Ajira mpya za walimu 10,000 zinakuja mwaka huu wa fedha 2021/22

SAKA25

Member
Jul 15, 2021
12
22
Ajira mpya zimepunguza uhaba wa Walimu wa Sayansi
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Ummy Mwalimu amesema kwa Sasa hakuna Shule ya Sekondari ambayo haina Mwalimu wa Sayansi.

Waziri Ummy amesema katika ajira 6,949 zilizotewa Mwezi Juni 2021, Walimu wa Fizikia walioajiriwa ni 1,360 na Walimu wa Hisabati Ni 599 ambao wamesambazwa katika shule ambazo hazikuwa na Walimu hao hapo awali.

"Ni imani yangu sasa hakuna shule yoyote ya Sekondari nchini ambayo haina mwalimu wa sayansi hata mmoja,"amesema.

Hata hivyo, ameiaagiza Mikoa kumleta taarifa iwapo kuna Shule ya Sekondari katika Halmashauri ambayo haina Mwalimu wa masomo ya Fizikia, Kemia, Baiolojia na Hisabati hata mmoja ili ufanyike msawazo wa walimu wa Sayansi.

Aidha, amesema katika mwaka huu wa fedha 2021/22 serikali inatarajia kuajiri walimu 10,000 na kipaumbele kitakuwa walimu wa Sayansi.

SOURCE:TAMISEMI FACEBOOK PAGE
 
Serikali ya AWAMU ya 6 ina nia njema ya kuajiri WALIMU cha ajabu baadhi ya watanzania wanapinga hizi TOZO za KODI za miamala ya fedha na mafuta sasa utashangaa sijui WANASIMAMIA LIPI LA MAANA ?😲🤣

MAENDELEO HAYAPATIKANI BILA YA KUIFUNGA MIKANDA
 
Mwalimu mmoja wa physics Shule nzima, wanafunzi shule nzima = 700+.
Ratio = 1:700
Serikali iajiri walimu, walimu wa masomo ya sayansi hawatoshi bado.
Yani wanajitekenya bure,waajiri walimu wa science na wa arts waongeze.

We shule Haijawahi kia na Mwalimu wa physics eti unampeleka mmoja Ili awadonolee donolee tu tena watoto wenyewe 700 na shule ya jirani si ajabu inataka imkodishe kupitia afisa elimu ana muamrisha tu mchezo imeisha.
Huyu Mwalimu lazima aombe uhamisho tu baada ya mwaka maana anatumika vilivyooo
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom