Ajira za utendaji wa mtaa/vijiji, ni kweli Tanzania inathamini elimu?

Na shahada yako wakupe 390K utawezana?

Kwanza now days hawachukui astashahada( cheti) wanachukua level 5 ambayo ni diploma 1.

Kama una wito na kuwa VEO/ MEO chukua vyeti vyako vya secondary ukasome., ganda lako la bachelor weka kabatini.
Sasa hivi kuna vijana wengi sana ni VEO/WEO.

Na hawa watu wana akazi nyingi sana zinazohusisha watu kila siku.

Bila VEO/WEO kazi za DEDs haziendi.

Ila sasa vijiji na kata nyingi ni porini mnooo ndio maana kazi hizi zinahitaji WITO.

Otherwise unaweza kuajiriwa kila siku ukawa unalalamika unaishi porini, hakuna nyumba na mshahara ni mdogo.
 
Kwa hiyo kuongoza wanakijiji elfu tano ni kazi ndogo siyo? Kitovu cha kwanza cha maendeleo hapa nchini ni vijiji au mitaa. Ni maajabu sana kuweka mtu mwenye cheti, ambaye hana hata uwezo wa kutafsiri sheria mbalimbali za nchi, kuongoza watu elfu tano. Ndiyo maana vijiji vingi vimedumaa kwa umasikini.
Nani kakudanganya kuwa mwenye astahahada sio msomi? Nani kakudanganya mwenye shahada ndio msomi?
 
Nimefuatilia sana posti za ajira za utendaji wa mtaa au vijiji sijawahi kuona wakiunganisha kigezo cha shahada kwenye sifa za kazi hiyo na nyingine 50 zimetangazwa wilaya ya Ilemela wanahitaji astashahada tu

Naona kusoma sana sasa hakuna maana Tanzania enzi za mwl Nyerere alithamini sana wasomi hata kipindi cha Rais JK ila kwasasa ni kupoteza muda na kufanya kila msomi kuwa mwanasiasa.
Mkuu nakibalia na wewe. Enzi za Mwalimu tuliona wenye digrii (BA) wakiajiriwa mameja wa Vijiji. Leo wapo wengi wenye digrii hizo kwa nini wasijiriwe? Kama tumekubaliana miradi ya maendeleo iibuliwe kuanzia Vijijini, maana wao (wanakijiji ndio wanaojua vipaumbele vya miradi yao) kwa nini tusiwajiri vijana hawa? Au utaratibu huu haupo tena?
 
Naona labda serikali imeshajiridhisha kuwa hamna tofauti kubwa sana ya kigezo za kiutendaji kati ya mtu mwenye astashahada na mwenye shahada.

Sana sana mwenye shahada atataka alipwe pesa ndefu kuliko mwenye astashahada kwa majukumu na utekelezaji ule ule anaweza kuufanya mwenye cheti a.k.a astashahada
Tunaangalia kupewa kipaumbele elimu
 
Nimefuatilia sana posti za ajira za utendaji wa mtaa au vijiji sijawahi kuona wakiunganisha kigezo cha shahada kwenye sifa za kazi hiyo na nyingine 50 zimetangazwa wilaya ya Ilemela wanahitaji astashahada tu

Naona kusoma sana sasa hakuna maana Tanzania enzi za mwl Nyerere alithamini sana wasomi hata kipindi cha Rais JK ila kwasasa ni kupoteza muda na kufanya kila msomi kuwa mwanasiasa.
tatizo wasomi ukiwapeleka wakawe watendaji wa kijiji nanjiringi huko ndanindani hawataa wadumu huko wanatafuta uhamisho warudi mteni wasomi wengi wa tz bado tunakasumba ya kuamini kama umeshasoma basi unapaswa ukae sehemu nzuri kazi nzuri mjini na n.k
 
Back
Top Bottom