Ajira za vijana na uelekeo wetu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajira za vijana na uelekeo wetu.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MTAZAMO, Jun 22, 2012.

 1. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Leo nimepita maeneo ya Ubungo na kuona mshikemshike kati ya mgambo na wamachinga.Hili halikunishangaza hata kidogo kwani tumeshazoea kipute hicho.Kilichonisukuma kuandika hili ni baada ya kujiuliza lini vita ya machinga na mgambo itakwisha? Halmashauri zitakuwa zinaajiri na kulipa mgambo kwaajili ya kufukuzana na wamachinga mpaka lini maana ndio kazi yao kubwa.

  Tokea tuliporuhusu soko huria biashara ya uchuuzi imekuwa ikikua kwa kasi ya ajabu.moja ya sababu kubwa ni kutokuwa na uchumi unaoweza kutoa fursa za ajira za kueleweka za vijana (hapa simaanishi ajira za mishahara mikubwa).
  Tabaka la vijana wachuuzi linakuwa kwa kasi maana tulizoea vijana walioshindwa kuendelea na sekondari lakini sasa hata wale wa sekondari hadi form six wanafanya shughuli hizi kutokana na ugumu wa maisha.

  Lazima tukubali kuwaondoa kabisa wamachinga kwa aina hii ya uchumi ni ndoto.Hata mbinu ya kuwatengea maeneo imeshashindwa haitekelezeki bora tuwaache ili tujenge uchumi mzuri utakaoondoa biashara hii automatically otherwise mgambo endelezeni maigizo ya kukimbizana kama mchezo wa kitoto wa kombolela!

  Imefika mahala serikali imeamua kuhalalisha usafiri wa pikipiki kubeba abiria kwasababu kwa kasi ya ajabu ya kundi kubwa la vijana wamejiajiri huko lakini hilo ndio suluhisho? Tuna mkakati gani? Madhara ya matumizi ya pikipiki hizi kubeba abiria tumetafakari pia? mpango wa kuwaondolea kodi ni mzuri lakini umefanyika utafiti wa matokeo yake na njia mbadala kuwasaidia vijana hawa?

  Bodaboda zimeanza kuadhiri hata kilimo na mfano nilipokwenda kijijini kwetu mara ya mwisho wazee wengi walikuwa wakilalamika mavuno kidogo sababu vijana wengi wakishavuna mazao kama kahawa wananunua bodaboda alafu wanaachana na kilimo.nilipohoji vijana wengi wakaniambia bora bodaboda inawapa kipato cha uhakika kwa siku kuliko kilimo ambacho kila kukicha bei inashuka! Bodaboda zimefurika hadi vijijini na asilimia 99.9% ni vijana.

  Ndugu zangu mfumo wa ajira za vijana (wasomi na wasiowasomi) ni mbovu mno na hakuna mkakati wa kueleweka kurekebisha mfumo wa uchumi hasa viwanda vyetu.Tuache kulalamika maana Chadema wanalalamika,CCM wanalalamika (wengi kinafiki),wananchi wanalalamika! Lakini hatuna suluhisho zaidi ya kutishiana tu "vijana wasio na ajira ni bomu",wizara inayohusika na vijana ni kama haipo(ni moja ya wizara mfu kabisa).Wanasiasa wanaendelea kutoa ahadi na sisi wananchi tunaendelea kuwapigia makofi!

  Natoa wito binafsi kwa wananchi wenzangu,tubadilike na tuanze kudai majibu ya utekelezaji wa ahadi za hawa wanasiasa,pasipo na majibu tuwawajibishe viongozi wetu kwa nguvu ya umma.Vijana wanakosa uelekeo kila kukicha kwasababu ya uongozi mbovu usio na maono.sasa tuseme basi,watuambie sasa wamefanya nini na sio watafanya nini maana sisi ndio tuliowapa nafasi na ndio mamlaka ya mwisho kabisa.
   
Loading...