Ajira sio ngumu ila watu wanafanya ajira ziwe ngumu

chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
7,581
15,713
Sikatai kuna tatizo la ajira lakini ukirudi nyuma tatizo la ajira linakuja kwa upande fulani watu kufanya ajira kukosekana kwa mambo haya.

Mchango mkubwa ajira hupo kwenye sekta binafsi na watu binafsi.

Hizi sehemu sio kwamba zinashindwa kupanua wigo mkubwa ajira bali ni kutokana na changamoto za watu kwenye ajira wanavyo ziwekea ugumu.

Nazungumzia hili ni moja ya wahaanga niliyependa kufungua ofisi zaidi ya mbili na kuajiri vijana wapige kazi na wapende ofisi kama yao,ila kilichotokea ni kuharibu ofisi mpaka kupelekea kufunga.

Sasa leo utaniambia nifungue ili niajili tena, hapo uwezi kufungua ni bora kubaki na ofisi moja.

Ugumu wa ajira unasababisha wengine wasiongeze wigo wabishara kuajiri kutokana na msingi mbovu wa watu wanaopelekea ajira kupungua.

Ajira kuwa ngumu kuna tokana na haya:

*Tamaa ya kufanikiwa haraka kwenye ajira uliyopata.
*Kutothamini ajira uliyopata
*Kutokuwa na uvumilivu
*Kufanya biashara yako ndani ya biashara uliyoajiriwa.
*Wizi na udokozi
*Kutokuwa na ushirikiano

Haya mambo nayo yataja ndiyo ya mesababiaha watu wengi kukosa ajira na wengine kuwa wahaanga wa ukosefu wa ajira.
 
Changamoto lazima mkuu ushajiuliza kivipi utaweza kutatua hizo changamoto zako

Kuna jirani yangu alifungua ofisi ya uhuduma za pesa na mtaji ulikuwa milioni 9.

Mwajiliwa wa kwanza alikuwa wa kike kumbe pesa alikuwa anatoa kidogo na kuonga mabwana haka fukuza.

Mwajiliwa wa pili alikuwa wakike naye huyu baada ya kuzungushia ofisi anazungushia biashara zake na ilipokuja kugundulika kalibia milioni 8 hipo nje yani ofisi ina milioni 1 tu.tukapeleka polisi na ndipo zikarudishwa.

Mwajiliwa wa tatu hapa ndo nimechoka baada ya pesa kufanya kazi ofisini anakopesha ili kupata riba, sasa kakopesha watu milioni 7 ya, ofisi wakakimbia na kusingiziwa kuwa kavamiwa na watu wasio julikana na kuporwa pesa zote.

bahati nzuri vituo vya polisi ndio nyumbani kwetu tukampeleka gereji kilichotokea na kufunguka!

we acha tu
 
kuna jirani yangu alifungua ofisi ya uhuduma za pesa na mtaji ulikuwa milioni 9.
mwajiliwa wa kwanza alikuwa wa kike kumbe pesa alikuwa anatoa kidogo na kuonga mabwana haka fukuza.

mwajiliwa wa pili alikuwa wakike naye huyu baada ya kuzungushia ofisi anazungushia biashara zake na ilipokuja kugundulika kalibia milioni 8 hipo nje yani ofisi ina milioni 1 tu.tukapeleka polisi na ndipo zikarudishwa.

mwajiliwa wa tatu hapa ndo nimechoka baada ya pesa kufanya kazi ofisini anakopesha ili kupata riba ,sasa kakopesha watu milioni 7 ya ofisi wakakimbia na kusingiziwa kuwa kavamiwa na watu wasio julikana na kuporwa pesa zote.
bahati nzuri vituo vya polisi ndio nyumbani kwetu tukampeleka gereji kilichotokea na kufunguka !

we acha tu
Aisee!
 
Hata maboss wakitanzania wanapenda kujichukulia wakamilifu "boss hakosei" Kwa sababu Tu katoa ajira, sikatai kuwa waajiriwa wanasumbua lakini hata maboss wakipata mtu muaminifu na loyal ndio wanamlalia, si ajabu hata mshahara asimuongezee hadi akitishia kuacha kazi au akishaondoka ndio wanaanza kumdorishia maslahi mazuri ili arudi

Yaani wapo radhi wamlipe mkenya au mzungu pesa ndefu ila sio kumpa mtanzania mwenzake maslahi mazuri. Wakipigwa ndio wanaanza kulaani na kulalamika as if wao ni wakamilifu
 
sikatai kuna tatizo la ajira lakini ukirudi nyuma tatizo la ajira linakuja kwa upande fulani watu kufanya ajira kukosekana kwa mambo haya.

