Ajira Serikali: Kwa tafsiri ya Serikali, ajira ni za walimu na watu wa afya pekee au?

Kila mtu hulia na mama yake, hongereni mliosomea Education na health hatuna husda.
 
Pumbavu aliyekuzaa.Unadhani saizi tukisema Kati ya walimu na watu wa afya against fani zingine wapi wanakabiliwa na tatizo la mass unemployment?

Eti maslahi madogo kwani unadhani fani zingine zina maslahi makubwa?

Ndio maana nikimsikia mtu anatetea waalimu namuonaga ni mpumbavu kama wewe,uache kutetea wakulima wako hoi na wasio na ajira huko utetee waalimu? Kama maslahi madogo mbona hawaachi Kazi ndio wanazidi kukimbilia?

Jibu ni moja tuu kitaani hakulipi tena
Boss mbona una hasira sana. Una taaluma gani ?
 
Mfano, lini ajira portal walitangaza nafasi za kazi BOT tangu mwaka 2015? Huko BOT watumishi hawastaafu?hawafi? Hakuna vitengo vipya muda wote huo
Naongezea na NIMR , TMDA ........

Binafsi napendekeza na hao waingie kwenye mfumo wa ajira portal.... ili kuondoa manung'uniko kwenye ajira za hao jamaa.
 
Ajira ni kwa sekta mbalimbali, lakini elimu na afya ndiyo kipaumbele namba moja katika ajira kutokana na uhitaji wao kwa uwingi.
Habari zenu wadau.

Tangu nimeanza kusikia ishu ya kuwepo na tatizo la ajira nchi hii mara zote wanaozungumziwa kukosa ajira inaonekana ni watu wa sekta ya Elimu na afya.

Hii dhana miongoni mwa viongozi wa serikali inashangaza Sana, kwamba hata wanapotangaza kwamba wataajiri watu kadhaa basi huwa wanaajiri walimu na watu wa afya yaani manesi na madaktari.

Hili jambo la ubaguzi wa ajira nimeanza kuliona toka enzi za Mkapa na miaka yote hiyo hawa watu huwa hawana usaili wala nini.

Kwamba nyie watu wa serikali mnataka mtuambie kwamba vyuo vyote vikuu na vya Kati Tanzania hii vinatoa kozi za Ualimu na fani za afya tuu? Mbona kozi zingine ndio zina vijana wengi kuliko hizo kozi 2 mnazozipendelea?

Ifike mahala muelewe kwamba ajira ni pamoja na vijana waliosomea kozi tofauti na Ualimu na afya.Kila ajira zinazotangazwa huwa ni hao tuu kana kwamba fani zingine hawana shida ya ajira au mahitaji hayapo au wao wanapata Kazi kirahisi.

Binafsi nachukizwa sana na huu mtizamo wa serikali. Kama mnaona hizi fani zingine sio muhimu basi watu wote wasome Ualimu na mambo ya Afya na vyuo vifute hizo zingine msidahili vijana huko maana inaonekana serikali haijishughulishi na ajira zao.

Mtu atakwambia wajiajiri,kwamba usiposomea Ualimu na afya wewe unakuwa unaweza kujiajiri Ila hao mnaowaajiri kila tangazo wao ndio hawana uwezo wa kujiajiri? Hivi majuzi nilimsikia Waziri wa TAMISEMI bungeni akidai Halmashauri karibu zote hazina wahandisi zinatumia Technicians wachache waliopo na kwamba eti wataazima wahandisi kutoka JWTZ afu wawape kazi kwa mkataba. Nilishangaa Sana badala ya kuajiri unaazima huko, mbona basi msiwape Kazi kwa mkataba? Kwani mtaani hawako?

Kiukweli serikali inaniboa Sana na dhana finyu na ajira walionayo hao watu, si ajabu Prof Assad alikuwa sahihi kwa ile asilimia 60 ya wasio na uwezo.

Kama mnaona hamuwezi kuwaajiri basi wawekeeni mazingira rafiki ya wao kujiajiri au kuajiriwa na sekta binafsi. Kwa mfano Serikali huwa haikagui makampuni binafsi kuangalia kama haki stahiki za wafanyakazi zinafuatwa ikiwemo kima cha chini cha mshahara, mikataba ya ajira, mafao yao, kuwawezesha kwa mikopo, kuwapa tenda ndogo ndogo japo upendeleo kama inavyopendelea walimu na manesi nk.

Mathalani sekta ya ujenzi, zaidi ya 70% ya matumizi ya serikali huenda kwenye ujenzi sasa huko kuna wakandarasi na force account.Kwa wakandarasi kuna kipengele au takwa la kimkataba kwa Kampuni kuwa na mhandisi au Fundi Sanifu kwenye mradi lakini cha ajabu kampuni karibu zote zinawasilosha CV za kuiba ya hao watu lakini wakati wa utekelezaji wa Kazi hawapo bali wanatumia tuu yeyote awe fundi awe layman ili mradi wakwepe kulipa.

Mbaya zaidi wasimamizi wa mikataba hawafuati sheria kuhakikisha jambo hili linafuatwa maana hii ndio njia mojawapo ya kuwatengenezea ajira vijana kwenye fani ya ujenzi ambao serikali haiwaajiri. Hawa watu wangefuata sheria hao vijana wangepata ajira,wangepata mafao na Serikali ingepata kodi kwa njia ya PAYE. Sasa hivi Serikalini imekazana kusomesha vijana VETA sasa hao wakimaliza watajiajiri vipi wakati saizi kuna mafundi lundo mtaani na mambo hayaendi?

Kama Serikalini inashindwa kulinda maslahi ya watu wake basi iwaajiri yenyewe la sivyo basi vijana angalieni namna ya kuwa na jambo lenu, umachinga sio Kazi ndio maana mnadharaulika. Uhalifu na ISIS wakija kushamiri hapo baadae msije kusema hamjui chanzo.
 
Ajira ni kwa sekta mbalimbali, lakini elimu na afya ndiyo kipaumbele namba moja katika ajira kutokana na uhitaji wao kwa uwingi.
Nonesense , mfano uhandisi , Mahitaji bado hi makubwa nchi hii Ila utashangaa ajira ni miaka mingi sasa imepita tangu serikali iajiri
 
Nonesense , mfano uhandisi , Mahitaji bado hi makubwa nchi hii Ila utashangaa ajira ni miaka mingi sasa imepita tangu serikali iajiri

Basi endelea kulia na uhandisi wako, walimu wanahitajika kila kona hasa shule za vijijini, sasa niambie mhandisi anahitajika kila kijiji kufanya nini! The mhandisi here will seem surplus to the requirements in the pecking order! Upo hapo au bado umeupuna usingizi!
 
Kwa wale wa VETA ,Technician Mwenye FTC au Diploma analipwa bei gani? Kuna tangazo la ajira za walimu wa Veta sasa nimeulizwa na mtu nimeshindwa kujibu.
 
Theory of demand and supply ndio inatumika apo
Halimashauri mwanasheria ni moja


Hospital inafanya kazi masaa 24 ko staffing yake ni kubwa
20220428_000824.jpg
 
Back
Top Bottom