Ajira za utendaji wa mtaa/vijiji, ni kweli Tanzania inathamini elimu?

Ukilipwa TGS B utakubali ??

Utaacha kulalamika ??
Na kwa nini alipwe hiyo TGS B, kinachomata ni elimu ya mtu aliyekaa kwenye nafasi au ni ngazi ya eneo analofanyia kazi.....yaani ukimpeleka injinia akafanyie kazi kijijini, je, utamlipa kwa elimu yake au utamlipa kama mtu anayefanya kazi kijijini.....
 
Haijui hiyo ndio maana analilia utendaji wa kijiji
Kuna mwingine humu alianzisha thread kwamba ameajiriwa na mahakama halafu analipwa TGS B wakatinana Diploma.

Lakini angeambiwa wanahitaji watu wenye cheti angesema yeye ni Diploma anabaguliwa.
 
Na kwa nini alipwe hiyo TGS B, kinachomata ni elimu ya mtu aliyekaa kwenye nafasi au ni ngazi ya eneo analofanyia kazi.....yaani ukimpeleka injinia akafanyie kazi kijijini, je, utamlipa kwa elimu yake au utamlipa kama mtu anayefanya kazi kijijini.....
Scale za Watendaji wa kata na vijiji unazijua ??
 
Ukilipwa TGS B utakubali ??

Utaacha kulalamika ??
Hawa wenye shahada wakilipwa hiyo watajikuta wanashindwa kuandaa taarifa za mapato na matumizi kwa kuwa kila robo itakuwa Salio ZERO. Watakula kila kinachoingia kwenye mapato ya kijiji.
 
Hawa wenye shahada wakilipwa hiyo watajikuta wanashindwa kuandaa taarifa za mapato na matumizi kwa kuwa kila robo itakuwa Salio ZERO. Watakula kila kinachoingia kwenye mapato ya kijiji.
In short watakuwa watu wa malalamiko tu.

Kuna vijiji viko porini sana.

Wataanza kulalamika maeneo ya kazi na mshahara. Hakuna kazi itafanyika
 
Scale za Watendaji wa kata na vijiji unazijua ??
Ndo nilichokisema huko juu, kinachokwepa hapo ni kubana mishahara siyo kwamba hayo maeneo yanastahili kuongozwa na watu waliokwepa umande, uwe unaelewa.....
 
Wewe omba kazi hiyo
Kwani wamekunyima sababu una shahada?
Kigezo kimojawapo ni kua na astashahada,sasa anaombaje huku akiwa na shahada si atawafanya hata wachambuzi wa maombi waone wanao uhalali wa kutoajili wenye shahada,kwasababu hata maelekezo tu hawazingatii.
 
Na kwa nini alipwe hiyo TGS B, kinachomata ni elimu ya mtu aliyekaa kwenye nafasi au ni ngazi ya eneo analofanyia kazi.....yaani ukimpeleka injinia akafanyie kazi kijijini, je, utamlipa kwa elimu yake au utamlipa kama mtu anayefanya kazi kijijini.....
Atalipwa TGS B kwa sababu wanaotakiwa ni wenye astahahada mwenye shahada akiipata hiyo kazi basi kasoma kuanzia astahahada hadi shahada. Kama ana shahada na hana astahahada akiupata utendaji wa kijiji ni bahati yake na atalipwa kama mwenye astahahada.
 
Ndo nilichokisema huko juu, kinachokwepa hapo ni kubana mishahara siyo kwamba hayo maeneo yanastahili kuongozwa na watu waliokwepa umande, uwe unaelewa.....
Anyway, kila Mwajiri ana utaratibu wake wa kuajiri kulingana na uzoefu wake.

Sasa hivi waajiri wengi wanaa halia uwezo wa ku-meet targets na siyo elimu.

Huwezi kuwalaumu Clouds au Wasafi kutokuajiri mtu mwenye Degree ya Mass Communication au Jornalism na badala yake wanaajiri kina Juma Lokole.

Yawezekana kwenye Utendaji watu wa ngazi hizo wanafanya vizuri zaidi na ndio maana serikali ilianzisha chuo kabisa cha SERIKALI ZA MITAA, HOMBOLO ingawa kwasasa hata watu waliosoma utawala na sheria wanachukuliwa.
 
Kigezo kimojawapo ni kua na astashahada,sasa anaombaje huku akiwa na shahada si atawafanya hata wachambuzi wa maombi waone wanao uhalali wa kutoajili wenye shahada,kwasababu hata maelekezo tu hawazingatii.
Mkuu hii point ni KUBWA MNO, wasipokuelewa basi degree zetu zichunguzwe.
 
Nimefuatilia sana posti za ajira za utendaji wa mtaa au vijiji sijawahi kuona wakiunganisha kigezo cha shahada kwenye sifa za kazi hiyo na nyingine 50 zimetangazwa wilaya ya Ilemela wanahitaji astashahada tu

Naona kusoma sana sasa hakuna maana Tanzania enzi za mwl Nyerere alithamini sana wasomi hata kipindi cha Rais JK ila kwasasa ni kupoteza muda na kufanya kila msomi kuwa mwanasiasa.
Hizo ni kwa Ajili ya WATOTO wa WANYONGE hata kama Ana Degree 3
 
Yaani mtu umesoma SHAHADA YAKO halafu unalilia kwenda kuwajibika kwa mwenyekiti wa kijiji? Ambao wengi wao ni la Saba. Walioweka hivyo vigezo waliyajua yote haya kwamba kuna ngazi wakiajiriwa hao wasomi ni kupeleka migogoro katika jamii.
 
Serikali ipo sahihi, kumwajiri mtu mwenye shahada kuwa mtendaji wa kijiji/kata ni anasa na matumizi mabaya ya taaluma. Shahada ni kiwango kikubwa sana cha elimu, by the way umeona ngazi ya mshahara wa mtendaji wa kijiji?? Wewe tafuta kazi ya saizi yako...!
Kwa hiyo kuongoza wanakijiji elfu tano ni kazi ndogo siyo? Kitovu cha kwanza cha maendeleo hapa nchini ni vijiji au mitaa. Ni maajabu sana kuweka mtu mwenye cheti, ambaye hana hata uwezo wa kutafsiri sheria mbalimbali za nchi, kuongoza watu elfu tano. Ndiyo maana vijiji vingi vimedumaa kwa umasikini.
 
Basi wewe jiongoze wewe uwe tajiri wa mfano kuliko kusubiri ukaongoze kijiji kitajirike.
 
Na shahada yako wakupe 390K utawezana?

Kwanza now days hawachukui astashahada( cheti) wanachukua level 5 ambayo ni diploma 1.

Kama una wito na kuwa VEO/ MEO chukua vyeti vyako vya secondary ukasome., ganda lako la bachelor weka kabatini.
 
Yaani mtu umesoma SHAHADA YAKO halafu unalilia kwenda kuwajibika kwa mwenyekiti wa kijiji? Ambao wengi wao ni la Saba. Walioweka hivyo vigezo waliyajua yote haya kwamba kuna ngazi wakiajiriwa hao wasomi ni kupeleka migogoro katika jamii.
True.
 
Back
Top Bottom