Ajira ni suala la mtu binafsi ama la Serikali?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
20,353
38,584
Kuna mjadala kuhusu ajira kuwa chini ya kiwango hapa Tanzania. Inasemekana ni watu wachache sana wapo kwenye ajira rasmi. Kuna watu wanaamini kwamba ni wajibu wa serikali kutengeneza na kutoa ajira kwa watanzania na wapo pia wanaoamini kwamba ajira ni wajibu wa mtu binafsi kuitafuta na kuipata.

Jee ajira ni suala la mtu binafsi kuitafuta na kuipata ama ni wajibu wa serikali kuhakikisha kwamba ipo na inapatikana. Wanasiasa wetu wao wanaonesha kwa matendo yao wapo upande gani, na upande waliopo wapo upande sahihi?
 
Taarifa yako kaifanyie utafiti tena urudi hapa. Utueleze ni kwa kiwango gani ajira ni tatizo kitakwimu. Sio unakuja na taarifa za jumlajumla tu kuwa 'inasemekana'

Huu sio ugreat thinker
 
Japo kumekuwepo malalamiko mengi juu ya kudumaa kwa ajira za serikalini kwa maana ya zile za utumishi wa umma.

Jukumu kuu la serikali ni kuweka mazingira safi ya kuajiri na kujiajiri mfano kupitia mazingira safi ya biashara, miundombinu sera nzuri za biashara za ndani na nje n.k
 
Back
Top Bottom