Ajira za utendaji wa mtaa/vijiji, ni kweli Tanzania inathamini elimu?

Big Eagle

JF-Expert Member
May 3, 2020
549
1,000
Nimefuatilia sana posti za ajira za utendaji wa mtaa au vijiji sijawahi kuona wakiunganisha kigezo cha shahada kwenye sifa za kazi hiyo na nyingine 50 zimetangazwa wilaya ya Ilemela wanahitaji astashahada tu

Naona kusoma sana sasa hakuna maana Tanzania enzi za mwl Nyerere alithamini sana wasomi hata kipindi cha Rais JK ila kwasasa ni kupoteza muda na kufanya kila msomi kuwa mwanasiasa.
 
balimar

JF-Expert Member
Sep 18, 2015
6,160
2,000
Naona labda serikali imeshajiridhisha kuwa hamna tofauti kubwa sana ya kigezo za kiutendaji kati ya mtu mwenye astashahada na mwenye shahada.

Sana sana mwenye shahada atataka alipwe pesa ndefu kuliko mwenye astashahada kwa majukumu na utekelezaji ule ule anaweza kuufanya mwenye cheti a.k.a astashahada
 
M kathias

JF-Expert Member
Jun 13, 2017
2,789
2,000
Sasa unataka awa wenye astashahada wale wapi?
Ndio ajira zao hizo kwasasa.
 
DustBin

JF-Expert Member
Jun 3, 2021
420
500
Nimefuatilia sana posti za ajira za utendaji wa mtaa au vijiji sijawahi kuona wakiunganisha kigezo cha shahada kwenye sifa za kazi iyo na nyingine 50 zimetangazwa wilaya ya ilemela wanahitaji astashahada tu...
Serikali ipo sahihi, kumwajiri mtu mwenye shahada kuwa mtendaji wa kijiji/kata ni anasa na matumizi mabaya ya taaluma.

Shahada ni kiwango kikubwa sana cha elimu, by the way umeona ngazi ya mshahara wa mtendaji wa kijiji?? Wewe tafuta kazi ya saizi yako...!
 
DustBin

JF-Expert Member
Jun 3, 2021
420
500
Wewe omba kazi hiyo
Kwani wamekunyima sababu una shahada?
Akidi inasema ikiwa kigezo cha kazi ni astashahada.., wewe ukiomba kwa cheti cha shahada au shahada ya uzamili unakua umeji disqualify mwenyewe
 
mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
14,458
2,000
Akidi inasema ikiwa kigezo cha kazi ni astashahada.., wewe ukiomba kwa cheti cha shahada au shahada ya uzamili unakua umeji disqualify mwenyewe

Unaweza kutwekea tangazo na sisi tuombe?
 
zipompa

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
7,161
2,000
Serikali ipo sahihi, kumwajiri mtu mwenye shahada kuwa mtendaji wa kijiji/kata ni anasa na matumizi mabaya ya taaluma. Shahada ni kiwango kikubwa sana cha elimu, by the way umeona ngazi ya mshahara wa mtendaji wa kijiji?? Wewe tafuta kazi ya saizi yako...!
Mambo ya mshahara yanahusiana vp? Serikali si Ina ngazi zake za mishahara kwamba kwenye shahada atalazimisha apewe milioni ikiwa anaomba anajua mshahara ni elfu 80

Serikali iruhusu wote waombe, atakaye ibuka kidedeo apewe shavu.
 
  • Thanks
Reactions: cmp

DustBin

JF-Expert Member
Jun 3, 2021
420
500
Mambo ya mshahara yanahusiana vp? Serikali si Ina ngazi zake za mishahara kwamba kwenye shahada atalazimisha apewe milioni ikiwa anaomba anajua mshahara ni elfu 80

Serikali iruhusu wote waombe, atakaye ibuka kidedeo apewe shavu.
Kila kazi ina level yake ya taaluma mkuu. Utendaji wa kijiji waacheni vijana wetu wenye astashahada wajimwae mwae jamani. Ninyi na mashahada yenu mkapambane huko kwenye maelfu ya watu wakati nafasi moja
 
zipompa

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
7,161
2,000
Kila kazi ina level yake ya taaluma mkuu. Utendaji wa kijiji waacheni vijana wetu wenye astashahada wajimwae mwae jamani. Ninyi na mashahada yenu mkapambane huko kwenye maelfu ya watu wakati nafasi moja
Hahahaha serikali inataka ua watu wake hii
 
Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
53,859
2,000
Nimefuatilia sana posti za ajira za utendaji wa mtaa au vijiji sijawahi kuona wakiunganisha kigezo cha shahada kwenye sifa za kazi iyo na nyingine 50 zimetangazwa wilaya ya ilemela wanahitaji astashahada tu...
Tangia meko awe rais hizo ndio ajira wanazotoa
Hata zile ZA tra ZA juzi ziliyeyuka
 
Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
7,905
2,000
Kinachokwepwa hapo ni wage bill ndugu, wanaona wakiajiri certificate watawalipa mshahara mdogo na hivyo kubana fungu la mishahara, wakati kiuhalisia kwa nafasi yoyote ile ya kiutumishi sifa standard ni ngazi ya elimu kwa kiwango cha shahada.

Hao wenye certificate na diploma wanabaki kuwa wasaidizi tu, huwezi kuwachukulia kama ndo watendaji wanaotakiwa kufanya final decisions.

Ukiona kiongozi anaanza kuegemea machifu ujue elimu na utaalamu hauna nafasi tena zaidi ya ndumba.
 
the12bdi

JF-Expert Member
Oct 12, 2018

Katika huo utendaji wa kijiji, degree Wala Haina chake na hausomewi, kinachotakiwa mtu uwe na uwezo binafsi wa kuratibu mambo hata la Saba kina msukuma wanafanya vizuri sana. Kingine mtazamo wa wasomi wetu mnawaza maslahi makubwa sasa tuwape utendaji wa vijiji nyie wenye shahada ili mkavifilisi? Hapana! Acha tuajiri hao astahahada ambao wataridhika na kinacholipwa. Wenye shahada kazi zenu kuanzia ngazi ya kata.
 
Na elimu yako ya la saba hili ndo umeona la maana kuchangia!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom