Ajira 6,000 za walimu zagubikwa na utapeli. Waziri Ummy amuagiza Katibu Mkuu kufanya uchunguzi

Hili suala wanapewa ajira kwa wanaojitolea tu ni rushwa hili mama angalia hili.inakuwaje mnasema ambao hawana ajira wajiajiri wenyewe.watu wamejiajiri wakisubiria ajira ,na sasa wanaambiwa ajira hakuna ila kwa wanaojitolea tu.hili suala litasababisha rushwa kufanyika.
Rushwa, undugu na kujuana ndivyo vimetamalaki katika zoezi la ukusanyaji taarifa za walimu wanaojitolea hata majina yaliyotumwa tamisemi mengi yamejaa udanganyifu. Mathalani kuna watu wamejitolea kwa miezi kadhaa lakini kwenye ripoti wameandikiwa wamejitolea kwa mwaka mmoja na zaidi. Wengine baada ya kusikia kuna zoezi la ukusanyaji taarifa za walimu wa kujitolea wameenda kwa walimu wakuu na maafisa elimu kata kuongea nao kiutu uzima na majina yao yametumwa. Kwaiyo ata kama tamisemi wataamua kuajiri wanaojitolea wajue kabisa kuna ubatili mwingi umefanyika kwenye taarifa walizotumiwa
 
Waziri Ummy ameyasema hayo mapema hii leo wakati akiwa katika ziara ya kikazi katika Shule ya Sekondari Zingibari Wilayani Mjinga, Tanga
Mmmh...!

Is it a typing error au ni mimi mwenyewe nimepitwa na wakati...?

Hii wilaya ya "MJINGA" iliyoko huko TANGA, ni mpya, au...?

Imeanzishwa lini aisee?

Sijawahi kuisikia. Ndo tu naanza kuisikia leo toka kwako...!!
 
Mmmh...!

Is it a typing error au ni mimi mwenyewe nimepitwa na wakati...?

Hii wilaya ya "MJINGA" iliyoko huko TANGA, ni mpya, au...?

Imeanzishwa lini aisee?

Sijawahi kuisikia. Ndo tu naanza kuisikia leo toka kwako...!!
Ni mkinga sio mjinga. Just a typing error!
 
TAMISEMI wao wenyewe ndio wanaotengeneza hili tatizo la rushwa kutokana na vipaumbele vyao ktk utoaji wa ajira. Hiki kipaumbele cha kujitolea ni hatari sana ni mwanya mkubwa Sana wa rushwa n vyema kingeachwa mara moj

Mfumo mzuri usio na makandokando ambao hata huko nyuma ulitumika ni ule wa "FIRST OUT, FIRST IN" yani unaajiri Kwanza waliowah kumaliza zen unafata wanaofatia kwa mwaka mwingne.

Faida za mfumo huu ni; Kwanza, kuondoa mwanya wa rushwa.
Pili, anayepata na aliyekosa wote wanakuwa kitu kimoja na kuona haki imetendeka maana aliyekosa ataona ni wazi kabisa aliyepata ni aliyemtangulia kumaliza mafunzo.
Tatu, kwakuwa taratibu za kuajirika ni mwisho miaka 45 kufata mfumo huu ni vizuri maana hutoacha mtu kuliko kutumia mifumo mingne huenda mtu fulani akawa anakosa tu hadi kufikia umri wa kutoajirika tena.
 
Hizi nafasi inabidi wawe makini sana,mfano zile nafasi 8000,jina mmoja lilirudia karibia page 18,sasa hii inapelekea walimu wasiokuwa na ajira takribani 17 wakose nafasi
 
Mama yangu anapenda ziara za Tanga huyu!

Mama Samia kama kuna kitu unatakiwa kupambana nacho kimoja wapo ni hii ya kila kiongozi kuweka kwao mbele. Awamu ya 5 viongozi walizoea sana makwao, Majaliwa na Magu walikuwa hawaishi Ruangwa na Chato respectively
Ndiyo madhara ya mbunge kuwa waziri at the same time
 
Faida za mfumo huu ni; Kwanza, kuondoa mwanya wa rushwa.
Pili, anayepata na aliyekosa wote wanakuwa kitu kimoja na kuona haki imetendeka maana aliyekosa ataona ni wazi kabisa aliyepata ni aliyemtangulia kumaliza mafunzo.
Kwa kuongeza tu ni kwamba hii iwe digitized
 
Back
Top Bottom