Ajira serikalini zipo nyingi sana

Mssassou

JF-Expert Member
Jun 17, 2015
1,537
597
Jamani serikalini kuna nafasi nyingi sana za kazi,kama serikali itaendelea kufuatilia watumishi wanaotumia vyeti feki au vyeti vya watu wengine katika wizara mbalimbali na kisha kuwafukuza kazi basi ajira nyingi zitapatikana.Hakika asilimia zaidi ya 50 ya waajiliwa wanatumia vyeti feki au vya watu wengine.Matokeo yake watu wenye sifa wanakosa kazi na kurandaranda mitaani.Wanaotumia vyeti feki au vya watu wengine wanashindwa kutoa huduma ipasavyo.Kwa uchunguzi wangu wa harakaharaka watumishi wengi hasa walimu ndio wanaongoza kutumia vyeti feki au vya watu wengine.Serikali ichunguze na iwafukuze kazi na kuwashitaki watumishi wa namna hiyo
 
Mbona hilo likifuatiliwa kwa ukamilifu na kwa uadilifu wa hali ya juu si ajabu hata nafasi ya urais ikabaki wazi mtu mwenye sifa za kushika nafasi hiyo akajipatia ajira.
 
Back
Top Bottom