Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,564
- 7,973
Salam WanaJF,
Kwa muda mrefu kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wadau wa sekta ya usafirishaji juu ya vitendo vya rushwa na ubabe vinavyofanywa na watendaji ama watumishi wa mizani zilizopo maeneo mbalimbali nchini kwa upande mmoja. Kwa upande wa pili kumekuwa na malalamiko toka kwa wafanyakazi wa mizani hizo hasa weighbridge operators na shift incharges kulalamikia vitendo vya unyanyasaji wanavyofanyiwa na mameneja wa mizani hizo katika mikoa mbalimbali nchini.
Kutokana na hali hiyo nimelazimika kufanya kautafiti kadogo ili walau kujua ukweli wa tuhuma hizi. Kuna vitu vichache namalizia kabla sijaweka bayana findings zangu kuhusu malalamiko hayo. Muda si mrefu nitaweka hapa ripoti yangu hapa JF.
Nikirudi katika mada ya leo kama kichwa cha habari kinavyosomeka; hivi karibuni Mameneja wa Tanroads wa mikoa yenye mizani (weigh bridges) wamekuwa wakitoa matangazo ya ajira kwa nafasi za Shift Incharge na Weigh Bridge Operators. Matangazo ya hivi karibuni kabisa ya ajira hizo ni katika mikoa ya Mwanza, Pwani na Morogoro.
Mojawapo ya sifa za lazima kwa waombaji ni kama ifuatavyo:
1. Shift Incharge;
a) Awe na elimu ya shahada ya kwanza [bachelor] ama Stashahada ya juu [Advanced Diploma] katika fani yoyote toka taasisi ya elimu ya juu inayotambulika na
b) Awe na umri kati ya miaka 35 hadi 40
2. Weighbridge Operator;
a) Awe na elimu ya Fundi Mchundo[FTC] katika fani za Umeme [Electrical Eng.], Ujenzi [Civil Eng.] au Mitambo [Mechanical Eng.] na
b) Awe na umri usiozidi miaka 35.
Kimsingi sina tatizo kabisa na kigezo cha elimu, isipokuwa hapo kwenye umri. Nimekuwa nikijiuliza masawali kadhaa bila kupata majibu, nikaona ni vizuri niwashirikishe maGT hapa ili tusaidiane kulitazama suala hili kwa pamoja. Vijana wengi sasahivi wanahitimu shahada/ stashahada za juu wakiwa na umri kati ya miaka 22-25, na wapo vijana wengi sana wenye uwezo mkubwa wa kushika nafasi za majukumu makubwa hata kuliko hiyo nafasi ya shift incharge. Na kwa kuwa wenye umri wa miaka 35 hadi 40 ambao wana elimu ya kiwango cha shahada/stashada ya juu watakuwa ni watu wenye kazi zao mahali kwingineko, hivyo basi kunakuwa hakuna mantiki ya kuweka kigezo cha umri mkubwa kiasi hicho katika ajira kama hizi.
Kwa mtazamo wangu naona kama kuna ubaguzi kama si upendeleo wa dhahiri katika ajira hizi za Tanroads, sina uhakika kama watu wenye umri huo mkubwa kiasi hicho ndio pekee wanaweza kuhimili majukumu ya kazi ya shift incharge. Nadhani hapa kuna mazingira ya mameneja wa Tanroads mikoa ama wizara ya ujenzi ama Tanroads makao makuu kuajiri watu wao wanaowataka wao, na kwa kufanya hivyo wanakuwa wanakiuka katiba yetu ya JMT pamoja na kufanya upendeleo wa wazi kwa baadhi ya kundi fulani la watanzania kwa kuwabagua wengine.
Na kwakuwa kama taifa tunakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa ajira kwa vijana, nilidhani Tanroads kama taasisi ya umma inawajibika kuisaidia serikali katika kupunguza ukosefu wa ajira kwa vijana badala ya kuweka vigezo ambavyo vinadhihirisha wazi kwamba wanataka kuendelea kufanya "recycling" ama kujuana.
Naomba kuwasilisha na karibuni kwa mawazo yenu na mitazamo yenu katika hili.
Copy kwa Asprin, Invisible, Ngongo, chama, Ritz, zomba, AshaDii, Dark City, Preta, WiseLady, Molemo, Nguruvi3, Mkandara, Mag3, Ben Saanane, fmpiganaji, Filipo, Crashwise, Mzee wa Rula, LiverpoolFC, Mungi, jogi, Rutashubanyuma, Nicholas, Daudi mchambuzi, Mtambuzi, Mchambuzi, nngu007, n00b na wengine.