Ajirusha Toka Ghorofani Kwa nia ya Kujiua, Amuangukia Kichwani Mpita Njia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajirusha Toka Ghorofani Kwa nia ya Kujiua, Amuangukia Kichwani Mpita Njia

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Sep 4, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 4, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mji wa Viladecans ambao tukio hilo lilitokea Friday, September 04, 2009 3:26 AM
  Mwanamke mmoja wa nchini Hispania aliyejirusha toka ghorofa ya nane kwa nia ya kujiua, alisababisha kifo cha mwanaume mmoja aliyekuwa akipita chini ya jengo hilo baada ya kumuangukia kichwani. Mwanamke huyo alijirusha kwa nia ya kujiua kutoka kwenye jengo moja la ghorofa katika mji wa Viladecans uliopo karibu na mji wa Barcelona, na kutua juu ya kichwa cha mwanaume mwenye umri wa miaka 50 aliyekuwa akipita chini ya jengo hilo.

  Mwanamke huyo aliyejirusha alifariki hapo hapo na mwanaume aliyeangukiwa na mwanamke huyo alifariki muda mfupi baada ya kufikishwa hospitali.

  Mwanaume huyo alikuwa akitembea na mkewe wakati mwanamke huyo alipomuangukia kichwani, mkewe alinusurika maisha yake lakini alijeruhiwa kidogo katika tukio hilo lililotokea jumatatu majira ya saa 12 jioni.

  "Huu ni mkasa wa kusikitisha, ni njia inayotisha ya mtu kujiua" alisema msemaji wa polisi wa eneo hilo.

  Polisi walisema kwamba hawaamini kuwa mwanamke huyo alikuwa na nia ya kuwadhuru watu waliokuwa wakipita chini ya jengo hilo.

  "Hatuamini kama mwanamke aliyejirusha toka ghorofani alikuwa na nia ya kumdhuru mtu yoyote, ilitokea bahati mbaya mwanaume huyu alikuwa akipita chini ya jengo hili" alisema msemaji huyo.

  Awali taarifa za magazeti ya Hispania zilisema kuwa mwanaume huyo alikuwa ni mtalii toka Ukraine lakini polisi baadae walisema kuwa alikuwa ni raia wa Hispania toka mji jirani wa Gava.

  Polisi walikataa kutaja jina la mwanaume huyo wala la mwanamke aliyejirusha toka ghorofani kutokana na maamuzi ya familia zao.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2992258&&Cat=2
   
Loading...