Ajira za udom mbona hazipitii sekretarieti ya ajira? Serikali mulika udom | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajira za udom mbona hazipitii sekretarieti ya ajira? Serikali mulika udom

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by imamu, Jun 27, 2012.

 1. i

  imamu Member

  #1
  Jun 27, 2012
  Joined: May 20, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwaka wa ajira uliopita UDOM walituita kwenye interview. Hawakuchagua wenye sifa. Walituita watu wote tulioomba kazi. Matokeo yake kada moja ya nafasi 4 tulijikuta watu zaidi ya 5,000 tulienda kwenye interview. Pamoja na hayo, walitufanyisha interview ya kuandika kwa madai kuwa watakaofaulu wangewaita kwa interview ya pili ya kuongea. Cha ajabu waliwaita watu waliowataka wao tena kimya kimya bila kutangaza popote. Sisi wengineo bado tunasubiri hadi leo na tumesikia wenzetu wameshaitwa kazini. Sasa kwanini walituita wengi vile? kwanini hawakuchagua wenye sifa tu? Haya tuseme kwani wao hawafuati sheria ya serikali ya kupitishia ajira kwenye sekretarieti ya ajira? Serikali iwabane wapitishie ajira zao huko bwana waache kutusumbua. Utaratibu wa ajira zinatangazwa, watu wanaomba na wenye sifa wanaitwa kwa interview na kisha wanaitwa kazini. Hatua zote hzo zinatangazwa katika vyombo vya habari. Kwanini wao wasifanye hivyo? Serikali iwamulike kazi kwanza zitangazwe kupitia sekretarieti ya ajira kuepuka upendeleo kama huo. Waache mtindo wao huo. Na mwaka huu tena wakituita twataka posho ya nauli sie.
   
 2. MAKOLE

  MAKOLE JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mimi sijakuwelewa unachomaanisha. Kwani walikuiteni au mlikwenda wenyewe? Nadhani kulalamikia kluwa mlikuwa wengi zaidi ya 5000 halikuwa tatizo la Udom, ila ni tatizo la ukosefu wa ajira kwa Tz wenyewe
   
 3. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,204
  Likes Received: 258
  Trophy Points: 180
  Wafanya kazi na wanafunzi wa Udom hawasikilizwi utakuwa wewe muombaji wa kazi...... Kasome vizuri sheria iliyoanzisha sekretarieti kama inahusu na wakala na taasisi za serikali zinazojitegemea kama Vyuo Vikuu
   
 4. m

  mkereketwamkereketwa Member

  #4
  Jun 30, 2012
  Joined: May 7, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani UDOM inaharibiwa na waisilamu tuu na si kingine...​
   
 5. m

  mkereketwamkereketwa Member

  #5
  Jun 30, 2012
  Joined: May 7, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lugha hii ni ya mkurugenzi wa utawala, angalia udom inavyoajiri punguani...bosi mzima una comment kwenye jamii forum?? Shame shame shame shame ptyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu, hovyooooooooooooooooooo
   
Loading...