Mchango mkubwa ajira hupo kwenye sekta binafsi na watu binafsi.

hizi sehemu sio kwamba zinashindwa kupanua wigo mkubwa ajira bali ni kutokana na changamoto za watu kwenye ajira wanavo ziwekea ugumu.

Nazungumzia hili ni moja ya wahaanga niliyependa kufungua ofisi zaidi ya mbili na kuajiri vijana wapige kazi na wapende ofisi kama yao,ila kilichotokea ni kuharibu ofisi mpaka kupelekea kufunga.

sasa leo utaniambia nifungue ili niajili tena.hapo uwezi kufungua ni bora kubaki na ofisi moja .

ugumu wa ajira unasababisha wengine wasiongeze wigo wabishara kuajiri kutokana na msingi mbovu wa watu wanaopelekea ajira kupungua.

ajira kuwa ngumu kuna tokana na haya:
*Tamaa ya kufanikiwa haraka kwenye ajira uliyopata.
*Kutothamini ajira uliyopata
*kutokuwa na uvumilivu
*kufanya biashara yako ndani ya biashara uliyoajiliwa.
*wizi na udokozi
*kutokuwa na ushirikiano

haya mambo nayo yataja ndiyo ya mesababiaha watu wengi kukosa ajira na wengine kuwa wahaanga wa ukosefu wa ajira.
WIZI ndo point niliyoiona
 
Point ya msingi ni maslahi tu!

Hilo eneo likiboreshwa kuendana na uchumi wa sasa hamna mtu atazembea kazini wala kufanya mambo ya ajabu!

Wewe commission unapata lets say million na laki 6 kwa mitandao yote na banks. Ila mshahara wa mfanyakazi unataka umlipe laki 1 kwa mwezi.

Hujifikirii huyo mtu anatakiwa ale akalipe na kodi hilo hulioni. Unachotaka wewe upate 1.5M yako kama ilivyo. Maisha ya mjini yalivyo kila kitu ni pesa kwanini usipigwe sasa😂
 
Vijana wengi wakitanzania hawajitambui.

Mwaka 2018 nilimunua Boxer 2 na Haujue 2(sijui kama nimepatia herufi)
Nikatafuta Vijana.
Niliowapa Boxer nikawaambia wanipe elfu 8 Kwa siku. Hivyo kila wiki wanipe Tsh 56,000/= kila mmoja wao.

Na niliowapa Haujue nikawaambia Wanipe elfu 6 Kwa siku hivyo Kwa wiki watanipa Tsh 42,000/= kila mmoja wao.

Mwezi wa Kwanza wote wakafanya vizuri.
Lakini mambo yakaanza kubadilika mwezi wa pili.

Watanzania wengi ni watu wa kutoa udhuru na kujitetea mno. Sasa Sisi tunaojali watu tunajikuta tunachukulia matatizo Yao kama yetu kumbe wao wanatuumiza.

Nikaanza kugombana nao, nikabadilisha wawili huku hawa wengine wakinililia mno. Ukicheki ni watu wazima kunishinda na wanafamilia lakini ni wapuuzi tuu. Hawathamini kazi.
Wakija kuomba kazi sasa wanavyojiliza si utasema watu ndio hawa, kumbe unafiki mtupu!
Kwa kweli walinifundisha roho ngumu na Mbaya.

Vijana wawili wakatoa Side Mirror, kuwaulizia wakasema ati zinawasumbua wakiendesha PIKIPIKI. Nikawakemea kuwa wasitoe maamuzi yoyote kwenye vyombo vyangu, wanunue vyao ili wafanye watakavyo.

Wakavirudisha,

Mmoja akakamatwa na polisi Kwa kusafirisha magendo nyakati za usiku, alivyokamatwa akajitahidi akachoropoka, PIKIPIKI ikapelekwa kituoni GOBA.

Ananipigia simu asubuhi nimeenda kazini kunitaarifu PIKIPIKI imeshikwa polisi. Nikamuambia twende akakataa. Nikasema Sawa.

