AJIRA: Startimes na kuwanyanyasa watanzania ndani ya nchi yao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

AJIRA: Startimes na kuwanyanyasa watanzania ndani ya nchi yao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by local, Jun 19, 2012.

 1. l

  local Member

  #1
  Jun 19, 2012
  Joined: Jun 19, 2012
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha kuwa na wawekezaji wa aina hii, Mtanzania mwenye degree analipwa 250,000/= hii ni aibu. mtu hana jinsi, inabidi afanye kwa sababu hana ajira. Jamani hebu serikali ifumbue macho, wanakusanya pesa nyingi sana. Kwanza hata kodi hawalipi! Jamani wana JF hebu tuangalie jinsi ya kuwasaidia hawa wenzetu wanaofanya kazi Startimes.
   
 2. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Tusiwe wajinga sana, hawa watu na digrii zao wanafanyishwa kazi kwa nguvu? au wanasaini mikataba kwa hiari yao wenyewe??? kama digriii alipata kimagumashi mwache afanye kazi hizo maana haiingii kichwani una digrii ya kiukweli ukubali kulipwa hiyo posho.

  Sioni kama tatizo ni startimes bali ni mtanzania mwenyewe na fikira mbovu (tunapenda kunyonywa sasa unamshangaa mnyonyaji???). serikali itaingilia mikataba ya watu wazima mpaka lini??? tena wamesaini kwa hiari!!!! kama ni umasikini unaanza ule wa akili harafu ndo wa fedha. Kama Startimes wanakiuka makubaliano kweli tuombe serikali iwafundishe adabu.

  Mimi ningefikiri mtoa mada angeongelea suala la startimes kuondoa UBC kwenye orodha wakati wa Euro2012 football ile hali baadhi ya wateja walilipia startimes kwa ajili ya UBC tu, je kuondoa bila taarifa ya mwezi mzima kwa wateja ni haki, au wamevunja mkataba na wateja? Hivyo watu wote warejeshewe fedha zao kwa kupewa mwezi mmoja bure kama wanataka au wapewe cash zao wasepe. au startime wapigwe fine ya mil. 150 fedha hiyo iende serikalini kutatua matatizo mengine ya jamii, maana walichofanya ni wizi.

  Nawasilisha.
   
 3. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Hatujadili majungu JF. weka payslip na degree certificate hapa tuthibitishe!
   
 4. ZALEOLEO

  ZALEOLEO Senior Member

  #4
  Jun 19, 2012
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ukute wewe ni mmoja wao wa wanaolipwa 250,000 afu unajifanya unaombea wenzio msaada! Anyway inawezekana kazi hyo ilikua inataka mtanzania yeyote wa kuifanya sema tu kwa sababu degree zimekua nyng mtaani ndo kama hivo kazi za drs la 7 wanafanya form six,kazi za form 4 mnafanya wenye degree! Ushauri wangu acha kulia lia pambana na maisha nje ya star times
   
 5. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #5
  Jun 19, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Startimes niwa kupigwa ban tu! Wanatunyanyasa ndani ya nchi yetu, haiwezekani waondoe ubc wakati wengine tumelipia tukijua ubc itakuwepo kwenye list ya channel zangu. Huu ni ujinga sana.
   
 6. M

  MaxMase JF-Expert Member

  #6
  Jun 19, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 500
  Likes Received: 249
  Trophy Points: 60
  Hawa jamaa inabidi wachukuliwe hatua cose euro ndo imafanya wengi tukanunua decoder na kulipia mwezi then wanakati channel bila ridhaa yetu wateja kwanini?
   
 7. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #7
  Jun 19, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapo kwenye red ndio pa kufanyia kazi.. Yaani walichofanya Star times ni utapeli wa hali ya juu na japo inaonyesha viongozi wetu hawajali inabidi sie wenyewe tuifanye kazi ya kulalamika kwa TCRA.. Hata wasipochukua hatua lakini wataona kwamba wametukwaza sana.. naomba wewe na wengine wote watakaopita hapa waingie hapa kujaza malalamiko dhidi ya Star times.. TCRA|Tanzania Communications Regulatory Authority
   
 8. j

  joe peters Member

  #8
  Jun 19, 2012
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 85
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 13
  Where is Hon. January now?..... Tanzanians need you to take bold steps
   
Loading...