Ajira Mpya 4300 Mbioni Kutolewa na serikali

guzman_

JF-Expert Member
Jan 27, 2016
1,268
2,310
Habari za wikend mabibi na mabwana
Ajira Mpya ziko mbioni kutangazwa.

=====

kairuki%283%29.jpg

Zaidi ya watumishi 4,300 wapya wanataajiriwa kuajiriwa katika kada ya elimu na wasanifu wa maabara ambapo ajira hizo mpya zinakuja bada ya kukamalia kwa zoezi zima la kuhakiki watumishi hewa.

Hayo yamebainishwa mkoani Tabora na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma Mh. Angela Kairuki, wakati akizungumza na watumishi na wanachuo, ambapo amesema kuwa, kwa muda mwingi taifa limekuwa likikabiliwa na changamoto ya watumishi hewa huku likipoteza fedha nyingi.

Adha Mhe Kairuki amesema kuwa kamwe serikali haitamvumilia mtumishi ambaye atabainika kuwa na vyeti feki, huku akiwataka watanzania kutambua madhara ya vyeti hivyo kuwa ni kutopatikana kwa huduma stahiki huku akiwataka wahitimu katika kada mbali mbali kutowaonea haya watu ambao wanataka kupora ajira za wenzao.

Chanzo: ITV
 
Muwe mnaangalia na tarehe zenyewe anaweza akakana kulingana na siku hii ya leo
 
Kama majina yaliyotolewa yalikuwa 3,079 pekee, ndo wanasubiri hata wale waliomaliza nyuma ya 2015 wahakikiwe! Ikizingatiwa mwisho wao kutuma vyeti ni juzi 30/03/2017. Huu ni ujinga wa kiwango cha standard gauge!
 
nitapigwa BAN na nitajikuta central.. ila hii serikali tuseme ukweli hamna kitu!
 
Kuhusu walimu wa sayansi na hisabati na mafundi sanifu wa maabara, tulikuwa tunasubiri walimu waliomaliza nyuma ya 2015 wamalizie kutuma maombi yao hadi 30/03/2017. Kimsingi ni wachache sana. Hivyo maombi yao tunayafanyia upembuzi yakinifu ili tuweze kutoa ajira kwa pamoja.
Tunaomba subira yenu kama mlivyoionesha kwa kipindi chote cha takriban miaka miwili toka mlipomaliza masomo yenu mwaka 2015. Kufikia Jumatano ya wiki hii tutakuwa tumemaliza na kutangaza ajira mpya.

jumatano gani mkuu
 
Habari za wikend mabibi na mabwana
Ajira Mpya ziko mbioni kutangazwa.

=====

kairuki%283%29.jpg

Zaidi ya watumishi 4,300 wapya wanataajiriwa kuajiriwa katika kada ya elimu na wasanifu wa maabara ambapo ajira hizo mpya zinakuja bada ya kukamalia kwa zoezi zima la kuhakiki watumishi hewa.

Hayo yamebainishwa mkoani Tabora na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma Mh. Angela Kairuki, wakati akizungumza na watumishi na wanachuo, ambapo amesema kuwa, kwa muda mwingi taifa limekuwa likikabiliwa na changamoto ya watumishi hewa huku likipoteza fedha nyingi.

Adha Mhe Kairuki amesema kuwa kamwe serikali haitamvumilia mtumishi ambaye atabainika kuwa na vyeti feki, huku akiwataka watanzania kutambua madhara ya vyeti hivyo kuwa ni kutopatikana kwa huduma stahiki huku akiwataka wahitimu katika kada mbali mbali kutowaonea haya watu ambao wanataka kupora ajira za wenzao.

Chanzo: ITV
Hizi mbio naona haziishi
 
Back
Top Bottom