Nikaenda kituoni pale. Nikajitambulisha, wakasema Pilipiki yangu ilitumika kubebea magendo hivyo wanaamini nami ninahusika na magendo.
Nikawaambia Mimi sihusiki Ila nimeajiri kijana anayehusika na PIKIPIKI hiyo, hivyo nitashirikiana nao kumkamata kwani vielelezo vyake alivyoombea kazi ninavyo.

Tukamkamata, naonyeshwa PIKIPIKI haina side mirror, fundi wangu anaikagua akasema imebadilishwa Betri.

Nikaongea na Mkuu wa kituo wamfunze adabu kijana, wakamfunza mpaka akasema alipoiuzia hiyo Betri.

Baada ya sakata lote Kuisha, polisi wakaniambia hiyo kazi YA bodaboda ni Kheri ufanye mwenyewe kwani hawa vijana wengi wao hawajielewi, na utakuwa unapata tuu hasara Kwa kuwalisha wao na familia zao.

Pili akaniambia, Kama nitawapa bodaboda basi iwe ya Mkataba, na nisiwe na huruma hata chembe.

Nikaondoka na PIKIPIKI, nikaweka za mkataba, lakini bado kukawa na shida nami kumfanyia mtu ushenzi Kwa kumzingua kisa kaenda kidogo kinyume na mkataba nikaona ni Shida.
Nikaziuza baada ya kuteseka na tabia za vijana wa kitanzania.

Sitaki kuelezea ishu za Shamba, na masuala ya migahawa.

Watanzania wengi bila ya kupelekeshwa na kufanyiwa unyambisi na ubabe hawawezi kukufanyia kazi

Ni Kama NG'OMBE hivi.

Ingawaje sio wote. Wapo wachache mno waaminifu.
 
Point ya msingi ni maslahi tu!

Hilo eneo likiboreshwa kuendana na uchumi wa sasa hamna mtu atazembea kazini wala kufanya mambo ya ajabu!

Wewe commission unapata lets say million na laki 6 kwa mitandao yote na banks. Ila mshahara wa mfanyakazi unataka umlipe laki 1 kwa mwezi. Hujifikirii huyo mtu anatakiwa ale akalipe na kodi hilo hulioni. Unachotaka wewe upate 1.5M yako kama ilivyo. Maisha ya mjini yalivyo kila kitu ni pesa kwanini usipigwe sasa😂

Hakuna cha Maslahi wala nini. Watanzania wengi ni michosho.

Nenda Kwa wanaolipwa mishahara minono kwenye MAKAMPUNI makubwa ndio utajua Watanzania mi wavivu, wapenda Umbeya na Stori kazi hawataki kufanya.

Mpaka boss apitepite. Bila usimamizi mkali Watanzania wengi hawawezi kufanya lolote likafanikiwa
 
kuna jirani yangu alifungua ofisi ya uhuduma za pesa na mtaji ulikuwa milioni 9.
mwajiliwa wa kwanza alikuwa wa kike kumbe pesa alikuwa anatoa kidogo na kuonga mabwana haka fukuza.

mwajiliwa wa pili alikuwa wakike naye huyu baada ya kuzungushia ofisi anazungushia biashara zake na ilipokuja kugundulika kalibia milioni 8 hipo nje yani ofisi ina milioni 1 tu.tukapeleka polisi na ndipo zikarudishwa.

mwajiliwa wa tatu hapa ndo nimechoka baada ya pesa kufanya kazi ofisini anakopesha ili kupata riba ,sasa kakopesha watu milioni 7 ya ofisi wakakimbia na kusingiziwa kuwa kavamiwa na watu wasio julikana na kuporwa pesa zote.
bahati nzuri vituo vya polisi ndio nyumbani kwetu tukampeleka gereji kilichotokea na kufunguka !

we acha tu
Mkuu kama haya mambo yamekutokea basi fahamu wewe ndio unatatizo.

Unatumia vigezo gani kuwapata hao wafanyakazi?

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
 
Hakuna cha Maslahi wala nini. Watanzania wengi ni michosho.

Nenda Kwa wanaolipwa mishahara minono kwenye MAKAMPUNI makubwa ndio utajua Watanzania mi wavivu, wapenda Umbeya na Stori kazi hawataki kufanya.

Mpaka boss apitepite. Bila usimamizi mkali Watanzania wengi hawawezi kufanya lolote likafanikiwa
Hahahahah sio wote mkuu😅 ukijumuisha watu wote unafeli
 
Hahahahah sio wote mkuu😅 ukijumuisha watu wote unafeli

Watu wakishazidi Average tunaitaga wote tuu.
Hata Kama kuna wachache waaminifu Ila watamezwa na HAO wahuni na washenzi.

Ndio maana nikaandikaga usisaidie Masikini
Soma hapo chini

Sio kwamba niliandika tuu. Ni baada ya kufanya uchunguzi Kwa muda mrefu Sana.
Kuwasaidia na kuwajali lakini ni Kama vile wapuuzi hivi.

Kwa kweli wamenifundisha roho ngumu na mbaya
 
Haya mambo yana pande mbili zote n ttzo boss wa kiswahili ni shida sana unakuwa royal sna biashara ikisimama anaanza dharau na kuamini huna pakwenda.nilifanyakaz sehemu nikawa mwema sna wenzangu wakichukua nawazuia,biashara nikaona kama yng at the end nikajakuambiwa mm ndio mwizi.

Nilichojifunza usimuoneee huruma boss mswahili ukipata chance nyoosha kabsa but in a advanced way maana maboss wengi hawajasoma.
 
Vijana wa kibongo mpite hapa:
JamiiForums2139938287.jpg
 
Sikatai kuna tatizo la ajira lakini ukirudi nyuma tatizo la ajira linakuja kwa upande fulani watu kufanya ajira kukosekana kwa mambo haya.

Mchango mkubwa ajira hupo kwenye sekta binafsi na watu binafsi.

Hizi sehemu sio kwamba zinashindwa kupanua wigo mkubwa ajira bali ni kutokana na changamoto za watu kwenye ajira wanavyo ziwekea ugumu.

Nazungumzia hili ni moja ya wahaanga niliyependa kufungua ofisi zaidi ya mbili na kuajiri vijana wapige kazi na wapende ofisi kama yao,ila kilichotokea ni kuharibu ofisi mpaka kupelekea kufunga.

Sasa leo utaniambia nifungue ili niajili tena.hapo uwezi kufungua ni bora kubaki na ofisi moja .

Ugumu wa ajira unasababisha wengine wasiongeze wigo wabishara kuajiri kutokana na msingi mbovu wa watu wanaopelekea ajira kupungua.

Ajira kuwa ngumu kuna tokana na haya:

*Tamaa ya kufanikiwa haraka kwenye ajira uliyopata.
*Kutothamini ajira uliyopata
*kutokuwa na uvumilivu
*kufanya biashara yako ndani ya biashara uliyoajiliwa.
*wizi na udokozi
*kutokuwa na ushirikiano

Haya mambo nayo yataja ndiyo ya mesababiaha watu wengi kukosa ajira na wengine kuwa wahaanga wa ukosefu wa ajira.
Chizcom analysis yako inazungumzia changamoto za walioingia tayari katika ajira na si walio nje ya ajira wanaohitaji kuipata hiyo ajira. Ni ufikiri finyu kama walivyo wanasiasa wengi kudhani bodaboda ndo mifano ya ajira zilizopo au hivi viduka uchwara vya wakala wa pesa kwa vijana waliomaliza darasa la saba au waliofeli kidato cha nne. Ungeenda mbali kuleta uchambuzi wa vijana waliomaliza vyuo wenye taaluma zao iwe ni ktk kikimo, afya, elimu nk ndo uoanishe na mazingira rafiki ya kuwawezesha kitumia taaluma zao. Hao bodaboda vijana ulikiangalia hata leseni wengi hawana. Hivi mfano unampa mtu sehemu ya uwakala wa pesa na uko makini kitaaluma mtaji wa milioni8 akuibie hadi ibaki moja wewe na yeye nani ana uwezi mkubwa kumshinda mwenzie?
Taifa linalojipambanua kutengeneza ajira za bodaboda na viduka vya uwakala wa fedha nikimaanisha mpesa, tigo pesa nk huku mzunguko wa pesa ukiwa mdogo ni kutengeneza bomu la vibaka na wauza miili maana unachomlipa hakiendani na mahitaji ya sasa.
Hebu leta uchambuzi kwa wahusika waliotumia muda wao miaka isiyopungua 19 wakiwa shuleni ndo ujikite katika hoja yako kuwa ajira sio ngumu. Mind you nazungumzia mazingira aidha ya kuajiriwa au kujiajiri mwenyewe. Hiyo miaka 19 ni wastani tu elimu ya msingi 7, sekomdari 6 na chuo miaka 3.
 
Back
Top Bottom