Ajira za madalali wa nyumba, vyumba na flemu za biashara Dar es Salaam

Manala An Academician

Senior Member
Oct 10, 2016
118
54
P2 Real Estate inajishughulisha na ununuaji na uuzaji wa viwanja, mashamba, nyumba katika mikoa ya Tanzania Bara, aidha, kampuni pia unajisikia na upangishaji wa nyumba, vyumba pamoja na flemu za biashara kwa- Dar Es Salaam ili kuwarahisishia usumbufu wateja wetu.

Ili kufikia malengo yaliyowekwa, kampuni inatangaza nafasi kumi (10) za kazi, kwa- madalali wenye sifa za kutafuta pamoja na kusimamia mchakato wa kumpangisha mteja kwa- uaminifu na bila mlolongo mrefu, ndani ya mkoa wa Dar es Salaam.

Sifa
1. Utayari wa kufanyakazi mda wote kutegemea na uhitaji wa mteja
2. Uaminifu, unadhifu na lugha nzuri kwa- mteja
3. Uzoefu katika kazi ya udalali ni sifa itakayopewa kipaumbele
4. Mahusiano mazuri na wenye nyumba, flemu n.k

Mshahara
Kwakuanzia mshahara utakuwa ni laki 3 kwa- mwezi. Nauli na gharama zingine za kila siku mfano kumpeleka mteja site n.k vitatolewa pia kwa- kila wiki

Kituo cha kazi
Ofisi iko Mabibo mkabala na lango la kuingilia Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji

Kama unahisi unazosifa, tuma maombi kwa- whatsapp namba 0765374146 au piga simu 0757930779
Mwisho wa kupokea maombi ni ijumaa tarehe 18/06/2021 saa 10:00 jioni
 
Back
Top Bottom