Ajira mpya zisipotoka serikalini mwezi huu hali itazidi kuwa ngumu mtaani

T-Bagwell

JF-Expert Member
Apr 6, 2017
1,190
2,323
Habari wana Jf

Zaidi ya wafanyakazi 10,000 hawatopokea mishahara mwezi huu.
Kwa mahesabu ya harakaharaka kuna wafanyakazi ambao walikiwa wanapokea 300000, 50000, 700000, na wengine zaidi ya 1.5M kwa mwezi lakini hawatopokea tena mwezi huu.

Tupige mahesabu madogo tukadirie labda kila mfanyakazi alikuwa anapokea 500,000 japokuwa ni hesabu ndogo kwasababu wengine wangepokea viinua migongo vyao ambayo ingekua zaidi ya 50M

500,000 X 10000 = 5,000,000,000 inamaana hiyo hela haitaingia kwenye mzunguko mwezi huu.

Kama tunavyojua tunategemea hela iingie kwenye mzunguko ndio mambo yaende sawa, sasa hiyo hela isipoingia mtaani hali itazidi kuwa ngumu sio kwa wafanyakazi hewa tuu, Bali hata wafanyabiashara na wafanyakazi wasio hewa pia watakuwa na hali ngumu.

NI MAWAZO YANGU TUU.
 
Nilitegemea penginine mleta mada ungesema tunaomba mishahara ya waliokamatwa na vyeti feki ambayo inakadiliwa kama trion tano...iingizwe kwenye sehem zenye mahitaji muhimu kama mashuleni na hosptal...kumbe unawaza mtaani huku watu wanakoshinda bar na kubeti mimechi ya ulaya?!!
 
Utapata akiri na ufahamu wa kutosha kama una lishe bora, na utahepukana na habari za hospitali kama una lishe iliyobora.
Sasa leo hata mfumuko wa bei za vyakula serikali imekosa hatua za kuchukua unategemea hizo sekta nyeti zako kipi kitafanyika.
 
Sio vyema kuitegemea serikali itoe ajira..Kijana badili fikra...Waza hata kujiajiri
Umeelewa maada!? Au ndio mkurupuko!?
Jamaa anazungumzia upungufu wa kwenye mzunguko....! Raisi alisema watuhumiwa wa vyeti feki wapewe mshahara wa mwezi mei. Na ujue kua katika pesa ilikuepo kwenye mzunguko hapo nyuma hawa watu (wenye vyeti vinavyodaiwa kua feki) walikua na mchango wao....(zingatia estimate ya mtoa maada). Hivyo kuondelewa kwa watu hao katika list ya mishahara kunapunguza pesa (changio lao) kwenye mzunguko as they can't spend what they don't have.
 
Mimi nasikia pana watu wanatafuta vyeti vya kununua,

Nakuja nipige mnada kuanzia cha nursery school to Bachelor degree ili Nipate mtaji wa kujiaajiri maana huku naona vinaweza vikakosa matumizi.

Kwa sababu, kama ajira hazitoki bora kujiaajiri, sasa mtaji bora niuze vyeti nitafute mtaji.
Sasa, nijiajiri.

Anayehitaji aje pm teeeh teeeh teeeh teeeh teeeh Haaa haaa Haaa haaa Haaa haaa Haaa
 
Umeelewa maada!? Au ndio mkurupuko!?
Jamaa anazungumzia upungufu wa kwenye mzunguko....! Raisi alisema watuhumiwa wa vyeti feki wapewe mshahara wa mwezi mei. Na ujue kua katika pesa ilikuepo kwenye mzunguko hapo nyuma hawa watu (wenye vyeti vinavyodaiwa kua feki) walikua na mchango wao....(zingatia estimate ya mtoa maada). Hivyo kuondelewa kwa watu hao katika list ya mishahara kunapunguza pesa (changio lao) kwenye mzunguko as they can't spend what they don't have.
Asee sawa mtaalamu wa uchumi...

BTW sio maada ni Mada
 
Mkuu cha msingi ni kutafuta mtaji...unaanza hata na mtaji mdogo mkuu...Usiogope kukopa hata mtaji ilimradi uwe na biashara yenye kuleta tija
Tatizo sio mtaji mkuu tatizo ni aina ya ajira gani nijiajiri ili nipate wateja maana saivi biashara za watu zinadoda kutokana na mzunguko wa pesa kuwa mdogo kiasi kwamba inapelekea watu kula mitaji
 
Tatizo sio mtaji mkuu tatizo ni aina ya ajira gani nijiajiri ili nipate wateja maana saivi biashara za watu zinadoda kutokana na mzunguko wa pesa kuwa mdogo kiasi kwamba inapelekea watu kula mitaji
UMIZA KICHWA MKUU..BIASHARA ZIPO NYINGI TU...ILA KAMA MZUNGUKO WA PESA NI MDOGO SIO MBAYA KUSUBIRI...TAFUTA KIBARUA MAHALI UINGIZE HATA 5000 KWA SIKU
 
Back
Top Bottom