Ajira zote za jeshi la polisi zianzie ngazi ya Diploma

Zaidi ya Polisi 20 ni PhD holders
Zaidi ya Polisi 100 wana masters
Zaidi ya Polisi 6000 Tanzania wana digrii,
Zaidi ya Polisi 1000 wana diploma
Zaidi ya Polisi 4000 ni form VI

Waliobaki ndo form iv na Std VII wasiozidi 500 kwa sasa.

Kama unaona polisi wanafanya vibaya si kwa sababu wote hawana Elimu, ila ni kwa sababu si chombo huru toka kwenye mikono ya wanasiasa. Hao uliosikia wameteliwa jana wanakwenda kutoa amri kwa Polisi kufanya chochote wanachoona wao kinafaa, na kama OCD husika hajiongezi ndo utakuta madudu na mafyongo kama ya Kaliua juzi ambako DC anasema "familia ilipanga mtoto wao afe kwa moto ili kuikomoa serikali".
Jambo la kuzingatia ni, Kuna masomo ya vyeti na masomo ya Kazi.
Tujiulize vyuo vya polisi vinafundisha Nini!!
Nafahamu kuwa ili uweze kuajiriwa katika jeshi lolote lazima ufuzu mafunzo ya jeshi husika, na ili upande cheo unapaswa kufuzo mafunzo ya cheo stahiki.
Haiingii akilini ofisa wa jeshi kutofaha taratibu za kazi yake. Wanamakusudi hawaaa ya kulitia jeshi letu aibu na kufedhehesha vyuo vyetu vya mafunzo ya jeshi ambavyo vimeaminiwa na kuhudumia mataifa mengi.
 
Una undugu au urafiki na Simbachawene ?
Kazi ya jeshi ni kazi ya kujitolea Kama ilivyo kada ya ualimu

"Kazi kubwa maslahi madogo"

Ukiweka wasomi wengi wataangalia maslahi yao kuliko kuangalia kazi
 
Tatizo lako mawazo yako yanatokana na njaa kali ya tumboni na sio kichwani.
Sio kila ajira za kweka kila mtu, mambo mengine ni nyeti sana wewe kilaza yanahitaji watu smart.
Acha ubinafsi. Kwa kuwa wewe umefikia kiwango hicho ndio unaona wale ambao hawakufika level hiyo hawapaswi kupata ajira hizo,unajiangalia wewe tu kama mtu mwenye pesa anapendekeza watu watoe mchango mkubwa kuliko uwezo wao kwa kuwa yeye anaumudu, waache wanaomaliza form four wapate pa kuanzia maisha zamani watu walikuwa wanamaliza la saba wanapata ajira ndio waliokufikisheni hapa mlipo.

Huko katika jeshi la polisi wenye hizo diploma, degree na masta wewe unadhani hawapo au umeamua kuwadharau polisi Tz.
 
Umemsikiliza Simbachawene juzi kwenye kipindi cha dakikia 45?
Police kuna graduate wa kutosha na dip nyingi sana. So kwenye mgawanyo wa majukumu lazima F4 nao wawepo
 
Ama kweli viongozi wa nchi huwakilisha aina ya watu wanaowaongoza, tuna safari ndefu kama nchi.
Mods fungeni huu uzi hapa.
Hao wenye diploma wataweza kukaa magetini? Kulinda benk?

Kufukua makaburi kama kuna kesi za mtu kuuwa na kuzika?
 
Jiite mchawi mweusi
Mbona hilo lilishawekwa wazi kuwa asilimia kubwa ya majeshi yana hitaji watu wenye elimu ndogo ya form 4, kwani ndio wenye majukumu mengi kwenye majeshi kulinganisha na hao wasomi, hao wasomi huwa ni wasumbufu sana, mtu anatafuta kazi kama kujiegesha tu, huko anakosubiria penye maslahi mazuri tu pakitiki anakimbia, kingine wanakuwa wasumbufu sana kudai maslahi, mala kwenda kutaka kuongeza elimu.

Lakini ukimchukua form 4, hadi aje ajiendeleze apate digrii sio leo, kama ni kwata ameshapigishwa sana, na huwa wanakuwa wavumilivu.
 
Unazungumzia mataifa yapi?
Polisi/jeshi ni kazi za amri na sio kazi za kutumia akili nyingi, mtu yeyote mwenye akili timamu, mkakamavu na mwenye uzalendo anaweza kua polisi/mwanajeshi.
 
Stendi ipi?
Hivi mtu mwenye digree ukampe kazi ya kulinda atm bank kweli si bora nibaki stendi napiga debe?

Tena hii kuajiri wasomi wasomi kwenye vyombo vya ulinzi ndio wanasababisha maadili yanapungua maana mtu ana elimu yake utamwambia nini.

Mi naona waajiri wala ma feria kabisa ili wawapelekeshe vizuri maana wanakuwa na adabu na utii na nidhamu ya kazi kuliko hiyo misomi alafu kicwani hamna kitu.

Angalia wastaafu wote kwenye vyombo vya ulinzi wale wa enzi za mwalimu walivyo na nidhamu na weledi huko mtaani alacu ulinganishe na hawa wa saa hivi uone tofauti
 
Ukiwa na Diploma unakosa nguvu za kukaa getini na kulinda benki?
Hizo nchi nyingine ambazo polisi wenye degree wanafanya hizi kazi ni miujiza?
Hao wenye diploma wataweza kukaa magetini? Kulinda benk?

Kufukua makaburi kama kuna kesi za mtu kuuwa na kuzika?
 
Zaidi ya Polisi 20 ni PhD holders
Zaidi ya Polisi 100 wana masters
Zaidi ya Polisi 6000 Tanzania wana digrii,
Zaidi ya Polisi 1000 wana diploma
Zaidi ya Polisi 4000 ni form VI

Waliobaki ndo form iv na Std VII wasiozidi 500 kwa sasa.

Kama unaona polisi wanafanya vibaya si kwa sababu wote hawana Elimu, ila ni kwa sababu si chombo huru toka kwenye mikono ya wanasiasa. Hao uliosikia wameteliwa jana wanakwenda kutoa amri kwa Polisi kufanya chochote wanachoona wao kinafaa, na kama OCD husika hajiongezi ndo utakuta madudu na mafyongo kama ya Kaliua juzi ambako DC anasema "familia ilipanga mtoto wao afe kwa moto ili kuikomoa serikali".
data za uongo mejeshi ya wenzxetu yana wasomi wewngi sana sema tuna fikra za kitumwa tu
 
 
Huo ndio ukweli ulivyo!!na utabakia hivyo hivyo!!mwenye degree huwezi kumzungusha kwenye lindo usiku kucha, mala akalinde bank!!akipata tu nafasi nyingine ya kazi ni rahisi kwenda huko,
Sasa ndio watujazie matutusa kwenye jeshi la polisi ambao kazi yao kila siku ni kuwavizia na kuwaua wafanyabiashara wa madini? Mkuu kumbuka hata wewe ndugu yako anaweza kuuwawa na polisi wakati wowote. Inauma sana.
 
Back
Top Bottom