Ajira kwa sasa zinatenganisha familia, Wanandoa wanaishi sehemu tofauti

amigod

JF-Expert Member
Mar 10, 2018
345
264
Kwenu wana JF habari za hapo ulipo

Niende kwenye mada miaka ya nyuma kulikuwa na utaratibu wa kuwaunganisha watumishi wana ndoa kuwa mume/mke alipata uhamisho wa kumfuata mwenza wote wakawa watumishi na wanafamilia

Kwa sasa imesitishwa kwa kipindi kirefu hali inayopelekea watoto kulelewa na mzazi mmoja na wanandoa hawa wanaingia majaribuni kwa kukutana mwezi mmoja katika mwaka

Mimi ninaomba kwa wanao husika waangalie upya jambo hili pia namuomba mheshimiwa Rais asaidie katika hili kwani waathirika wapo wengi. (Ndoa na iheshimiwe na kila mtu)

Kuwatenga sababu ya ajira zao sio haki yao pia ni kukiuka maagizo ya Mungu mnao husika tafakarini upya
Aksante nawasilisha
 
Unataka arudishe serikali Dar es salaam?.

Ni mawili kazi au ukae na mkeo mtizamane nyumbani
Mbona yeye mzee baba ameshindwa kuhamia Dom sababu mama yake anaumwa?

Ni watumishi wangapi wenye matatizo ya dizaini hio wamelazimishwa kuhamia Dom?

#Ubinadamu kwanza.
 
Mbona yeye mzee baba ameshindwa kuhamia Dom sababu mama yake anaumwa?

Ni watumishi wangapi wenye matatizo ya dizaini hio wamelazimishwa kuhamia Dom?

#Ubinadamu kwanza.
Ss hilo muulize yeye mwnyw watu wanakufa na tai shingoni saivi
 
Muajiri hatambui ndoa, anachojali kazi zake zifanyike. Kuna maeneo mengine ya kazi ni magumu huwezi kwenda na familia kuishi huko, pia kuna suala la wanandoa wote kuwa na ajira tofauti, labda ufanyike utaratibu wa kuwapangia kazi eneo moja au jirani wanandoa
 
Mbona uhamisho bado unaruhusiwa..mke yupo Dom mume omba uhamisho ukaungane na mkeo

Mume yupo Dom mke omba uhamisho ukaungane na mkeo

Mkiona vyote haviwezekani Kila mmoja abaki kwenye mkoa wake na mkishindwa zaidi acheni Kama mnyoane vuvu
 
Pumbavu!
 
Nilijua mke wangu ananidanganya anataka kutoka k’njaro kuhamia Dom lakini anaambiwa asubiri uhamisho umesitishwa.
 
Zamani ndo ilikuwa tatizo lkn kwa sasa sio hivo, kwa sasa watumishi wa kutosha wapo mmoja akiomba ruhusa ya dharula hakuna kitakachokwama kazini, pili watumishi wanavipato vya kutosha kusafiri kila wakati ili kuudumia familia zao.
 
Ndugu hili jambo inategemea, mfano, mtumishi aliyeko labda Mtwara mfno kama mwalimu/ muuguzi hawezi kuwa na uwezo wa kuzulu familia yake mara kwa mara iliyoko kule Kagera/Arusha. Kwa kuwa serikali inasuasua kwenye uhamisho wa watumishi nadhani inapaswa ije na njia mbadala ya kuondoa kero hii. Pia jambo hili limeimarisha nguzo ya RUSHWA japo Tamisemi ilikana hili jambo ila huo ndo ukweli, watu wengi wamehonga wakahamishwa, wengine wakatepeliwa pia. Lakini bila serikali kuliwekea utaraibu ulio wazi na kuusimamia basi watumishi hawa wataendelea kuhonga maana wanauhitaji kweli.
 
Huyo unaemuomba aingilie kati ndie muasisi wa vurugu uliyoielezea hapa. Wasichokijua hawa watawala ni kuwa mfanyakazi alietenganishwa na familia yake hawezi kuwa motivated kufanya kazi anayotarajiwa aifanye. Halafu gharama za maisha zinaongezeka bila ulazima wowote kwa kuwa mfanyakazi analazimika kuhudumia nyumba mbili.
 
msijali tunawaletea treni ya kasi,, mtalala na wake zenu dar asubuh mtaenda Dom kazin,jion mtarud kwenye familia zenu. Cc msiba
 
Back
Top Bottom