Ajira za Watanzania ziko mikononi mwa wageni

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
makopo.jpeg

TANGU kuchaguliwa kwa serikali ya awamu ya tano ya uongozi Tanzania chini ya Rais John Pombe Magufuli kumekuwa na wimbi la wageni wasio na vibali kuondolewa nchini.

Pasi na shaka, uamuzi huu wa kuwaondoa wageni wasio na vibali kufanya kazi nchini ni jambo la msingi kabisa. Lakini wasiwasi ni kwamba, wale wanaoondolewa wasio na vibali ndio ambao wameshika nyanja muhimu za uzalishaji Tanzania ama ni wavuja jasho wa kawaida tu?

Kwa habari zaidi, soma hapa => Ajira za Watanzania ziko mikononi mwa wageni | Fikra Pevu
 
Huu uzi umfikie Jenista Mhagama, nchi imejaa wahuni, matapeli, vibaka, wasokota bangi, na vibari wamepata kutoka kwenye wizara yako, vya kufanya hivyo hapa nchini mwetu.

Inauma sana Mh waziri nchi yetu, kila kitu cha kwetu ila wizara yako inakaribisha wawekezaji wahuni, wavuta bangi na wasio na Elimu yoyote?

Janista Mhagama ebu toka ofisini njoo na ufanye operasheni kabambe, iite jina la KAMATA MWIZI MEN, na utakamata wengi.

Mimi ni miongoni mwa vjiana wa kitanzania tunaorandaranda mtaani kutafuta kazi na taaluma tunayo, na uzoefu tunao alafu wizara yako inawapa watu vibari hawana hata taaluma kuja kujifanya wawekezaji pasipo hata kuangalia viwango vya elimu zao.

Naomba ufanye yafatayo haraka Janesta Mhagama.

Kwanza watangazie wageni hasa wachina wote, kuanzia leo wote waende maofisini kwao na vibari vya vya ajira.

Pili wambie kuwa wawe na vyeti vya taaluma zao hapo hapo ofisini.

Tatu, yeyote anayefanya kazi, awe na job disripition yake aimbatanaishe na cheti cha elimu yake.

Nne, wewe tuma wanaotoa vibari wakague ofisi waaangalie hakuna mtu yeyote anayeweza kufanya kazi wanazozifanya wawekezaji hao?

Nitakupa ushikiriano mkubwa sana mkuu, tafadhali nipm tu ntakupeleka kwenye ofisi zote za kichina, nyingi nazijua, ila kwa kuanza anza na China Commerical Bank,IT PLAZA Pale, kuna ofisi nyingi za kichina, njoo fanya operesheni nakwambia kabisa, utatengeza ajira si chini ya elfu moja kwa vijana wako ndani ya lisaa limoja.

Inauzunisha huku, TAESA wanatafutia watu kazi, alafu kuna watu wasio waaminifu wanatoa vibari kwa machinga wa kichina kwani Bongo wamakonde wamekwisha kuwa machinga?
 
Naunga hoja mkono ifanywe ukaguzi tena na nimpe pole Mama alieteuliwa Kamishna wa Kazi,watu walishapiga pesa ndefu kutoa hivyo vibali.Wanacholalamika Watanzania ni kweli tembeeni mfanye face to face na wenye vibali ukweli mtaufahamu
 
Back
Top Bottom