Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,564
- 7,973
- Thread starter
- #21
Mkuu Mwita Maranya siku hizi mashirika ya umma karibu yote yanatumia mtindo huo wa hovyo kupitiliza.
Ukitia mguu AUWASA Mamlaka ya Maji jijini Arusha yuko afisa mwajiri mpare/mchagga yeye anahakikisha tatizo la ajira kijiji alichozaliwa na familia yake linamalizwa kama si kupunguzwa na uwepo wake AUWASSA.
Sasa mkuu ni kwanini tuendelee kufumbia macho vitendo kama hivi vinavyofanywa na wahuni wachache kwa manufaa yao na familia zao? mashirika ya umma na idara/wizara za serikali lazima ziwe na utaratibu unaowawezesha watanzania wote kuajirika bila vikwazo.
Nadhani katika hili tuna jukumu la kufanya nadhani tunalazimika sasa kuwamulika wale wote wanaotumia ofisi za umma kwa manufaa yao binafsi kwa kuwabagua wengine na kuwapendelea ndugu, jamaa na marafiki zao.