Ajira 5000 za Hayati Magufuli zimepotea, ajira 6,000 za Rais Samia hazieleweki. Sasa hivi tunazungumzia ajira 12,000 bajeti ijayo

KUTATABHETAKULE

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
3,223
2,000
Utaajiri bila bajeti mkuu achana na wanasiasa wanaongea kutafuta kupendwa ila kwa ground mambo tofauti serikali aijatenga bajeti utaajiri alafu uwalipe nini
Tulilijua hilo. Ajira za amri tu ni uongo wa kutupa. Hizi ni pamoja na zile za jeshi. Ni njia ya kuudanganya Umma kwa kujua kwamba baada ya muda unasahau na pia kuahirisha matatizo kwa kudhania yatajitatua yenyewe.
 

Samiaagain2025

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
1,776
2,000
Tulibaki na kipolo Cha walimu 5000+ kutoka kwenye ajira 130000 za mwaka jana.Ila baada ya Rais Magufuli kufariki zimeyeyuka.

Tukubali kuwa hatuna viongozi wenye busara na uwezo wa kuongoza.

NB: Kidumu chama Cha mapinduzi(CCM).
 

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
8,450
2,000
Tanzania ni nchi ambayo ajira imegeuka kama jamari yaani ni mchezo wa kubahatisha sana.
 

balimar

JF-Expert Member
Sep 18, 2015
6,163
2,000
Jiajili tuukiona viongozi hawawezi tena na hawana uwezo

Sasa wewe mwenyewe uwatukane na kuwatweza halafu waje wakuajili. Haiwezekani
 

Dayone

Member
Aug 24, 2017
75
150
Hii tuhuma inamhusu Waziri mkuu Majaaliwa mwenyewe maana alisikika bungeni akisema ajira hizi (5000) wamesha maliza kupanngia watu vituo vya kazi, watu tumesubiri watoe majina lakini mpaka dakika hii comment hii inaenda hewani hamna majina na mbaya zaidi Watanzania nasi tupo kimya. Hawa viongozi wanatuona wapumbavu ndio maana wanafanya wanachojisikia, ajira hizi ni haki yetu ya msingi kwa maana pesa za kutulipa tuwapo kazini hazitoki mifukoni mwenu (viongozi) ni kodi ya watanzania!!! Waziri mkuu tunaomba ufafanuzi juu ya ajira hizi zimeishia wapi?
 

LIMBOMAMBOMA

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
9,128
2,000
Kitendo Cha JPM kuharibu uwekezaji na sekta binafsi kimeharibu mfumo mzima wa ajira kwa nchi yetu.Hivi inakuwa nafasi 6000 za walimu zigombewe na watu 120000 na huku viongozi wafurahie? Hili Ni tatizo kubwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom