Ajitesa Ili Kuwatetea Papa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajitesa Ili Kuwatetea Papa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jun 16, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  [TABLE="width: 491"]
  [TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD]Mwanamke mmoja wa nchini Uingereza ili kupinga mauaji ya samaki aiana ya Papa duniani ameamua kuonyesha machungu yake kwa kujitundika mwenyewe kwenye ndoano kubwa ya kuwatundika papa.[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Alice Newstead huku akivuja damu mgongoni alijining'iza mwenyewe kwenye ndoano kubwa ya kuwatundika papa baada ya kuvuliwa na aliwaacha watu wengi wakiwa hawaamini macho yao.

  Alice alijitundika ndoano hiyo kubwa kwa kutumia ngozi yake ya mgongoni ambapo uamuzi wake wa kufanya hivyo ulikuwa ni kwaajili ya kupinga mauaji ya samaki aina ya papa duniani ambao wamegeuzwa kiteweo duniani na pia kutumika kwenye kutengeneza dawa za urembo wa wanawake.

  Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), jumla ya papa milioni 73 wanauliwa kila mwaka.

  Ili kuwafanya watu wamuunge mkono harakati zake za kupinga biashara ya nyama ya papa, Alice aliamua kujitundika mwenyewe kwa kutumia ndoano.

  Mwaka 2009, Alice alifanya tukio kama hili lakini uuzwaji wa nyama ya papa ulivyozidi kuendelea, Alice ameamua kuingia tena mtaani kuwakumbusha watu ukatili unaofanywa kwa papa.

  Gonga linki chini kuangalia picha hizi za kusisimua nywele zinazomuonyesha Alice akiwa amejitundika kwenye ndoano.


  1214.jpg

  Mwanamke mmoja wa nchini Uingereza ili kupinga mauaji ya Papa duniani ameamua kuonyesha machungu yake kwa kujitundika mwenyewe kwenye ndoano kubwa ya kuwatundika papa.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
Loading...