Ajira za TANESCO mchakato umesitishwa

Kaparare

Member
Apr 19, 2021
93
230
Mwezi october mwaka huu wa 2021 zilitangazwa nafasi kadhaa za ajira shirika la umeme Tanzania-TANESCO. Juzi hapa waliita watu kadhaa kwa baadhi ya kada.

Sasa basi nikamuuliza jamaa yangu ambae kwa nafasi yake pale Tanesco sina shaka nae kabisa. Jmaa akaniambia mchakato umesitishwa kwa baadhi ya kada hasa madereva ambapo kulikuwa na nafasi 93. Sio hao tu pia kuna baadhi ya kada hawatosikia kuitwa kwenye usaili labda mpaka itokee mabadiliko/vinginevyo.

Sababu kuu ni sintofahamu ya hali ya mambo inayoendelea kwenye Shirika hilo. Kwahiyo wale mliokuwa mnasubiri mkeka wa utumishi fanyeni maombi sana mambo yakae sawa au karibu nyasa tuvue dagaa
 
ww acha kudanganya watu kibari cha ajira kinatolewa na Rais Tanesco wao wakiomba kibari basi hawausiki na kuita watu hiyo ni kazi ya Sekretarieti
 
Hamna kitu kama hicho we muongo, tanesco walitangaza nafasi awamu mbili, hao walioita saivi ilikuwa awamu ya kwanza ya pili itafuata baada ya usahili huu kuisha, usipotoshe watu
 
Hamna kitu kama hicho we muongo, tanesco walitangaza nafasi awamu mbili, hao walioita saivi ilikuwa awamu ya kwanza ya pili itafuata baada ya usahili huu kuisha, usipotoshe watu
Asante kwa kutupa moyo .
 
Shida ya hizi ajira hasa tanesco, afya na zile sekta muhimu huwa zinavamiwa na mamluki....ajira zinatangazwa 49 mfano kwa nafasi ya artisan lakini wanaoomba ni watu 400..ukija kuchunguza vizuri wenye sifa zinazohitajika hawafiki hata 100, kwa hiyo mchakato unavurugwa kwa style hiyo...
 
sasa naelewa kwanini sijasikia chochote hadi leo. loh niangalie mengine sasa.
Asante kwa Kuelewa. Mimi ni mbobezi wa Ajira za Serikalini. Najua michezo yote inayochezwa.
NB. Tuko kwenye awamu ambayo ajira zitatoka nyingi Sana both Government and Private lakini kupata nafasi utasota mpaka basi.
Tusubiri TRA Lakin................
 
Jmn ajira za tanesco cna mshiko mzuri jamn nilifanya hili shirika Kam STE na baadae tempo kabal maguful ajafuruga utaratibu wakt nasubiria namba kutk a makao makuuu duh
 
Back
Top Bottom