magazeti.....?
   
Loading...