Ajira za maafisa mipango wa wilaya katika mikoa mipya zitatangazwa lini?

Mwanakanenge

Member
Nov 25, 2012
75
16
Wana jamvi mimi ni mhitimu wa shahada ya kwanza ya Development Finance and Investment Planning katika Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini kilichopo mkoani Dodoma nilimaliza chuo mwaka 2011.Kutokana na kozi niliyoisoma naweza kufanya kazi zifuatazo:-
1.Kuwa mhasibu
2.Kuwa afisa mikopo
3.Kuwa afisa mipango fedha
4.Kuwa mtafiti
5.Kuwa afisa uwekezaji
Wana jamvi yoyote anayejua ajira za mikoa na wilaya mpya kwa kada nilizozitaja hapo anijulishe.
 
Maofisa mipango huwa ni watu wenye shahada za uchumi mkuu..wewe na hyo shahada yako cjui unafit wapi kwa kwel.
 
Maofisa mipango huwa ni watu wenye shahada za uchumi mkuu..wewe na hyo shahada yako cjui unafit wapi kwa kwel.
Kiongozi hapo kwenye Red umemeza makosa unamlisha mkuu kasa,....hata mtu aliyefanya shahada ya uhandisi,takwimu anaweza kuwa afisa mipango seuze mkuu hapo yupo full na Development Finance and Investment Planning bana tena kutoka kule kule wanakopikwa maafisa mipango.....lol!....usimtishe mwenzio akarudi Dodoma kumuuliza Doctoro wake umuhimu wa shahada yake bana.

 
kwa nini unaitaka hiyo mikoa mipya au ndo unataka ukafanye ufisadi?
 
Shahada ya Usimamizi wa Fedha,Mipango na Uwekezaji.Hii ni kozi mpya toka Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini.Nafikiri kunatofauti kubwa kati ya wachumi na watu mipango ingawa katika halmashauri nyingi watu wengi waliopo katika ofisi za mipango sio waliosomea mipango wapo walioseomea uchumi na maendeleo ya jamii.
 
Naitaka hiyo mikoa mipya ndiyo yenye nafasi za ajira kwasababu mikoa na halmashauri za zamani uliuliza unaambiwa nafasi zimejaa na kwa sababu hiyo tu na sio kwa ajili ya kufanya ufisadi@chenge
 
Au kama kuna mkoa au halmashauri unajua kuna nafasi katika idara ya mipango nijulishe sio lazima iwe mpya@chenge
 
Au kama kuna mkoa au halmashauri unajua kuna nafasi katika idara ya mipango nijulishe sio lazima iwe mpya@chenge
mwakanenege pamoja na kusoma na kupata shahada bado uelewa wako ni mdogo sana hasa katika mifumo ya ajira za serikalini.Hujui kuwa kuna taasisi inaitwa TUME YA AJIRA"www.ajira.go".Hicho ndicho chombo kinachoratibu ajira zote mpya za taasisi za umma isipokuwa majeshi pekee yake.Pia degee za kuunga unga hizi nazo ni mizigo kwa mtaalamu mzuri anajua kuwa taasisi zetu zinakurupuka kuanzisha kozi mpya bila hata tathimini za kina na kufikiri kuwa kuuunga kozi kunasaidia kuongeza credibility kwenye employment wakati ni zero kabisa hivyo mtu anakuwa ni half way learned.
Kwa ufupi ni kwamba
1.Finance ni kozi yenye kujitosheleza na kusoma miaka mitatu bila kumaliza
2.Investment in field pia ya kushinda kubeba magunia ya misumari
3.Economic planning nayo isiombe. Tujiulize wewe kwa miaka mitatu unajua nini na nini kwa field zote tatu.?.Chagueni kozi nzuri zinazojitosheleza .Hivi kozi kama hii siamin kama unaweza kupata exemption ya mtihani ya NBAA. aluta catabuu
 
Last edited by a moderator:
mwakanenege pamoja na kusoma na kupata shahada bado uelewa wako ni mdogo sana hasa katika mifumo ya ajira za serikalini.hujui kuwa kuna taasisi inaitwa tume ya ajira"www.ajira.go".hicho ndicho chombo kinachoratibu ajira zote mpya za taasisi za umma isipokuwa majeshi pekee yake.pia degee za kuunga unga hizi nazo ni mizigo kwa mtaalamu mzuri anajua kuwa taasisi zetu zinakurupuka kuanzisha kozi mpya bila hata tathimini za kina na kufikiri kuwa kuuunga kozi kunasaidia kuongeza credibility kwenye employment wakati ni zero kabisa hivyo mtu anakuwa ni half way learned.
Kwa ufupi ni kwamba
1.finance ni kozi yenye kujitosheleza na kusoma miaka mitatu bila kumaliza
2.investment in field pia ya kushinda kubeba magunia ya misumari
3.economic planning nayo isiombe. Tujiulize wewe kwa miaka mitatu unajua nini na nini kwa field zote tatu.?.chagueni kozi nzuri zinazojitosheleza .hivi kozi kama hii siamin kama unaweza kupata exemption ya mtihani ya nbaa. Aluta catabuu


salute mkuuu hukumung'unya maneno
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom