Ajira katika Shule za Jumuiya ya Wazazi- CCM

Kitanga

Senior Member
Oct 17, 2012
198
250
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi amatangaza kiama kwa walimu wasio wanachama wa CCM? Hivi ni busara kweli kulazimisha walimu wa shule hizo kuwa na itikadi ya CCM? Je, ni watoto wa wana CCM ndiyo wanasoam shule hizo tu au ni kukosa kazi ya kufanya ndo maana anatoa maneno haya? Nawasilisha kwa mjadala.


SOURCE: Gazeti la Nipashe Ijumaa 23, Novemba, 2012
Vigogo wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliojimilikisha mali za jumuiya hiyo wametakiwa kujisalimisha wenyewe na kuzirudisha kabla hawajapelekwa mahakamani.


Hayo yalielezwa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Abdallah Bulembo wakati wa sherehe za kupongezwa na wajumbe kwa kushika wadhifa huo.


Bulembo alisema kuna baadhi ya watu wamechangia jumuiya hiyo kufilisika kuliko jumuiya ya UWT na UVCCM zote za chama hicho kwa kujichukulia mali na kujimilikisha.


Alionya kwamba mtu ambaye anaona hawezi kufanya kazi kwa uadilifu na kufuata masharti ajiuzulu mapema kabla ya kuachishwa kazi.


“Walimu wote waliopo chini ya jumuiya hii sharti wawe CCM na kama kuna mwalimu aliyepo chama kingine ajiuzulu mapema na kesho tutafanya ziara katika baadhi ya shule za hapa Dar es Salaam,” alisema Bulembo.


Naye Makamu Mwenyekiti wa Wazazi wa Jumuiya hiyo, Dogo Idd, alishukuru kwa kumchaguliwa tena kwa kipindi kingine cha miaka minne.


Aliwaomba kuondoa ubinafsi, ukabila na udini na kwa kufanya hivyo kamati yao itasonga mbele kwani jumuiya hiyo ni kubwa na inahitaji ushirikiano ili kufikia lengo.
 

Magwangala

JF-Expert Member
Oct 4, 2011
2,103
2,000
Kwanza walimu wenyewe wanaofundisha katika shule hizi wengi hawana sifa na pia hujitolea na kulipwa posho kidogo huku wakifarijiwa na kulimiwa mashamba yao na wanafunzi,Bulembo hapa anabwabwaja tu!
 
Top Bottom