AJIRA: Wenyekipato kizuri nendeni Makanisani na Miskitini.

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,171
2,000
Naibu waziri wa Kazi na Ajira mh Milton Makongoro Mahanga' amesema leo katika kipindi cha TUONGEE, kuwa watu wenyekipato ndiyo wanafanya tatizo la watoto wa mitaani kuwa sugu, kwa kuwapa vijisenti ombaomba mitaani, na kuwavutia wale walioko mikoani kuja mijini kuongeza idadi ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi. Amesema ni bora watu wanaojiona wana pesa za kuwapa ombaomba WAENDE MAKANISANI NA MISKITINI wakatoe sadaka na zaka, kwani taasisi za dini zina utaratibu mzuri wa kuwasaidia wenyeshida ili kupunguza tatizo kuwa kubwa katika jamii yetu. Amesema wazazi wenye watoto ombaomba wanabweteka wakisubiri watoto wao walete walivyopata kwa njia ya kuomba. Na akazidi kukemea wale weendesha magari kwamba waache kuwapa hizo shilingi mia, kwa tabia hii inafanya serikali ishindwe kuhimili wingi wao, kwavile wanatoka makwao wanajua kuwa wakifika mjini watapa fedha. Pia aliulizwa kwa nini nchi ya Kenya wameweza kufanikisha tatizo la kuondoa watoto wa mitaa? Akajibu kama watanzania wataacha kutoa hizi shilingi mia zao, basi tatizo linaweza kupungua au kuisha kabisa. Amesama kuwa watu wasio kuwa na elimu ndiyo wanao zaa sana, na kushindwa kuwatunza watoto. Amesema serikali ya tanzania haijafikia hatua ya kuwapangia idadi ya watoto wa kuzaliwa katika familia' kama nchi kama China inavyofanya. KWAHIYO WANA JF PUNGUZENI IDADI YA KUZAA WATOTO, MWISHO WAWILI TU.
 

Nyenyere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
13,497
2,000
Kuna ukweli fulani katika hili la kugawa hela ovyo. Hata hivyo serikali nayo iboreshe mazingira ya vijijini ili kuepuka kukimbilia mijini.
 

enfuka nkulu

Member
Dec 4, 2012
48
0
viongozi wetu kumbe hawana elimu!!!!!!!!!!!!! mbona wana watoto kibao, mbali na hilo kujaa watoto mitaani ni sababu ya serikali kukosa mipango mizuri juu ya watoto, jamii kutowajibika kama koo za zamani, kuvunjika kwa ndoa na wazazi kukimbia majukumu yao. inabidi waziri aeleze ana mkakati gani wa kusaidia kupunguza tatizo hilo badala ya kulalamika tu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom